How the Berlin Conference Clung on Africa: What Africa Must Do
Friday 27 April 2012
Tumpongeze Maige kabla ya kumsulubu
Taarifa ya kufumka siri za utajiri wa kutisha wa waziri kijana wa Maliasili na Utalii Ezekiel Maige zinapaswa kutufanya tumpende na ikiwezekana tumsaidie kumfikisha mbele ya vyombo husika ingawa vyombo vyenyewe vinatia shaka.
Kwanza, Tanzania ina akina Maige wengi kiasi cha kushindwa hata kujua idadi yao. Tuwape mfano, hao vijana wengi mnaowaona Mipakani, Viwanja vya ndege, Uhamiaji, Benki kuu, Bandari, mita za mafuta na kwingineko ni akina Maige sema hawajafichuliwa.
Pili akina Maige wana wazazi wao waliowatengeneza. Hawako peke yao hawa. Wanaweza kufanya kila watakalo kuuza wanyama, unga, madini hata watanzania na hakuna anayewagusa. Hii ndiyo siri ya kila kitu nchini kujiendea bila yeyote kujali hasa uhujumu na ufisadi.
Kama vijana kama Maige wana ukwasi kiasi hicho, hao baba zao wana ukwasi kiasi gani? Hapa hatujaongelea wale wageni wetu akina Chavda ambao Idd Simba aliwahi kusema kumi tu wanamilki uchumi wa Tanzania. Kimsingi hao ndiyo wenye fweza maana akina Maige ni vijikuadi na limbukeni vinavyohongwa kupitisha mizigo na mambo ya wakubwa wenyewe. Tumpongeze Maige kabla ya kumsulubu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment