How the Berlin Conference Clung on Africa: What Africa Must Do

How the Berlin Conference Clung on Africa: What Africa Must Do

Tuesday, 1 April 2014

Kijiwe chastukia usanii wa Nyaranduuu

MPEMBA  anaingia na Newspaper ya Danganyika Always. Kama ada, anaamkua na kuagiza kahawa tayari kushiriki kikao. Anaonekana kuwa na jambo linalomkera. Anaanza, “Wallahi hii kaya mie yanshida. 
Mmensikia huyo mjivuni aliyeshindwa majangili halafu aanza kuandama wake zetu? Eti wake zetu wakivaa urembo wenye nakshi za ndovu mtawakamata?”
Unaogea huyu Nyaandu siyo? Ankamate mama Hamdaa nimpige mtu zongo,” Anajibu Mgosi Machungi wa Kiango huku akionyesha alama ya kuapa.
Mbwa Mwitu anaamua kuchomekea, “Hakuna haja ya kupigana zongo. Akikamata wenu nanyi mnakamata wake. Ngoma droo au siyo?”
Mgosi anaendelea huku akisonya, “Nasema bia kufumba. Nyaandu acha ushamba. Kamataneni nyinyi mnaouza wanyama tena wako hai. Mnakingia kifua majangii na wauza unga huku mkijifanya kuwasaidia wa bwibwi. Akii au matope?.”
Msomi Mkatatamaa anaamua kumuunga mkono Mgosi. Anasema, “Hizi nazo sanaa nyingine. These geezers are totally bankrupt and need to be kicked out just soon. Samahani nimeongea ukameruni tokana na hasira.
Yale yale ya kujifanya wanasaidia mateja wakati wakilala kitanda kimoja na wauza bwibwi. Mgosi hapa umenena.  Mpe kahawa hadi azimie,”
Anaamuru Msomi na kuendelea, “Wanalala kitanda kimoja na majangili kama lilivyosema gazeti la The Mail on Sunday kuwa wanatafuta njuluku za kampeni na hawakukanusha.”
“Mmeipata ya juzi? Si walimleta mwandishi wa kitasha eti kuja kufanya fact finding akawasafishe huko kwa mama yao. Jamaa alipofika kweli akafanya fact finding na akapa facts nyingi na kwenda kuwachoma tena kuwa hawapambani na ujangili bali wanaufanya.
Alihoji kutokamatwa kwa majangili papa. Wakati Njaa Kaya anatuongopea kwa wako 40 kumbe ni 50. Wakanushe tuwaumbue zaidi. Wanadhani hatujui uchafu wao siyo?” Anazoza Mijjinga huku akiweka tai yake vizuri.
“Baba wakanushe nini wakati kila kitu kiliwekwa wazi? Wakanushe nini  wakati namba zinazoongoza kwenye ujangili zimejaa kwenye ulaji? Unadhani Abduli Kinamna yuko pale kucheza?” Anajibu Kapende.
 Mipawa anazidi kukandia, “Tembo wanaouawa kwa maelfu mazao yao yanaishia Asia siyo Tuliani, Tanga wala Mtwara.” Anamalizia akimkata jicho Mgosi ambaye anamuunga mkono kwa kuamsha vidole viwili.
Mchunguliaji anakwanyua mic, “Huu nao usanii kukimbizana na vidagaa wanaovaa mapambo ya ndovu tena waliyorithi kwa mabibi zao wakati mwawafumbia macho majangili papa walojazana maofisini. Acheni uvivu wa kufikiri kama Nkapa.”
Mijjinga, “Mie anazovaa shemeji yenu alirithi toka kwa bibi ambaye naye alizirithi toka kwa bibi ambaye naye anasema zilikuwa ndiyo mahari ya nyanya wa bibi yake. Hapa kosa lake liko wapi?”
Bi Sofia Lion aka Kanungaembe naye anaamua kukatua mic, “Hakuna haja ya kulalamika. Sheria ni msumeno hukata huku na kule. Hii ndiyo tabu ya watu wetu. Mnataka sheria itumike kwa kubagua. Acheni lawama za bure. Wake zenu watashikwa mtake mistake.”
Kanji kama kawa amepata upenyo kwa Sofi, anachomekea, “Kama hii Nyandu sema kamata vote nawaa products ya tembo lazima takamata hata kama piga kelele. Mimi shauri veve fuata sheria epuke sumbufu dugu yangu.”
“Kama ni kukamata basi wakamate mkeo Kanji ufurahi maana huwa hamna wivu nyie. Mwaka huu tutasikia mengi hasa ikizingatiwa kuwa uchakachuaji wa uchaguzi ni mwakani. Hamkusikia mwana wa mfalme akiwahadaa jamaa kuwa ataongeza idadi ya mashule na kuboresha barabara wakati mfalme mwenyewe alishindwa?” Anachomekea Kapende.
“Manawasikiliza hawa wahuni.” Mipawa anajibu huku akinywa kahawa. Anaendelea, “Msinikumbushe wanavyohimiza watu walipe kodi ya ubuyu wakati wakisamehe wachimba madini mabilioni ya kodi. Hamjaona wawekezaji wanavyobadili majina kila baada ya miaka mitano?”
 Msomi anaamua kukatua mic, “Hao si wawekezaji bali wachukuaji wanaoshirikiana na wezi wetu kutuibia tu. Hawa na akina Rugeemalira wa vijisenti vya ugoro ni majizi ya kawaida. Hizi zote ni kelele za kampeni na kuzidi kuumbukuliwa.”
“Wanazidi kukaribisha Wachina waje kuwekeza wasijue wengi wao ni majangili.” Analalama mzee Maneno.
Mbwa Mwitu huku akimtazama Kanji anachomekea, “Wanakaribisha hata Wahindi.”
Kanji hakubali, “Hindi hapana jangili bwana. Hindi siku zote iko dukawallah si jangili dugu yangu. Wewe onea Hindi bure.”
“Kanji please sema kweli bana. Ile Pakistan torosha nyama yetu pale Kia iko hindi bwana.  Kama sema iko dukawallah ya pembe ya ndovu iko kubali nawe.
Kanji, “Hiyo Hindi moja si Hindi yote dugu yangu,” Anaongea Mijjing akiigiza lafudhi ya Kihindi.
Mpemba anadakia, “Yakhe samaki mmoja akioza?”
Wote wameoza tunajibu kwa mpigo.
“Mbona Swahili mingi uza pembe ya ndovu lakini hapana sema?”
“Kanji waishi wapi? Sisi twasema tena wazi kuwa tuna majangili maofisini na porini ati.
Wale walioruhusu ndege kupakia wanyama hai ni majangili hatari kuliko wale wanowaua na kutorosha kwa uficho. Lau au wanaogopa umma na sharia kwa kufanya mambo kwa uficho kuliko hawa wanaowasafirisha mchana tena wakiwa hai.”
“Majangili ni majangili hata wawe wenye madaraka au makuwadi wao. Majangili wanapaswa kunyongwa bila kujali vyeo vyao. Wengine wamepewa ulaji hata ukatibu mkuu wa vyama. Kinamna Andaaman upo?” Anazoza Kapende huku akichezea kifuniko cha kamera yake.
Mzee Maneno anachomekea akisonya, “Mie naona kama kaya imewashinda wangekitoa ili wenye uwezo tuchukue usukani na kuwakomboa wachovu.”
Msomi anajibu, “Hawa jamaa walevi kweli. Hamkusikia juzi wanapiga vita bajaj wakati wakiruhusu mikangafu na mashangingi yanayonunuliwa hovyo kwa pesa ya wachovu? Badala ya kupanua miji na kuijenga kisasa wanaonea wachovu.”
“Msomi unashangaa haya! Kesho watazuia walio konda kuingia downtown ili wasiwasumbue. Kesho kutwa watapiga marufuku wasio na kazi wakati ukosefu wa ajira unatokana na sera zao za kibabaishaji na kiupendeleo.” Analalamika Mijjinga.
Kijiwe kikiwa ndiyo kinanoga si likapita shangingi la Nyaranduu! Acha tulikimbize kwa zomea zomea na mitusi ambayo siwezi kuandika hapa!
Chanzo: Tanzania Daima April 2, 2014. 

5 comments:

Jaribu said...

Ndio serikali ya Tanzania, inamwacha Kinana awamalize tembo lakini ukiwa na heleni ya ivory ndio kosa kubwa. Nchi imeoza.

Ndugu Nkwazi N Mhango said...

Jaribu we acha tu. Kinana ndiyo huyo eti anaongea mambo ya muungano wakati ameshindwa kurejea kwao akawasaidie al shabaab.

Anonymous said...

Sifa ya kiongozi maskini wa mawazo na ubunifu ni kuishi kutegemea mipango ya mfupi ya wizi badala mikakati halali endelevu ya muda mfupi na mrefu kwa vizazi na vizazi vijavyo.

Hawa viongozi tulionao sasa wanaishi kwa miradi ya ujambazi ya tena kwa kufikiria na leo na kesho siyo mtondogoo.

Anonymous said...

Ana nini huyu mnyiramba nyarandu
Degree yenyewe ya kubebwa. Chuo kwani hatujui course work na theiss ya kuandikiwa
Leo anachonga

Ndugu Nkwazi N Mhango said...

Anon one and two mmmenena. Kama mna details za huyu kihiyo mwaga ili watu wamjue naye ajue kuwa wanamjua. Hata mimi nina shaka na elimu yake pamoja na kujinakidi kuwa alisomea nje. Si wote waliosomea nje wameelimika. Tunao akina Januari Makamba ambao tunajua walighushi kidato cha sita na kukimbizwa nje kuficha aibu yao.
Nawashukuruni kwa kuliona hili.