How the Berlin Conference Clung on Africa: What Africa Must Do

How the Berlin Conference Clung on Africa: What Africa Must Do

Monday, 7 October 2024

Ndoa, Tendo, na Faida Zake

Leo tutadurusu ndoa na mambo mengine yanayohusiana nayo. Moja ya mambo yanayohusishwa na ndoa nit endo la ndoa. Sisi tutaiita ibada. Wengine wana majina yao. Wapo waiitayo ibada, dawa, chakula cha usiku nakadhalika. Ukilidurusu neno ndoa, inakuwa rahisi kuliunganisha na kitendo, yaani tendo la ndoa. Hapa, hatuhitaji kuelezea nini tunamaanisha.         Ndoa ni mambo mengi ingawa kubwa na la kwanza nit endo, tendo la ndoa. Ni tendo la ndoa linalozalisha watoto. Ni tendo hili huongeza upendo, amani, na furaha katika ndoa. Hivyo, bila tendo lake, ndoa siyo ndoa na bila ndoa hakuna tendo la ndoa ingawa wapo wanaolishiriki katika kile kiitwacho uzinzi ila si tendo la ndoa. Ni zinaa. Tendo la ndoa huwa tendo la ndoa pasipo ndoa, ni uzinzi wa kawaida tu. Badala ya kuwa ibada, tendo la ndoa huwa machukizo na hufichwa kwa vile ni aibu na dhambi. Linapotendwa na wanandoa, tendo huwa baraka, ibada, na kitu cha kuonea fahari mbali na kuridhika nalo.
            Bila tendo, hakuna ndoa. Zifuatazo ni faida na sababu za Mungu kuumba tendo la ndoa ili kudumisha na kuendesha ndoa.
Mosi, bila tendo la ndoa kwa wanandoa, hakuna ndoa bali msiba, lawama, majuto, hata kifo. Kama mwanandoa au wamanandoa hawawezi tendo la ndoa, hakuna ndoa, na kama ipo, ni kwa muda tu.
            Faipili, tendo la ndoa ni dawa ya usingizi. Kwa walioko kwenye ndoa, jiulize au jikumbushe. Nini hutokea baada ya tendo la ndoa?
            Tatu, dawa ya msongo wa mawazo (stress) na upweke ukiachia mbali kuupa mwili mazoezi ya kiakili na kibailojia. Tendo hili, hasa kwa wanaume, huunguza karoli nyingi kiasi cha kuwapunguzia siyo stress to bali mafuta mwilini. Kwa mujibu wa jarida la Women’s Health (2018), wanasayansi waligundua kuwa wanaume huunguza karoli nyingi kuliko wanawake kwa uwiano wa 101  kwa 69 mtawalia ndani ya dakika 25.  Hata hivyo, kwa wanaolifanya tendo hili bila kuoa au kuolewa, laweza kuongeza msongo wa mawazo hasa hofu ya kubeba au kubebesha mimba. Ndiyo maana tunasisitiza kuwa tendo la ndoa linawafaa wanandoa kuliko wasio wanandoa.
            Nne, licha ya kupunguza msongo wa mawazo, tendo la ndoa linaweza kuondoa mawazo na kuleta ridhiko na liwazo. Kwa upande wa pili, hali siyo hivyo kwa wale wasio wanandoa.
            Tano, ni daraja na kiunganishi baina ya wawili. Kwa wanandoa, kadri muda unavyokwenda na kupata uzoefu, kuna aina fulani ya mazoea na utegemezi hujengeka baina ya wawili hawa. Wanandoa wanapofikia kiwango hiki, huwa na ridhiko kiasi cha kuona kama kuchepuka ni ujinga, ugonjwa au kujitengenezea balaa hasa ikizingatiwa kuwa kufanya hivyo kunaweza kusababisha kumpoteza mwenzako.
            Sita, ni hakikisho na ushahidi kuwa wawili wanapendana na kuhitajiana. Wengi wa wanandoa wenye ugomvi au kutokuelewana, huchokana kiasi cha ima kusalitiana hata kuuana ili wapata fursa ya kupata wale wanaodhani wanaweza kuwapenda au kuelewana nao.
            Saba,  chachu na kichocheo cha ushirikiano, upendo, na uhakika wa utegemezi baina yao. Wanandoa wenye ushirikiano na upendo wa kweli, hutegemeana karibu kwa kila kitu. Kwa wale ambao wazazi au mababu na mabibi zao wameishi kwenye ndoa hadi uzee, anapokufa mmoja, mara nyingi, wanaume hufuata tokana na kukosa ule ushirikiano, mazoea, upendo, na hakikisho katika maisha. 
       Jarida la PLOS (Machi, 2023) lilifanya utatifi juu ya matokeo ya ujane katika nchi za Singapore, Uingereza, na Denmark na kugundua kuwa wanandoa wenye kuanzia miaka 65 kwenda juu wanaweza kufariki ndani ya mwaka mmoja wa kufariki kwa mwenzi wao ambapo wanaume walikuwa 70% ikilinganishwa na 28% kwa wanawake. Hivyo, msishangae kuona wanaume wanakufa wanapofiwa na wake zao. Ni kutokana na mazoea na utegemezi na ukosefu wa hakikisho kimaisha.
            Nane, ni kitu cha lazima na muhimu katika maisha. Ni sawa na chakula au mahitaji mengine muhimu kwao. Ndiyo maana wapo wanaoliita chakula cha usiku.
    Mwisho, ni chanzo cha furaha hata huzuni. Ni mara ngapi umesikia kuwa mwanandoa fulani kaua mwenzake kwa kunyima tendo la ndoa (ibada)? Ni kipimo cha afya ya mwili, roho, na mapenzi.
Chanzo: Mwananchi Jana.

No comments: