The Chant of Savant

Thursday 10 May 2012

Akili za mchwa na kifisadi ATC na ukodishaji ndege


Wakati tukipiga kelele za sayansi na teknolojia uwekezaji na ushirikiano wa Afrika Mashariki, Tanzania tunaonyesha upuuzi. Sijui kwenye huo ushirikiano tutachangia nini zaidi ya upuuzi wetu. Hebu fikiria. Wakati wenzetu Kenya wakizidi kununua ndege za kisasa chini ya shirika lao la ndege la KQ, Air Tanzania eti inakodisha ndege tena mbovu! Kenya haina madini kama Tanzania ila ina watu wenye akili tofauti na mchwa na vilaza wetu.

No comments: