The Chant of Savant

Friday 27 April 2012

Taarifa ya Kamati Kuu ya CCM changa jingine la macho


Balozi mpya wa Tanzania nchini Ubelgiji Diodorus Kamala akiongea na Rais Jakaya Mrisho Kikwete ikulu jijini Dar es Salaam wakati balozi huyo alipokwenda kumuaga.
Taarifa iliyotolewa kuhusiana kikao cha dharura cha Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) yaweza kuwa usanii mwingine kama ukiisoma kipengele baada ya kingine. Kwa ufupi ni kwamba eti Kamati imeridhia shinikizo la wabunge kutaka kuwawajibisha mawaziri mafisadi. Ajabu taarifa hiyo haitoi muda wa utekelezaji wa hatua hii muhimu! Pili Kamati inaposema eti utekelezaji ufanywe mapema iwezekanavyo inamaanisha nini? Ajabu Kamati kuu haijapendekeza wahusika kufikishwa mbele ya vyombo vya sheria. Kutofanya hivyo ni sawa na kuwakingia kifua wahusika.Kimsingi, hata kama Kikwete atafanya mabadiliko ya baraza la mawaziri, kuna mambo makuu mawili au matatu yatajitokeza. Mosi, ataondoa uoza na kuweka uoza maana CCM yote imeoza. Pili atawarudufu (recycle) makapi yaliyotajwa kwa kuwapa nafasi nyingine nono kama vile ubalozi kama alivyofanya kwa aliyekuwa katibu mkuu wa wizara ya Maliasili na Utalii, Ladislaus Komba ambaye alimteua balozi nchini Uganda au akina Adadi  Rajabu ambaye ni balozi Zimbabwe pamoja na kuvurunda kote.
Jikumbushe makapi aliyorudufu rais. Diodrous Kamala, Dk. Batilda Burian, Philip Marmona Mwantumu Mahiza. Hapa hujagusia watuhumiwa wegine wa ufisadi kama Mwanaidi Majaar balozi wa Tanzania nchini Marekani au Peter Noni, mkuu wa Benki ya Uwekezaji (TIB) ambao wanajulikana wazi wazi walivyoshiriki kwenye wizi wa EPA iliyomwezesha kuingia madarakani kwa njia ya rushwa na uchakachuaji mkubwa.
The Tanzanian ambassador to the U.S. talks about how increasing economic ties could benefit both countries. -

Kamati Kuu iliyokutana leo tarehe 27/04/2012 chini ya Mwenyekiti wake Mhe. Dr. Jakaya Mrisho Kikwete Jijini Dar es salaam, pamoja na mambo mengine imefanya yafuatayo.;

A. UTEUZI
Kamati Kuu imeteua wafuatao kuwa makaimu Katibu wa mikoa. Vituo vyao vya kazi vitapangwa baadae. Uteuzi huu unatokana na kuwepo kwa mikoa wazi mitano, mikoa hiyo ni;

Geita
Njombe
Simiyu
Katavi
Magharibi
Hivyo wafuatao wameteuliwa kuwa makaimu katibu wa CCM wa Mikoa.

1. Ndg. Hilda Kapaya
2. Ndg. Shaibu Akwilombe
3. Ndg. Hosea Mpangile
4. Ndg. Alphonce Kinamhala
5. Ndg. Aziz Ramadhani Mapuri

B. HALI YA KISIASA:
Rais amepokea taarifa na maazimio ya Kamati ya wabunge wa CCM na Kamati ya uongozi ya wabunge wa CCM juu ya kilichotokea kwenye bunge lililopita mjini Dodoma.

Taarifa hizo zimewasilishwa kwenye kamati kuu na kujadiliwa. Pamoja na taarifa hizo kamati Kuu imepokea taarifa ya jinsi Rais alivyojipanga kuchukua hatua za kuwawajibisha mawaziri na watendaji wa serikali na wale wa mashirika ya umma waliobainika kuhusika na ubadhirifu ulioinishwa na taarifa ya Mkaguzi na mdhibiti mkuu wa hesabu za Serikali, Kamati za kudumu za bunge na wabunge bungeni.

Kamati Kuu imeamua yafuatayo;
1. Kamati Kuu inatambua na kuheshimu haki na wajibu wa wabunge kujadili utendaji wa serikali yao.Inapongeza juhudi za serikali kuhakikisha kuwa ripoti ya mkaguzi na mdhibiti mkuu wa hesabu za serikali inajadiliwa kwa uwazi na hivyo kuibua mapungufu yaliyojadiliwa.

2. Kamati Kuu imeridhika na imebariki uamuzi wa Rais KULISUKA UPYA BARAZA LA MAWAZIRI na taasisi zingine zilizoanishwa katika ripoti hizo. Imesisitiza utekelezaji wa uamuzi huo ufanywe mapema iwezekanavyo.

Aidha kamati Kuu imeipongeza Kamati Teule ya baraza la wawakilishi Zanzibar iliyoundwa kuchunguza utendaji katika sekta mbalimbali kwenye serikali ya mapinduzi Zanzibar kwa taarifa yao.

Kamati Kuu inawapongeza wajumbe wa Baraza la Wawakilishi kwa jinsi walivyojadili taarifa hiyo na pia Kamati Kuu inaipongeza Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kwa kuipokea taarifa na kuanza kuifanyia kazi.


Nape Moses Nnauye
Chama Cha Mapinduzi
The Ideology and Publicity Secretary

No comments: