The Chant of Savant

Wednesday 25 April 2012

Taifa linaomba eti lahitaji kuombewa!


Wanohitaji kuombewa wawezaje kuliombea taifa?





Je tatizo ni maombi au maadili?
Je kuomba ni jibu au sehemu ya tatizo?
Kura tunaomba
Misaada tunaomba
Haki tunaomba
Kila kitu tunaomba
Kweli sisi ombaomba. 
Kwa sasa wamejitokeza matapeli wengi wanaotaka kuwa karibu na watawala ili wafaidi mabaki ya ufisadi. Hawa si wengine bali wale wanaojiita viongozi wa dini wanaojua fika tatizo la nchi yetu kuwa ufisadi lakini wanalikwepa na kusema ni laana! Maana unaposema nchi inapaswa kuombewa badala ya kuambiwa ukweli kuwa utawala uliopo hauna visheni na ni wa hovyo, unamaanisha nchi yetu imelaaniwa. Kuna haja ya kuwaogopa hawa kama ukoma. maana nao ni sehemu ya tatizo. Tanzania aihitaji kuombewa bali kuwajibika na kutenda haki. Badala ya kuombea nchi shinikizeni watawala waache ufisadi na usanii.

2 comments:

Yasinta Ngonyani said...

nanunuu " Kuna haja ya kuwaogopa hawa kama ukoma. maana nao ni sehemu ya tatizo. Tanzania aihitaji kuombewa bali kuwajibika na kutenda haki. Badala ya kuombea nchi shinikizeni watawala waache ufisadi na usanii." mwisho wa nukuu:- Nakubaliana kabisa tunahitaji kuwajibika sio kila kukicha kuomba omba. Kuna wakati wa kuomba na wakati wa kujikakamua....

Ndugu Nkwazi N Mhango said...

Wow! Da Yacinta, habari za siku nyingi? Nadhani sasa unafaidi spring ksma sisi. Nashukuru kwa kunitembelea na kuacha unyayo.