How the Berlin Conference Clung on Africa: What Africa Must Do

How the Berlin Conference Clung on Africa: What Africa Must Do

Tuesday 24 April 2012

Kama wabunge wako serious, they must go for Kikwete

Image Detail
Hali ilivyo nchini kuhusiana na kuibuka kwa kashfa ya ufisadi wa mabilioni  kiasi cha wabunge kutaka baadhi ya mawaziri wawajibike au wawajibishwe ni tete. Kwa mambo yanavyokwenda, ni kwamba rais Jakaya Kikwete anaonekana kuwalinda watu wake kama kawa. Ingawa ofisi yake ilikanusha habari zilizoripotiwa na gazeti la Tanzania Daima kuwa Kikwete alikuwa amepiga chini mipango ya waziri mkuu Mizengo Pinda kutaka wahusika wajiuzulu, hali inaonyesha ni kweli Kikwete atawanusuru watu wake. Ili kuondoa  aibu na balaa kwa taifa, wabunge wanapaswa kuachana na mipango ya kuwalazimisha mawaziri shutumiwa au waziri mkuu Pinda kuachia ngazi. Badala yake, wamshughulikie Kikwete mwenyewe. Hapa tatizo si wabunge wala mawaziri bali Kikwete. Tatizo litakuwa wabunge kama wataendelea kulialia badala ya kutumia mamlaka waliyopewa na wananchi kumwajibisha Kikwete. So if MP are really serious, they must go for Kikwete instead of Pinda and other suspected ministers.

No comments: