How the Berlin Conference Clung on Africa: What Africa Must Do

How the Berlin Conference Clung on Africa: What Africa Must Do

Tuesday 17 April 2012

Wakati Tanzania tukigawa mali zetu Argentina wataifisha


Image Detail
Rais Fernandez pichani

Rais mpya wa Argentina Cristina Kirchner Fernandez ameamua kutaifisha kampuni kubwa ya mafuta nchini humo ya YPF oil baada ya kugundua kuwa wawekezaji wa Kihisipania waliinunua na kuiua kampuni husika kama ambavyo tumeshuhudia nchini Tanzania.
Baada ya kutaifisha kampuni ya YPF Oil, nchi nyingi hasa zinazounga mkono Hispania zilitoa tishio kuwa hatua hii ingeogofya wawekezaji hivyo kuathiri uchumi wa nchi. Rais Fernandez aliwajibu kwa kusema, " Huyu rais  hatapoteza muda kujibu matishio yoyote... kwa sababu ninawakilisha watu wa Argentina." 
Rais aliongeza, " Mimi ni mkuu wa nchi na si jambazi."  Laiti rais wetu mpenda kugawa gawa mali zetu angekuwa na lau nusu ya ujasiri wa mama huyu! Majambazi wa EPA na Dowans wasingeweza kumweka mfukoni mtu kama huyu.  Uzuri ni kwamba alichaguliwa kidemokrasia na si kwa hongo wala uchakachuaji au kuhonga pesa ya wizi kama ile za EPA.

No comments: