Kuna wanadoa tena wengi tu wanaonekana wakiishi nyumba, chumba, hata kitanda kimoja lakini kiukweli wanaishi mbali mbali. Kwa wanandoa, kuishi pamoja siyo kimwili tu bali kiroho, kimkakati, na kwa kila kitu kiwe kikubwa au kidogo. Ni kujenga utegemeano na ushirika usiyoyumba au kuyumbishwa kama mtaishi pamoja kiukweli. Mfano, kama mmoja au wote wawili mna siri ambazo wenzi wenu hamtaki wajue basi mnaishi nyumba au vyumba tofauti.
Yafuatayo yatakuonyesha kama mnaishi pamoja au tofauti:
Mosi, kama hamuaminiani mjue mnaishi mbali mbali, na kuishi hivyo, kuna madhara makubwa na fichi ambayo mojawapo ni kuachana au kutengana. Kimsingi, ndoa huanza na upendo. Kwani, bila kumpenda mtu, huwezi kumuoa au kuolewa naye. Na upenda si kusema nakupenda bali kutenda na kuuonyesha upendo katika kila jambo. Upendo pia huleta ubora na upekee baina ya wawili. Baada ya upendo, kinachofuatia ni uaminifu. Bila vitu hivi, kila mnachofanya ni bure tu. Kuna siku kitaitafuna ndoa yenu.
Pili, kutoaminiana unaweza kuuona kwenye vitu kama namna mnavyotumia simu au tuseme mahusiano na mawasiliano yenu. Hivyo, kama mnafichana simu na vitu vingine, mjue mnaishi mbali mbali. Hapa, tusisitize. Hakuna jambo au mali ya mmoja peke yake bali vyote vyenu kwa usawa.
Tatu, japo ushindani ni jambo jema kama nia yake ni njema. Kama mnashindana shindaneni katika kutenda mema na kujengana na si kubomoana au si kwa lengo la kufanikiwa pamoja. Kama hamfanyi hivyo bali kushindana tu, mjue mnaishi mbali mbali. Maana, mashindano ya kila mtu na lake ni sawa na vita ambavyo lazima mmoja ashinde na mwingine ashindwe, lazima mmoja apate na mwingine apoteze. Nani analitaka au kulifanya hili akawa pamoja na yule anayeshindana naye? Hili, katika ndoa si jambo la kufanya au kuvumilia kwa sababu halivumiliki na madhara yake ni makubwa kwa wawili na hata familia kwa ujumla.
Nne, katika ushindani ambapo kila mtu anafanya hivyo kwa maslahi binafsi, lazima mbomoane. Nani aweza kujenga au kudumisha kitu kwa kukibomoa? Kinachotakiwa kwenye ndoa ni kujenga na kujenga na si kubomoa au kubomoana. Mjue. Kama mnabomoana, iwe kwa kujua au la, jua mnaishi mbali mbali ila athari na matokeo ya kufanya hivyo vitawarejesha pamoja kwa njia tofauti na mbali mbali. Ndoa ni kama baiskeli yenye magurudumu mawili. Moja likipata pancha, baiskeli haiweza kubeba chochote wala kupandwa.
Tano, upendo unapoisha, chuki huchukua nafasi. Kama mnachukiana, mjue mnaishi mbali mbali maana chuki si mojawapo ya ajenda katika viapo vyenu wakati mkiamua kufunga ndoa. Hakuna chuki inayojenga isipokuwa chuki dhidi ya mambo mabaya.
Sita, japo kila binadamu hukosea, kama mnakoseana bila kusameheana na kuombana radhi au kusuluhisha mgogoro wenu kwa njia chanya, mjue mnaishi mbali mbali.
Kitu kingine muhimu kuhusiana ndoa ni ukweli kuwa huleta ulinganifu, uchangamfu, upendo, na usawa kama inazingatiwa na kufuatwa inavyopaswa au mifarakano kama wahusika hawatakubali na kujua kuwa ndoa siyo kitu kinachopaswa kutenganishwa hata kidogo. Hata hivyo, tukiri.

Ndoa inapofeli, wahusika hukosa hayo hapo juu na wengi huishia kwenye majuto hata kujiondoa au kuondoa uhai wa wenzao japo si wote. Hii ndiyo siri ya kukithiri kwa mauaji, migogoro, na talaka vyote vikiwa hatarishi baina ya wanandoa hata watoto. Mfano inapotokea mmoja wa wanandoa akaamua kukatisha uhusiano na maisha yake, ya mwenzake, hata ya watoto, huacha majuto na msiba mkubwa tu. Hii, mara nyingi, hutokana na kutaka kulipiza kisasi baada ya wahusika kukataa au kushindwa kukubali ukweli kuwa mahusiano yao sasa ni hatarishi na hauwezi kuendelea.
Katika uzoefu wetu kama wanandoa wakongwe tumegundua kuwa hakuna kitu kinawaweka mbali wanandoa kama kufanya hayo hapo juu.
Mwisho, ushingae kujikuta kuwa wewe na mwenzio mnaishi mbali mbali japo mnaishi chumba, nyumba, na kitanda kimoja. Kuepuka hili, lazima mjue viashiria na visababishi vya utengano huu ambao madhara yake ni makubwa kuliko mnavyoweza kufikiria au kujua. Yazingatie haya msiishi mbali mbali mkaishia kujuta.

Chanzo: Mwanachi J'pili iliyopita.
No comments:
Post a Comment