Mpendwa Fyatu Ticha Nchonga, salamu.
Samahani kwa kufyatuka na kukuvurugia amani na mapumziko yako. Salamu toka kwa Mada na Bi Mkubwa na mafyatu wote wanaokukumbuka.
Leo, ni kumbukumbu yako. Najua. Bado unanikumbuka pamoja na mafyatu kama tunavyokukumbuka na kukumiss fyatu mwenzetu mfyatuka na msifika aliyefyatuka akatenda makuu kuliko hata yeye mwenyewe? Nakukumbuka wewe uliyekufa japo una nguvu na udhu kuliko baadhi ya wanene wanaoishi japo wamekufa kiakili na kimaadili.
Fyatu Nchonga, kama fyatu mwenzetu wa kweli uliyechukia ufyatuaji wa wengine, tunakumiss kwa sana hasa pale tunapofyatuliwa na kila aina ya mafyatu hata wadudu baada ya kugoma kufyatuka hata kufyatuliwa na kuwafyatua watufyatuao tena wengi malimbukeni, mafwala, na mazwazwa. Japo umelala, naamini, roho yako haijalala, umefumba macho. Ya rohoni yanaona. Kama vyote havioni, matendo yako yanasema tena kwa sauti kuu kiasi cha kuwafyatua baadhi yetu hadi wakafyatuka na kukamia hata kuthubutu kuwafyatua wawafyatuao.
Japo umefyatuliwa kimwili, kiroho, wewe ni fyatu orijinali asiyesahaulika. Hivyo, niruhusu nifyatuke na kukufyatulia yafuatayo. Mengi yake yatakufyatua utamani kuamka na kufyatuka ili uwafyatukie wote wawafyatuao mafyatu wenzako.
Mosi, siishi kayani kwako. Niko ughaibuni kidogo nikifyatua mambo ili nirejee haraka nifyatuke na kufyatua wawafyatuao mafyatu wako. Nikishindwa, nitawafyatua wafyatuke na kuwafyatua wawafyatuao. Fyatuland tunakuenzi na kukumbuka kinomi. Kama munene na msemaji wa mafyatu wako uliowaacha wakafyatuliwa baada ya wewe kufyatuliwa, huwa nafyatuka na kusoma habari za kule. Mfano, mwezi wa kumbukumbu yako mwaka fulani, si watoi waliingiwa na roho yako fyatu. Iliwafyatua wakafyatuka na kutaka kuwafyatua wawafyatuao. We, acha! Kilifyatuka, kikanukishwa, na kikanuka usipime fyatu wangu.
Vitegemezi vilijaa na kufyatuliwa na roho yako ya ushujaa vikaijaza mitaa kwa kujifyatua na kujiamini kabla ya ndata na ndutu kuamriwa na kukubali amri za kikumbaff kuvifyatua bila aibu wala huruma wakati ufyatukaji wao ulilenga kuwakomboa hata wao. Ilikuwa patashika nguo kuchanika fyatu wangu. Vya moto vilifyatuka, kufyatuliwa, na kutembea katika kuwafyatua na kuwadedisha hawa mafyatu walioazimia na kukamia kuwafyatua wawafyatuao. Hiyo cha mtoto.
Juzi tu, alifyatuliwa fyatu mnene namba be na kutokomea. Can you believe? You better do. Japo huwezi kufyatuka ukaja kufyatua, naamini, unaniunga mkono kufyatuka na kufyatua haya niyafyatuayo ili yakufyatue lau uwaombee mafyatu wako wafyatuke na kuwafyatua wawafyatuao kama ulivyowaahidi wakati ukiondoka kwenda uliko. Mambo yamefyatuka na kufyatua. Sahau enzi za yule wako Abi Juu mbee. Huyu fyatu alifyatuliwa na akafyatuka kikwelikweli hadi mafyatu wako hawajui alikofyatuliwa na kwanini alifyatuliwa. Guess what.

Hakuna fyatu yoyote isipokuwa mimi anayefyatuka na kuongelea ufyatuzi huu wa kizwazwa. Huwezi kuamini. Hadi nafyatuka, mafyatu wamefyatuliwa na kukubali dhuluma hii na kuigeuza suala la kawaida lisahaulikalo haraka. Huwezi kuamini. Kuna mafyatu mazwazwa ambayo huamini kuwa wana hati milki ya kaya yako inayofyatuliwa kizwazwa.
Nani angejua kuwa kutakuja mafyatu ambao wanagejifyatua na kufyatua kila kitu ulicholinda kwa ukali wakikiweka mnadani hadi mafyatu wenyewe na hakuna anayefyatuka kuuliza kunani? Nakukmbuka ulivyoniasa. Sasa hivi, hakuna tofauti baina ya mafyatu na mifugo. Mafyatu wamefyatuliwa na kuufyata kiasi cha kutisha. Wamegeuka wadudu wa hovyo.

Natamani wafyatuke na kuwa kama nyuki lau wawafyatue wawafyatuao. Natamani waamke na kufyatuka wafyatue wawafyatuao wajue ufyatuaji una mwisho tena mwingine mbaya lakini wapi. Hakika, mafyatu wapo pakanga. Kuishi na haki vimefyatuliwa na kugeuka hisani.
Maadili yamegeuzwa madili. Ukweli umefyatuliwa na kugeuka uongo. Uchafu sasa ndiyo usafi na usafi ni uchafu. Halali imegeuka haramu ilhali uadilifu ukifyatuliwa na kugeuka uhalifu. Kila kitu kimefyatuliwa na kuwa kichwa chini miguu juu.
Walio uchi wanawacheka wenye nguo. Mataahira wanawazodoa wenye akili. Mashujaa wanang’ongwa na woga ilhali wasomi wakifyatuliwa na kupotezwa au kupotoshwa na mazwazwa. Huwezi kuamini. Watenda mabaya wanasifiwa ilhali watenda mema wakilaaniwa. Laana imefyatuliwa na kugeuka vibaraka na vikaragosi. Wabovu sasa ni wabora na wabora ni wabovu. Wenye heshima wanadharauliwa. Watakatifu wamefyatuliwa na watakakitu. Mfalme akiwa utupu, anasifiwa na ajifyatuaye na kusema yu utupu anapatilizwa. Woga umegeuka ushujaa na ushujaa na kujigongagonga ndiyo fasheni ya wachumia matumbo.

Ukifyatuka hovyo, hata ufyatue haki na ukweli vipi, unafyatuliwa. Vipofu sasa wanawaongoza wanaoona ilhali viziwi wakiwasikilizia wasikiao. Hakika ni wakati wa ngozi ya simba kuliwa na mchwa.
Mpendwa Nchonga, sikujua kuwa wakati mwingine dunia hufyatuka na kuwafyatua waliogoma kufyatuka hadi wakakubali na kushabikia kufyatuliwa. Sikujua kuwa kuna kaya ambapo fisi wanaaminiwa kuwalinda mbuzi. Sikujua kuwa mafyatu wangegoma kufyatuka na kufyatua hadi wezi wanalinda mali zao. Sikujua kuwa kuna siku makaburi ya watakatifu yatatunzwa na wanajisi. Du! Hivi niko wapi na nafanya nini? Ni kama mgoshi Machungi kishanipiga zongo! Acha nimtokee huko Mashindei.

Chanzo: Mwananchi J'tano leo.

No comments:
Post a Comment