The Curse for Salvation

The Curse for Salvation

Sunday, 9 March 2025

Sasa Kanji nafyatuka nageuka fyatu dugu yangu!


Juzi natoka Bombei ona mama na toto. Iko furahi kuba sana. Naacha toto moja. Nakuta mama nakwisazaa toto sita. Yote faida. Nakaa Bombei. Woo! heva iko chafu veve hapana ona. Sikia tu. Nalala naota Tanjania. Baada ya peleka faida, sasa narudi tafuta faida nyingine.
        Napanda dege. Nafika hapa. Swahili moja fyatu nataka fyatua mimi. Nalalamika kama toto eti fyatu fyatuzi iko nafyatua mimi hadi nafyatuka! Swahili nakuta mimi iko soma gazetini. Nauliza kwanini juluku naibiva kila siku? Nasikia hii iko chava. Kama nasema baya sirkal, nachukia veve. Kwanja, naanja. “Hii hindi iko chafu nachanganya Swahili sana. Napenda sana siasa na iko na multiple citizenship.” Nalalamika eti hapana piga kura lakini kama ongozi nachaguliwa, yeye nakaribisa na kuwa karibu nayo. Naongeza kuva Kanji nafanya ongozi sahau ile nachagua yeye. Sasa iko kosa ya yangu au ongozi? 
        Hii jinga naita mimi choli! Lini swahilihindi nakuwa safi dugu yangu? Kama nafyatua hindi nachanganya na Swahili nafanya juli sana. Naondoa baguzi ya luga na rangi dugu yangu. Sasa kosa nini veve nataka fyatua mimi dugu yangu? Mimi iko penda veve sana na juluku yako naleta dukani yangu nunua witu. Vote napata faida. Veve chukua witu. Mimi chukuva juluku. Hapana pendeja hiyo dugu yangu?
Nafika jumbani. Nakuta Swahili nalalamika sana. Nauliza “iko nini veve nalalamika owo kama toto dogo? Swahili iko sangaa kama paka naona juluku! Nauliza tena. Veve napata sida gani nasangaa hiwi? Nasema eti mimi hapana ongea Swahili juli. Nasangaa hadi nataka fyatua Swahili. Nauliza yeye “kwani Swahili iko ongea hindi juli? Sasa Swahili nataka fyatua kila kitu. Nataka hata kuoa totoz ya hindi! Kwanini nakuwa chokoji? Veve iko ona hindi naona totos ya Swahili? Sasa kama siyo nafyatuka, kwanini taka oa totos ya hindi veve Swahili choli?
        Swahili iko tabu mingi sana. Maisha iko gumu au fyatu iko gumu fyatuka na kufyatua ile nafyatua yeye? Naona vatu ikolalamika maisha iko gumu kama jiwe. Kwani, swahili siyo gumu? Swahili nalalamika kama toto dogo. Hindi nalalamika kama vatu kuba. Kama maisha nakuva gumu, kwanini hapana fyatua ile nafanya maisha kuwa gumu? Sasa lalamika nageuka sera ya vatu vote kwa kayani. Hindi nalalamika. Sirkal nalalamika. Tajir na sikini yote lalamika! Kama sirkal nalalamika, nan tasaidia nani? 
            Maisha iko gumu. Sasa hindi nafatyatuka nageuka fyatuzi dugu yangu. Sasa nauliza polepole. Juluku kayani nakvenda vapi? Mbona ile kuba naishi peponi? Kama Swahili napata juluku, naoa vake mingi. Hii hapana lalamika! Natumia juluku mingi fanye serehe. Juzi nakwenda Bembei. Kule jimboni yangu India, vaziri moja ya koa nasamehe juluku rupia laki moza nafukujwa kaji. Hapa vaziri nasamehe, trilioni napandishwa choo! Sasa hapa laumu nani na nini dugu yangu? Kvanini hapana fyatuka ikafyatua ile nafyatua veve dugu yangu?
Svahili iko tabu sana. Nakwenda sule. Napata digrii mingi. Hapana fanya biasara. Naogopa hasara lakini naishi kwa hasara. 
        Swahili iko penda faida. Vapi tapata faida kama hapana biasara? Au nataka kwenda kwa sirkal na kuibia chofu na fyatu juluku? Ile nasoma nayo howo kabisa. Napata digrii ya chumi nakuja chuma chovu na fyatu! Ile napata kazi kwa sirkal nageuka fisadi kuba. Kama hindi nasindva kwepa kodi, hapana lalamika. Hapa svahili nalalamika. Nasema hindi fisadi kuba. Kwani, hindi dio naongoza kayani?
         Sasa sirkal kama nalalamika hapana juluku, kvanini nasamehe kodi ile fanyabiasara kuba kuba? Hapana ona nafyatua na kuumija vatu yake? Nasikia kwa bungeni vaziri naulizwa kwanini nasamehe kodi bila kufuata sharia. Yeye nanyamaza kama jusi nabanwa na lango au chura kuba!
Sasa fyatu vote nakaa kimya hapana fyatukia vaziri lakini nafyatua kelele tu! Napiga kelele mingi kama chura ya bawani. Chura iko imba “yangu yangu.” Kama naokota jive napiga yeye, nakimbia! Natoka bawani hapana guo ya mvilini. Mingine naita chava. Naitwa chava nafurahi! Chava iko dudu chafu. Iko dogo na howyo sana dugu yangu. Je Swahili natofautina na chava guoni na chura bawani? 
        Kama nataka pata juluku, napasa kwenda fyatua ile fyatu kuba nafyatua juluku yao. Napasa zuia choli na mizi kuba. Kama naiba juluku na fyatu naomba yeye saada, sasa taacha kuiba juluku? Hapana nunua gari mingi ya sirkal. Naharibu kusudi. Nanunua vatu kuba kuba. Nakaa jumbani kuba kuba. Naoatesa tumbo kuba kuba. Naitwa kuba. Kila kitu ya kuba, kuba tu. Sasa dogo naishi vapi na wipi? Hapana tumia gari ya sirkal sereheni. Hapana nasafiri sana. Hapana fanya sanii na babaisaji mingi mingi. 
Kama nafanya mambo kuba na veve iko dogo na akili dogo, hapana ona naleta balaa na fyatu mingi nakosa juluku hadi nafyatuka nataka kufyatua veve kwa sababu ya jinga yako na akili dogo? Du! Kumbe naota!!
Chanzo: Mwananchi Alhamis iliyopita.

Chunga yasikukute ya Aziz na ndoa ya majuu

Aziz ni kijana wa miaka 24 wa Kipalestina aliyekimbia udhalilishaji kwao akaishia kudhalilika majuu. Kisa cha Aziz kinafikirisha, kusikitisha, na kufundisha. Wapo wengi kama Aziz walioharibikiwa maisha baada ya kuolewa wakidhani wameoa majuu. Kijana huyu, akiwa hajui hata Kiingereza, alijikuta akijiingiza kwenye ndoa ya mateso. Nkwazi alimjua Aziz. Alikuwa rafiki wa kaka yake aliyemlalamikia kuwa mdogo wake alikuwa akipoteza mwelekeo.
Tokana na kuwajua wote wawili, Nkwazi aliamua kuingilia kati kumsaidia Aziz. Kaka mtu aliwakutanisha Aziz na Nkwazi nyumbani kwetu walikozoea kuja kupoteza muda na kufundishwa Kiingereza. 
        Baada ya kaka mtu kueleza kisa kizima mbele ya mdogo wake, kama marafiki na walezi, tulimuuonya Aziz asijiingize kwenye uhusiano ambao ungemletea majuto baadaye. La kufa halisikii dawa. Azizi alichukia hadi kutwambia “hii ni Kanada nchi huru ambapo kila mmoja anaweza kufanya atakavyo.” Kwa maneno mengine, alitaka tusimuingilie katika maisha na uhuru wake hasa ikizingatiwa kuwa Kanada, vijana huweza kuamua kufunga ndoa hata bila kuwahusisha wazazi na ndugu japo si wote. Ghafla, Aziz aliacha kuja kwetu. Tulijua sababu. Aziz alikuwa kwenye mapenzi na mama aliyemzidi umri tutakayemuita Meg japo si jina lake aliyetaka wafunge ndoa. 
Pamoja na kumuonya asisikie wala kujali,  tulijua ni haki yake kufanya hivyo japo tulimtahadharisha juu ya tofauti za mila na dini. Mfano, tulimjua Meg kama mama aliyekuwa amempenda akipanga kufunga naye ndoa, alipenda sana kuongelea mbwa wake ambaye alikuwa akisema kuwa hata hula na hulala naye wakati mwingine. 
        Si ajabu huku kwa baadhi ya watu kula na mbwa kwa sababu kwao, mbwa ni sehemu ya familia. Hivyo, tuliona hatari itokanayo na kutofautiana kidini na kimila ambavyo vingemkwaza Aziz japo hakusikia. Baada ya kugundua kuwa Aziz alianza kutuchukia mbali na Meg ambaye alikuwa ameambiwa juu ya ushauri wetu, tulimuacha. Maana, yalikuwa ni maamuzi na maisha yake.
Hakika, Aziz na mama wa Kizungu walifunga safari kwenda kwenye visiwa vya Saint Lucia na kufunga ndoa na Meg.doa ilifungwa. Ndoa ilifungwa na fungate ikafanyika. Aziz na Meg walirejea Kanada wakiwa mke na mume. Baada ya muda mfupi, tuliamua kuhama mkoa tuliokuwa tunaishi na kusahau mambo ya Aziz na Meg.
Siku moja, Nesaa alikwama kwenye theluji usiku akitoka shule. Alijitokeza baba mmoja wa Kiarabu aliyekuwa na familia yake akamsaidia kwa kujaribu kukwamua gari asifanikiwe. Hivyo, alishauri ampe lift hadi nyumbani. Yule baba alimfikisha Nesaa nyumbani. Tuligundua kuwa kumbe aliishi mtaa wa pili toka kwetu. Alimsaidia Nkwazi kukwamua gari na tangu siku hiyo wakawa marafiki.
Baada ya miezi kupita, yule Mwarabu alikuja kutuaga kuwa alikuwa anahamia Toronto. Tulifurahi sana na kusikitika. Hata hivyo, alituuliza kama tunamjua Aziz toka kule tulikokuwa tukiishi mwanzo. Alituelezea namna Aziz alivyomuomba atuombe msamaha kwa kudharau ushauri wetu.             Tulimuuliza yule Mwarabu sababu za Aziz kukimbia na kujutia ndoa yake. Alitwambia kuwa Meg hakuwa tayari kubadili dini wala kuheshimu mila ya Aziz mbali na kutokuwa tayari kuacha kufuga mbwa wake kipenzi pamoja na mambo mengine binafsi kama nani mwenye madaraka zaidi ya mwingine kati yake na mkewe. 
        Kwa ufupi, Aziz alijikuta kwenye ndoa ya mateso hadi akakimbilia Toronto kuepuka ndoa ya mateso. Tulifurahi kusikia kuwa Aziz alikuwa amegundua makosa yake na mchango wetu na kujutia. Hata hivyo, maji yalikuwa yameishamwagika. Aziz, licha ya kuonja mateso na kuumia, alipoteza malengo na muda wake. Kwani, tulimshauri akasome kwanza akaghairi. 
Sasa tujiulize. Kisa hiki kinafundisha nini? Mosi, usilolijua litakusumbua hata kukuuumiza. Pili, asiyesikia la mkuu huvunjika guu. Tatu, vijana waepuke kujiingiza kwenye makubaliano ya ndoa bila uzoefu wala ushauri.
        Nne, tofauti za dini hata mila ni muhimu katika kufikia maamuzi ya kufunga ndoa. Mfano, Aziz, muislam, asingeweza kuishi na hata kuchangia kitanda na vyombo na mbwa.
        Tano, umri katika ndoa ni muhimu. Japo hatukatazi waliozidiana umri kuoana, kuna haja ya kulidurusu na kulijadili hili kabla ya kujifunga kwenye ndoa. 
        Sita, si kila ving’aravyo ni dhahabu.
saba, ingawa haya yanaweza kuchukuliwa kama masuala binafsi, yana somo kubwa kwa vijana wanaofikiri kuwa kuoa majuu ni kuukata. Wakati mwingi na mwingine, kufanya hivyo si kuukata bali kukatwa kama ilivyo kwa Aziz na wengine kama yeye.
Chanzo: Mwananchi Leo J'pili.