Taarifa kuwa jaji Jon Utumwa (Si jina lake Halisi) kutoa huku mu usiku si za kusikitisha tu bali kustaaajabisha. Sikuweza
kuamini kuwa jaji angetoa hukumu saa 2:30. Laiti kama habari hii
ingetoka kwenye magazeti ya udaku huenda ingeingia akilini haraka. Hata
hivyo si uzushi. Hili lilitokea kama lilivyoripotiwa na vyombo vya
habari. Kesi husika ilihusisha kampuni tata ya kuzalisha umeme ya IPTL
ambayo imehusishwa na utapeli na ufisadi usio kifani. Chombo kimoja cha
habari kiliandika, “Hukumu
hiyo iliyotolewa na Jaji….. katika Mahakama Kuu ya Dar es Salaam,
Januari 17, mwaka 2014 saa 8: 30 usiku, imezusha maswali kutokana na
umuhimu wa Tanesco kwa wananchi wengi.” Pamoja na kusoma kwangu sheria
sijui sheria yoyote inayompa mamlaka hakimu au jaji kutolea hukumu
nyumbani kwake tena usiku. Maana kisheria hukumu inapaswa kutolewa
mahakamani na mahakama inaelezewa kuwa ni washitaki na washitakiwa,
waendesha mashitaka (kwa mhakama za juu) na lazima iwe imekamilika.
Kuonyesha
kuwa hukumu hii ina mshikheri kiasi cha aliyeitoa kutia shaka,
Alipoulizwa kwanini alifanya hivyo badala ya kutoa majibu yanayoingia
akilini alikaririwa akisema, “Mbona
wenzako wameshaandika kuhusu hiyo kesi, wewe ndiyo unataka kuandika
leo? Mimi nimeshatoa hukumu siwezi kuizungumzia tena, wasiliana na
Msajili wa Mahakama.”
Msajili
wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, Amiri Musumi naye alionyesha
mshangao akisema, “Kwa kweli ndiyo nasikia kwa mara ya kwanza kuwa
hukumu ilitolewa saa 8:30 usiku.”
Imefikia
mahali kuna majaji na mahakimu hawasifiki kwa ujuzi wa sheria wala
utendaji haki bali kuwaachia wauza unga. Inaonekana kuna mtandao kama
aliosema rais Jakaya Kikwete wa majangili ambapo kesi fulani chafu
hupangiwa jajifulani mchafu au junk.
Hata
hivyo hii si mara ya kwanza kwa baadhi ya majaji kufanya madudu tena
wazi wazi. Mfano, wamekuwapo majaji wanaolalamikiwa kuwaachia ima
mafisadi au wauza unga. Mfano gazeti la moja liliwahi kuandika, “Mheshimiwa
Jaji huku akifahamu kuwa kesi hiyo imefika mbele yake kwa ajili ya
kusikiliza maombi ya dhamana tu, na kuwa ilikuwa haijafikishwa Mahakama
Kuu kwa taratibu wa sheria, aliamua kumfutia kesi mshitakiwa na kuamuru
kuwa yuko huru."
Kadhalika
Mbunge Ester Bulaya alikaririwa akiliambia bunge kuwa kuna mtandao wa
maovu unaowahusisha watendaji wa mahakama polisi na taasisi nyingine
nyeti za umma. Bulaya alikaririwa akisema. “Kwa kutumia mtandao huo,
baadhi ya Majaji wamekuwa wanatafsiri sheria kwa jinsi wanavyotaka na
kuwapa dhamana watuhumiwa wa kesi za dawa za kulevya ambazo hazina
dhamana. Mfano mzuri ni kesi Na.6/2011, Jamhuri dhidi ya Fred William
Chonde na wenzake ambao walikutwa na kilo 179 za Heroine yenye thamani
ya shilingi Bilioni 6.5.”
Bulaya
aliendelea kusema, “ Washitakiwa hawa wanashitakiwa kwa kosa la
kusafirisha dawa za kulevya ambalo kwa mujibu wa kifungu cha
148(5)(a)(ii) cha sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai pamoja na
kifungu cha 27(1)(a) cha Sheria ya Kuzuia usafirishaji wa dawa za
kulevya halina dhamana.” Je baada ya mbunge kulalamika ni hatua gani
zilichukuliwa? Hakuna. Maana kama zingechukuliwa huyu aliyetoa hukumu
usiku asingefanya hivyo bila shaka.
Mbali na mbunge Bulaya gazeti la Jamhuri mwaka 2012liliandika hivi, “Jaji
Pendo Msuiiya, wakitambua kuwa sheria sheria inazuia. Bila kuchukua
jalada wala kuwasiliana na Mahakama ya Kisutu, huku Jaji Msuiiya akijua
fika kuwa kilo 175 ambazo thamani yake ni zaidi ya Sh bilioni tano, na
watuhumiwa hawapaswi kupewa dhamana; yeye kwa mamlaka aliyonayo kama
Jaji aliamua kuwapa dhamana watuhumiwa hawa. Baada ya kupata dhamana,
Wapakistani walirejeshewa pasipoti zao na wakakimbia nchi. Hawajakamatwa
hadi leo.” Si Bulaya tu aliyelalamikia kadhia ya kuwa na majaji wasio
waadilifu. Mbunge wa Singida Kaskazini Tundu Lissu amewahi kuwalipua
wengi. Aliwataja Fatuma Masengi
na Mbaruku Salumu Mbaruku aliyesema elimu zao ni ya utata, Latifa
Mansoor aliyesema alifukuzwa kwa udanganyifu na ubadhirifu akiwa
mfanyakazi katika Manispaa ya Ilala. Lissu aliwataja pia Kassim
Nyangarika na Zainab G Muruke kuwa hawakuwa na maadili. Pia Lissu
alimtaja Mwendwa Malecela liyesema kuwa tangu ateuliwe mwaka 2006
hajawahi kusikiliza kesi hata moja. Badala yake Lissu alidai kuwa jaji
huyo huenda matibabu India tu.
Ajabu
hakuna hatua iliyochukuliwa zaidi ya watuhumiwa kuendelea kuwa kazini
wakifanya madudu kama kawaida. Je mamlaka zinazowateua zina maslahi gani
katika jinai hii ya kutisha ambayo kimsingi inadhalilisha mahakama na
kushusha hadhi yake ukiachia mbali kukosa imani ya wananchi katika mfumo
wetu wa sheria.
Gazeti
liliendekea, “Julai 30, 2012 baada ya Jaji Dk. Fauuuz kutoa hukumu hiyo
ya ajabu, mawakili wa Serikali ambao ni upande wa mashitaka
wakawasilisha nolle chini ya Section 91 ya CPA.”
Gazeti
liliendelea, “Tulishangaa, kwamba kwanza Mahakama hii haina mamlaka ya
kusikiliza kesi hii, lakini pia baada ya kupita siku 60; bila mamlaka
kisheria, Hakimu Luagooo (si jina lake halisi) akaifuta. Hakimu huyu ni
kero.” Kwa mujibu wa gazeti la Jamhuri la Agusti 2013, hakimu Luangoo
alihamishiwa Lindi akagoma kwenda. Hii inaonyesha mtandao wa maovu
ulivyo na nguvu kiasi cha watu kujipangia ni wapi wafanyie kazi kwa
maslahi yao.
Kama
hali inayoendelea haitarekebishwa, kuna uwezekano Mahakama zetu licha
ya kuendeshwa na vihiyo, zitaendeshwa na wahalifu wanaotumia sheria
kuwaokoa wenzao. Je nini chanzo cha kazia hii? Ni ule uteuzi wa haraka
au vodafasta ambapo majaji wenye mabaka kama vile kuwahi kuhonga kwenye
kesi za wateja wao walipokuwa mawakili na wengine wenye elimu ya kutia
shaka kuteuliwa? Je kwanini mamlaka zinatuletea majaji wabovu kama hawa
hata kama si wote? Maana majaji kama tulioainisha hapo juu wamezidi ya
kuzidisha wameishiwa na kuisha kiasi cha kuchusha na kupaswa kuwa
magerezani badala ya mahakamani. Hapa hujaongelea maaskari
wanaoshirikiana na wahalifu au viongozi wanaokula na wawekezaji
wanaohujumu uchumi wetu kwa kutolipa kodi na kuingia mikataba ya kiwizi.
Chanzo: Dira Aprili 21, 2014.
2 comments:
Hawa ni Magwanda na siyo Magadi
Anon umesikika hasa wao wamekusikia vizuri.
Post a Comment