The Chant of Savant

Monday 21 May 2012

Kama vigogo wa Uhamiaji mabilionea hao wa TRA ni nini?


Taarifa kuwa vigogo wa Uhamiaji katika vituo mbali mbali nchini Tanzania ni matajiri wa kutupwa kutokana na kuuza vibali bandia kwa wageni haramu. Kimsingi vigogo na wafanyakazi wengi wa mipakani hawapati utajiri wa kutisha kutokana na kuuza vibali tu bali kupitisha unga na madawa yaliyokwisha wakati wake wa kutumika. Na tatizo la kutumia ofisi za umma kujitajirisha haliko uhamiaji tu. Lipo Mamlaka ya Mapato (TRA), Bandari,TAKUKURU, Usalama barabarani, Madinini,  Mbuga za Wanyama, Benki kuu, Balozi zetu nje ya nchi na kila sehemu yenye ulaji. Matajiri si vigogo wala wakubwa tu bali wafanyakazi wote wa hizo idara tajwa. Waache wauze ila kuna siku wataanzisha vurugu. Hivyo badala ya kudanganywa kuwa imeundwa tume ya kushughulika na vigogo wa Uhamiaji walituhumiwa, wizara zote zingefumliwa na kuundwa upya huku mfumo mzima wa utendaji wa serikali ukibadilishwa. Ni Tanzania pekee wageni wanaweza kuingia na kujifanyia watakavyo bila kushughulikiwa. Siku hizi kuna wahindi wana hata makampuni ya kuingiza wafanyakazi haramu na kuondoka na utajiri. Hivi kama vigogo wa uhamiaji ni wakwasi hivi, hao wa TRA si balaa? Kwa habari zaidi BONYEZA hapa.

No comments: