How the Berlin Conference Clung on Africa: What Africa Must Do

How the Berlin Conference Clung on Africa: What Africa Must Do

Monday 16 April 2012

Vasco da Gama na Imelda Marcos wako Brazil huku Millya akiachia ngazi kwa kuukosa ubunge wa EALA


Vasco da Gama na Imelda Marcos wakishuka kwenye uwanja wa ndege wa Sao Paulo

Aliyekuwa mwenyekiti wa UVCCM Arusha ambaye ameachia ngazi baada ya kuukosa ubunge wa Bunge la Afrika Mashariki. Ametoboa siri kuwa kumbe vijana wengi wanaendelea kubaki CCM wakitegemea kupewa ama ukuu wa wilaya au mkoa. Kumbe ni waathirika wa ufisadi! Kweli mwaka huu tataona mengi kama siyo kusikia.

Pamoja na kupigiwa kelele kuacha ziara zisizolingana na hali ya uchumi wetu, rais Jakaya Kikwete aka Vasco da Gama na mkewe Salma aka Imelda Marcos wako Brazil kujivinjari. Ameandamana na watu wangapi na wa aina gani? This is top secret. Kwanini deni la taifa lisiumke? Baada ya kuona nafuu ya Kanumba inapungua, ametafuta tukio jingine la kukwepa aibu kama kawa! Kweli yetu ni Danganyika! Anavyojipelekapeleka, hakuna hata rais mwenzake kumpokea! Ama kweli tumepata watawala baada ya kiongozi wetu Mwalimu Nyerere kututoka.

No comments: