Kuna jambo limeniudhi na kunifyatua hadi natamani nidedishe au kuweka manyani na manyang’au rupango kwa hasira. Japo hii jinai ilikuwa ikiendelea, umefika wakati muafaka kuifyatua na kutiokomeza. Mafyatu wangu mavivu na mazwazwa yanafyatuliwa na kuangamizwa na uzwazwa. Kuna ujambazi, utapeli, na wizi ambao umefyatuka na kuota mizizi Fyatulandi. Majizi na matapeli yanawafyatua mafyatu wangu waliogoma kufyatuka lau wakatumia japo commonsense achia mbali akili. Ipo mijambazi na mitapeli yenye uroho uliofichwa kwenye roho mtakakitu iitwayo mtakatifu inayofyatua mafyatu wangu kirahisi na kuishia kuwa matajiri wa kutupwa tena kizwazwa.
Hivyo, kukomesha jinai hii, natangaza rasmi leo. Hakuna ‘kufanya au kutenda miujiza’ Fyatuland. Nimechoka na ushenzi huu uchwara. Bila kufyatuka na kufyatua, mafyatu yangu mazwazwa na mavivu yasiyofyatuka hadi yanafyatuliwa kirahisi na matapeli na mazwazwa tena uchwara yawe ya kidini au kisiasa yataangamia naona. Lazima nifyatuke na kufyatua. Mafyatu yangu yanafyatuliwa kirahisi eti yaukate yanaishia kufyatuliwa na umaskini. Huu ni wizi na ujambazi wa mchana kweupe. Uliona wapi fyatu akatajirika bila kuchapa kazi au kutumia akili na ubunifu kama siyo ugonjwa wa akili unaoneemesha majambazi ya kiroho? Eti yanafyatuliwa kuwa yatakuwa matajiri kwa kuuziwa kila uchafu na upuuzi kama mafuta, vitambaa tena vinavyounuka jasho na mengine ndiyo yaukate. Mtakuja kuuziwa hata mavi. Mtafyatuliwa hadi mfe makapuku amkeni mfyatukeni na kufyatua kabla hamjaendelea kufyatuliwa.
Juzi, wakati nakata kalaji kuna fyatu alifyatuka na kunitolea uvivu. Aliniuliza inakuwajue lisirkal langu linafyata mkia wakati mafyatu haya majambazi yakitapeli na kuwafyatua mafyatu kana kwamba lisrikal langu halipo. Nilimjibu kuwa lisirkal langu ni la kifyatu. Hivyo, haliwezi kufyatuliwa au kuruhusu ufyatuliwaji wa mafyatu waliofyatuka wakaniamini maulaji ili niyafyatue. Kutokana na uvivu na uzwazwa, Fyatuland imegeuzwa shamba la bibi tena bibi mwenye kipofu na tahahira. Sasa natangaza rasmi, msinijaribu nikawafyatulia mbali wana hizaya nyie. Mali haiji kwa kuomba, kukopa, wala kubomubomu. Inakuja kwa kufyatuka na kuchapa kazi kinomi. Haiwezekani kaya inayoongoza na daktari mwenye magunia ya PhD za kusotea iendelee kufyatuliwa na mbumbumbu na matapeli kila aina.
Fyatu aliyejifyatua akanifyatua alidai kuwa nimefumbia macho matapeli wa kiroho kwa vile nami natumia unene kuwafyatua mafyatu waliogoma kufyatuka hadi wanaufyata kwa kila upuuzi. Nilimjibu kuwa si kweli na nilikuwa nafanya utafiti ambao umezaa hili tangazo muhimu kwa mafyatu na Fyatuland. Kuanzia sasa, atakayetangaza au hata kuwazia kutenda miujiza, namfyatua. Napeleka mswada kwenye kigwena wa kupiga marufuku hii jinai na usanii. Kwanini mafyatu wangu wafyatuliwe na kila tapeli awe wa kalamu au wa kitabu nami niiufyate kama yenyewe wakati ni msomi wa kupigiwa mfano? Kama kweli kuna miujiza, basi wahusika waende kwenye mahaspitali na zahanati wakatuonyeshe uwezo wao.
Ajabu ya maajabu, nimegundua kuwa matapeli wanatengeneza mabilioni ambayo, licha ya kutostahili, hayalipiwi kodi. Hivyo, kuanzia leo, hata kuhubiri lazima wahusika wakatwe kodi na tozo za kuwafyatua wenzao. Kwangu, hii si huduma bali hujuma. Natangaza rasmi kuwa hakuna fyatu aruhusiwaye kutupigia mikelele na kuwafyatua mafyatu wangu bila leseni. Naamuru wote waende wakachape kazi na kula jasho halali na siyo kuwaibia mafyatu wangu wajinga na mazwazwa wanaoamini katika kila upuuzi. Hakuna kaya duniani iliyowahi kujengwa kwa maombi na miujiza uchwara mfyatuke na kujua.
Haya matapeli uchwara yanapanga mafyatu wao kwenye halaiki wanazohubiri na kujifanya wametendewa miujiza wakati ni utapeli mtupu. Yanajiangusha na kupiga makelele ili kuwazuga na kuwafyatua mkenge mafyatu mazwazwa na mavivu ya kufikiri. Mtaliwa mkiona msipofyatuka na kushika ukweli kuwa hakuna miujiza zaidi ya kuibiana na kunyonyana. Yapo yanayodanganywa kuwa yanaweza kuombewa na kupona magonjwa au kumaliza matatizo yao. Mnafyatuliwa na kuongezewa magonjwa na matatizo kwa sababu ya uzwazwa na uvivu vyenu. Fyatukeni lau mtumie akili kidogo. Anayekufyatua atakufanyia miujiza anataka njuluku. Kama kweli anao uwezo huo, kwanini asijifanyie yeye mwenyewe kwanza? Kama kuna miujiza mnayofanyiwa siyo mingine bali kufyatuliwa bila kufyatuka na kuuona ukweli hata uwe mchungu.
Ninachukizwa na kuhuzunishwa sana namna mafyatu wa kaya nyingine wanavyotucheka wakituona manyumbu yasiyo na akili. Eti unataka uombewe. Kwani wewe maiti au ni kwa vile mmefyatuliwa hadi mnageuka maiti zinazotembea kiasi cha kufyatuliwa na kuchumwa kama mimea? Heri hata majambazi wa siasa. Wao wanakujaza ahadi na ujinga na kukufyatua. Japo, wote ni sawa, kuna haja ya kuwa wabunifu japo kidogo na kutumia akili na ubunifu.
Hakuna kinachouma kama kuona jamii nzima inageuka manyumbu na wapenda vya dezo na vya haraka. Wenzenu wanawacheka na kuwashangaa. Mbona huko nyuma hamkuwa hivyo hadi mnaliwa kama ujaka tena mkijiona kwa kugoma kufyatuka na kufyatua? Hakika, huu nao ni ufisadi wa kiakili.
Nihanikize na kumalizia. Ni marufuku na mwiko kutenda, kutendewa, au kutegemea miujiza Fyatuland. Mlishapewa akili, ardhi, mikono, na nguvu ili mchakarike na siyo kutegemea miujiza ruya senzi nanyambaff nyie kabisa. Mgosi Machungu tuheshimiane tafadhali.
Chanzo: Mwananchi J'tano jana.