The Chant of Savant

Tuesday 24 April 2012

Hivi tatizo la Pinda ni uroho au upogo?

Image DetailRais Kikwete akiongea huku Pinda akikenua kama mwanafunzi mbele ya mkuu wa shule
Hakuna ubishi kuwa waziri mkuu Mizengo Pinda hakuwa chaguo la rais Jakaye Kikwete kama waziri mkuu bali kiraka baada ya kutimliwa kwa swahiba na mshirika wake mkuu Edward Lowassa. Tangu Pinda apachikwe hapo alipo amekuwa akidhalilishwa sana kiasi cha kuonekana kama dodoki au hata nepi ya Kikwete. Kila linapotokea tatizo lenye kutaka lawama, lazima Pinda atapelekwa kule ili azidi kujiishia. Mojawapo ya mambo yaliyothibitisha kuwa Kikwete anamtumia Pinda vibaya ni sakata la mgomo wa madaktari na hili la Bunge na baraza lake la mawaziri.
Maskini Pinda alijitutumua kuwa alikuwa amewabana mawaziri wapatao nane waandike barua za kujiuzulu. Wakati huo  Kikwete alikuwa Brazil. Aliporudi akasema wazi kuwa hakubaliani na juhudi za Pinda. Baada ya Kikwete kunusa upepo aliishia kutoa kanusho la habari iliyohusiana na msimamo wake. Wengi walishangaa kuona Pinda akidhalilishwa hivi. Pia wengi walishangaa ni kwanini Pinda amejiruhusu kutumika kama nepi. Wengi wanashangaa ni kwanini Pinda ameendelea kuvumilia upuuzi huu. Je tatizo la Pinda ni uroho au upogo?

No comments: