The Chant of Savant

Tuesday 10 April 2012

Watanzania rejeeni kwenye mambo muhimu

Ingawa tumesikitishwa na kifo cha Steven Kanumba, kuna haja ya kuuangalia ukweli kama ulivyo. Pamoja na kupewa heshima kubwa kuliko hata aliyostahiki kutokana na wakati wa kifo chake, sasa basi turejeeni kwenye mambo muhimu. Tumefanikiwa kuuonyesha ulimwengu kipaumbele chetu hasa kujali sana usanii kuliko uchapakazi. Najua wengi hawatapenda mawazo haya. Ukweli ni kwamba nimeshangaa kuona Kanumba akishabikiwa na viongozi kuliko hata marehemu makamu wa rais Omar Juma. Kunani? Je hii ni sawa? Sikuona rais, kwa wakati tofauti na mkewe, na vigogo wengine wakimiminika kwenda kwenye msiba wa Omar Juma kwa spidi kama hii. Hakika Tanzania ni nchi ya wasanii.
Bwana alitoa Bwana amechukua. Maisha yanaendelea. Turejee kwenye kupambana na ufisadi, usanii, uvivu na urongo basi. Au siyo?

4 comments:

Malkiory Matiya said...

Kifo cha Kanumba kimeniachia fundisho na hasa kwa wanasiasa wetu wapenda sifa na watafuata umaarufu wa kisiasa. Nilikuwa nasubiri Kanumba afikishwe kwenye nyumba yake ya milele halafu niandike a short article. Muda ukiniruhusu nitafanya hivyo karibuni.

Malkiory Matiya said...

Mkuu, article niyoahidi hapo juu imeshaiva naimeshaingia hewani ndani ya www.malkiory.com. Kazi kwako! kuiperuz.

Malkiory Matiya said...

http://www.malkiory.com/?p=2467

Jaribu said...

Inasikitisha. Ni kikombe cha babu cha mwaka huu