Mosi, ndoa yako ni siri yako binafsi asiyopaswa kujua mtu yeyote. Ndoa siyo gazeti wala kitabu ambacho unaweza kusoma na wenzako. Ndoa yako ni siri kuliko hata nguo zako za ndani, maana huwa unazinunua au wengine kuzianika zikaonekana. Ndo ani kama moyo wako. Anayeweza kuuona ni daktari wako pekee na Mungu aliyeuumba.
Pili, chumba chenu cha kulala ni sehemu ya siri asiyopaswa kuijua wala kuingia mtu yeyote isipokuwa wawili nyinyi. Hivyo, wale wanaowaruhusu mashoga au wasichana wao wa kazi kuingia kwenye chumba chao cha kulala ni makosa makubwa.
Tatu, matatizo yako ya ndoa yanapaswa kutatuliwa na wawili. Kwanini iwezekane kuyatengeneza mshindwe kuyatatua? Ushauri wa mashoga na marafiki hausadii. Hawajui thamani ya ndoa yako. Na lolote baya likitokea, wao hawatakuwapo. Kitanda usicholala hujui kunguni wake. Hapa lazima usiri uwepo na si usiri tu bali hata hofu na kutomwamini mtu yeyote. Hata inapotokea ukapata ushauri, lazima uupime kwa kuangalia thamani ya ndoa yako na si mawazo ya aliyekupa ushauri. Kupewa ushauri ni jambo moja na kulifanyia kazi ni jambo jingine.
Hakuna anayefungwa na ushauri wa mtu yeyote. Kupanga–––tujue–––ni kuchagua. Unapopanga au kuchagua, fanya hivyo vizuri ukijua wazi. Ndoa yako ni sawa na kaburi. Tunatoa mfano huu siyo kwa sababu ya kukutisha. Tunataka upate ujumbe kama ulivyokusudiwa. Hebu piga picha mtu anapokufa. Kuna mtu anaweza kumsaidia kukaa kwenye kaburi lake? Msaada pekee hapa ni kumchimbia kaburi na kumuingiza wakimuacha mhusika aingie na kuishi kwenye kaburi lake. Unaweza kuugua au kuhisi njaa na kupata msaada lakini si kwenye kaburi. Samahani kwa kutoa mfano wenye majonzi ingawa ndiyo hali halisi.
Kitu kingine wanachopaswa kufahamu wanandoa ni mategemeo au matarajio yao. Wengi wanapofunga ndoa huangalia upande mmoja yaani wa kufaidi. Wanasahau kuwa–––kama ilivyo katika nyanja nyingine za maisha–––kila kitu lazima kiwe na majaribu na mitihani mbalimbali yenye changamoto juu ya kujifunza namna ya kutatua matatizo. Hivyo, unapoingia kwenye ndoa, lazima uangalie pande zote. Ndiyo maana baadhi ya dini na mila hufundisha kuwa ndoa ni kifungo ambamo mhusika asitegemee vinono tu hata machungu. Hata hivyo, ikitokea mitihani, dawa si kuachana wala kukimbiana. Kwani unaweza kumkimbia mjuzi ukajikuta uso kwa uso na mamba. Hii maana yake ni nini?
Ni kwamba mwanandoa mzuri unaweza kudhani ni wa mwenzako kwa sababu kitanda usicholalia hujui kunguni wake. Kila binadamu ana matatizo awe hata rais au msomi wa kiwango cha juu. Huu ndiyo ubinadamu tunaopaswa kuukubali na kuufanyia kazi si katika ndoa tu bali katika maisha yetu yote. Maisha ni safari ndefu yenye kona, mabonde, mito, milima, vikwazo na hata lift.
Ni bora kuhitimisha tukisema wazi. Pig aua. Jua. Hakuna Daktari, mchungaji, mganga, fundi wa ndoa wala mwalimu bali wanandoa wenyewe kuwa tayari kuilinda ndoa yao, kujifunza, kufundisha, kujielimisha, na kuelimishana. Tumeyaona. Tumeyapitia.
Chanzo: Mwananchi leo.
No comments:
Post a Comment