Robert "Rider" Dewey wa Colorado nchini Marekani ni mtu aliyeonja adha ya makosa ya mfumo. Mwaka 1994 ulitokea ubakaji na mauaji ya msichana Jacie Taylor (19) huko Palisade Colorado. Kama kawaida polisi walianza kumtafuta muuaji na hatimaye kumshuku Dewey ambaye alishitakiwa na kufungwa kifungo cha maisha miaka 16 iliyopita. Tangia hapo jamaa alikaa gerezani kwa kosa ambalo hakutenda hadi jana alipoachiwa baada ya kipimo cha DNA kubaini muuji mwingine ambaye hata hivyo yumo ndani akitumikia kifungo cha kuua na kubaka. Kwa habari zaidi BONYEZA HAPA.
No comments:
Post a Comment