The Chant of Savant

Friday 11 May 2012

Kichanga kinavyozuiwa kusafiri kwa vile ni gaidi!


  • (Yahoo! News)

Baada ya shambulio la Septemba 11, usafiri wa anga uliharibika na kubadilika na kugeuka kero. Kila kitu kinafanywa kwa sasa kwa kisingizio cha usalama. Usishangae kukaribia kuvuliwa nguo hasa watu wa viwanja vya ndege wanapohisi wewe ni gaidi. Wanatumia vigezo gani? Nani anajua? Hivi karibuni mtoto mchanga wa miezi 18 alizuiliwa kusafiri eti kwa vile jina lake lilikuwa kwenye kile kinachoitwa orodha ya magaidi. Inashangaza watu walioweka jina hawana hata taaluma ya kutosha kutofauti kati ya kichanga na mtu mzima? Mbona huku kwenye nchi za magharibi wanatumia sana tarehe ya kuzaliwa kama password ya watu wao, je ilikuwaje hili likatokea?  Na hii si mara ya kwanza wala ya mwisho. Kwa habari zaidi Bonyeza hapa.

No comments: