Pal Schmitt
Hakuna ubishi kuwa Tanzania ina mawaziri wengi wanaotuhumiwa kughushi shahada zao. Hawa wanapaswa kuiga mfano wa rais wa Hungary ambayo alijiuzulu baada ya kugundulika kuwa aliiba maneno ya wengine kwenye wakati akiandika tasnifu kwa ajili ya shahada yake ya PhD. Kitendo hiki kilimfanya anyang'anywe shahada hiyo pamoja na kujiuzulu urais. Je hawa wetu waliotuhumiwa tena miaka mingi wanangoja nini? Wanaotuhumiwa ni Makongoro Mahanga, Mary Nagu,William Lukuvi, Emanuel Nchimbi na baadhi ya wabunge. Je hawa waharifu wanawachukulia watanzania kuwa mataahira kuendelea kuwa kwenye ofisi zao?
1 comment:
Kama wanavyosema Waingereza, "Not bloody likely!" Rais mwenyewe ana Phd lundo za usanii!
Post a Comment