How the Berlin Conference Clung on Africa: What Africa Must Do

How the Berlin Conference Clung on Africa: What Africa Must Do

Thursday, 31 March 2011

Je mwanzo wa mwisho wa Gbagbo umefika?


Gen Mangou katikati akiwa na wasaidizi wake kabla ya kukimbia

Laurent "Badboy" Gbagbo
Habari toka Abidjan Ivory Coast zimelipoti kuwapo mapambano makali baina ya wafuasi wa rais halali wa nchi hiyo Alasane Ouattara na mwizi wa urais Laurent "Badboy" Gbagbo.
Pigo la pili kwa Gbagbo ni mkuu wake wa majeshi Gen. Phillippe Mangou, mkewe na watoto wao watano kutafuta na kupata hifadhi kwenye nyumba ya balozi wa Afrika Kusini nchini humo.

Habari ambazo hazijathibitisha ni kwamba wafuasi wa Ouattara wameishateka Televisheni ya Taifa RTI ambayo imetoweka hewani tangu Jana. Pia wafuasi wa Ouattara kwa sasa wanadhibiti zaidi ya 80% ya nchi.

Baada ya Ouattara kuona Gbagbo anaendelea kung'ang'ania ameamrisha majeshi yake kupambana na wafuasi wake huku akitanga kufunga mipaka yote ya Ivory Coast na hali ya hatari.Kwa habari zaidi BONYEZA HAPA

Wednesday, 30 March 2011

Kweli Makinda ni chaguo la mafisadi


Hakuna shaka kuwa waliofuatilia majibu na namna spika wa bunge Anna Makinda alivyohemka na kuchemka baada ya mbunge wa Arusha Godbless Lema (CHADEMA) kudai waziri mkuu Mizengo Pinda alidanganya bunge wamemjua Makinda ni nani?

Sijasoma ushahidi wa Lema. Ila nikikumbuka Pinda alivyoliambia bunge kuwa watanzania watatu waliuawa kwenye vurugu za Arusha, naona uongo wa wazi. Maana waliuawa watanzania wawili na mkenya mmoja kiasi cha Kenya kuja juu. Pamoja na kuwa Pinda aliongopa mengine, hili pekee lilitosha kupata karipio. Maana hata kuku wanajua kuwa waliuawa watanzania wawili hata walikozikwa kunafahamika, majina, jinsi, umri na shughuli zao. Je Pinda hasomi hata magazeti? Na Makinda je? Hili halikuhitaji digrii ya uchunguzi ua ubukuzi bali common sense kwa pande zote.

Hata hivyo tusimshangae Makinda. Maana wengi walishangaa kuona Makinda alivyochukia na kuchachamaa utadhani Pinda ni Mungu ambaye hapaswi kutenda dhambi. Walishangaa zaidi na kuuliza mantiki ya ukuu wa mhimili mmojawapo wa dola. Walikereka kuona mkuu wa mhimili unaopaswa kuwa mfano tena ukiitwa mtukufu kutumika kama nepi.

Alipoteuliwa kugombea nafasi ya uspika akitumika kumwengua Spika wa zamani, Samuel Sitta, wengi walishuku na kusema wazi kuwa alikuwa chaguo la mafisadi ili kumtimua Sitta wapitishe mambo yao.

Bahati nzuri au mbaya Makinda hakutoa majibu yanayoingia akilini kukanusha hili. Wapo walioenda mbali na kudai mmojawapo wa watuhumiwa wakuu wa ufisadi wa kutisha aliyeko karibu na rais Jakaya Kikwete mbunge wa Igunga Rostam Aziz alimfuata na kumtaka agombee naye akakubali kugombea. Makinda hajawahi kukanusha hili kwa majibu yanayoingia akilini.

Japo rafu iliyochezwa kumchomoa Makinda kusikojulikana kwa kisingizio cha kuwafikiria akina mama ni historia, kwa wenye kumbukumbu hili halitafutika. Ndani ya nyoyo za akina Sitta ukweli ni kwamba Makinda ni tunda la uchakachuaji, udhalilishaji akina mama na hata ufisadi.

Kila mti utaujua kwa matunda yake. Taarifa kuwa Makinda alimlazimisha mbunge Lema kutoa uthibitisho wa uongo wa Pinda kuepusha malumbano ni za kusikitisha. Kwani Pinda si binadamu ambaye tena ameishaongopa mara nyingi tu? Rejea alivyojivuvumua kuwa atakomesha ununuzi wa magari ya bei mbaya bila kutoa namna atakavyokomesha hili na yakaendelea kununuliwa huku yeye akiishia kulalamika na hatimaye kuficha uso wake.

Hii inathibitishwa na kuja kwa Pinda na kile kinachoonekana kama madai ya ajabu- kukataa shangingi jipya na kushauri apewe mtu mwingine badala ya kulirudisha lilikonunuliwa. Ushauri wa namna hii licha ya kuwa wa woga ni wa hovyo. Maana waziri mkuu ndiye mwenye mamlaka ya kuamuru nini kinunuliwa na nini kisinunuliwe.

Hapa Pinda alionyesha udhaifu usiokifani. Nao ni uongo. Wapo wanaoona: kushindwa kutumia wadhifa wake na kuishia kulalamika na kususa ni kuongopea umma kuwa anafaa wakati hafai.

Rejea usanii wa Pinda wa kutoa amri magari ya umma yasitumiwe nje ya ofisi na saa za kazi. Mbona juzi yameonekana Loliondo kwa babu yakifanya shughuli binafsi na hajasema lolote?

Taarifa za ijumaa ya tarehe 11 mwezi huu ni kwamba Makinda amekataa ushahidi wa Lema zinazidi kumfichua Makinda na waliomsimika hapo alipo kwa faida zao binafsi.

Turejee kwa Makinda. Hivi karibuni alikaririwa akisema, “Lema aliwasilisha vielelezo kimaandishi kama Bunge lilivyomtaka, kuhusu hatua gani atachukuliwa, hizi ni taratibu za ndani siwezi kuziweka hadharani,

Makinda anamaanisha nini anaposema hataweka hadharani hatua atakazochukuliwa Lema zaidi ya kuishiwa? Je kama ataadhibiwa kwa siri Lema atawaambia nini wananchi waliomtuma kuwawakilisha? Je Lema atakubali uhuni huu? Kwanini suala la umma,. tena lililoibuka hadharani mbele ya bunge, ligeuzwe la chumbani? Hili si suala la mke na mume bali la umma ambao ungetaka kuona ama Lema akiadhibiwa kwa kumsingizia waziri mkuu au waziri mkuu akiwajibika kwa kulidanganya bunge.

Hata kama Pinda hatawajibika au kuwajibishwa kutokana na serikali ya sasa kutokuwa na ustaarabu huu, angalau umma utajua mbivu na mbichi.

Kuficha utatuzi wa suala la Lema-Pinda-Makinda ni ushahidi tosha kuwa nchini hatuna utawala wa sheria bali ubabaishaji mtupu ambapo kikundi kidogo cha watu kinaweza kuuteka umma na kujifanyia kitakavyo kama ambavyo Makinda anadhamiria kufanya. Tusiruhusu uhuni huu. Makinda anataka kulidhalilisha bunge kwa maslahi ya mtu mmoja. Je wabunge nao watakubaliana na uhuni huu?

Kwa majibu ya Makinda, unapata kujua asivyofaa kiasi cha kuamini shutuma kuwa alipendekezwa na mafisadi ili kulinda maslahi yao. Kama tunamzushia basi atupe msingi wa kuingilia uhuru wa mbunge na kuminya haki zake hata anapoleta ushahidi mzito.

Bunge ni mali ya wananchi. Linapaswa kuendeshwa kwa sheria, viwango na taratibu na si mapenzi ya mtu au kundi la watu.

Isitoshe uspika ni cheo na si utukufu wala kuwa na thamani kuliko wabunge na watu wengine. Kuna haja ya kumbana Makinda atende haki na ikishindikana zifunguliwe kesi za kumtaka aachie ngazi kutokana na kutaka kuligeuza bunge biashara binafsi. Nawashauri CHADEMA, kuliongeza hili kwenye ajenda yao ya kuwaambia wananchi uchafu wa CCM ambao umegeuza maisha yao kukosa maana na kuwaongezea mateso kwa ajili ya kulinda genge la watu wachache.

Makinda asipokuwa makini, ataondoka pale amechafuka zaidi. Kwani uteuzi wake licha ya kuwa udhalilishaji wa akina mama, utaonekana kuwa machukizo hata kwa wanawake wenyewe. Maana haiingii akilini kwenye nchi yenye katiba inayoharamisha ubaguzi wa aina yoyote mtu kuchaguliwa kwa jinsia yake. Ingawa hili lilipoibuka Makinda alikaa kimya, kwa haya madudu anayofanya aamini asiamini baadaye ataumbuka.

Tumalize kwa kumpa ushauri Makinda asome alama za nyakati. Maana kuna kesho na hakuna kisicho na mwisho chini ya jua. Je kwa matendo ya Makinda tumuweke kundi gani?
Chanzo:Tanzania Daima Machi 30, 2011.

Hii mitoto ya CCAM imenikera sana

WANAOKUMBUKA utawala wa kupigiwa mfano wa shujaa Hastings Kamuzu Banda pale Malawi, watakumbuka Chitukuko Cha Amai M'Malawi kilichoanzishwa na mistress wake kama alivyoitwa, Cecilia Kadzamira.

Baada ya Kadzamira kuwa karibu na mkuu, aliona ni bora kumtumia kupata ulaji. Hapa ndipo ilikuja filosofia ya Mbumba za Kamuzu, yaani wanawake wa Kamuzu kwa lugha nyepesi. Msishangae huyu kayapataje haya. Niliwahi kualikwa huko na Ngwazi mwenyewe ili kuona nchi zinavyoendeshwa mchakamchaka. Ilikuwa mwaka gani tusiulizane.

Acha twende kwenye mada ya mose wa lelo. Hivi karibuni kumetokea mchezo mchafu sana kayani. Mchezo huu usipouliwa mbali tutachenjiana huko tuendako. Hivi unajisikiaje unapomuona mke wa kijiwe au mwanae wakitanua kana kwamba nao ni wakuu?

Wanatoa matamko ya kisiasa wakitumia hata mishangingi na midege ya umma kufanya upuuzi wao! Nani aliwachagua na lini? Je, huu si ufisadi aina mpya ambao wachovu na walevi, sijui, hawajaustukia au wanaridhika nao!

Wakati kupe hawa walioko mgongoni mwa mkuu wakitanua, nao wamewakaribisha kupe wengine chini ya magenge mbalimbali, yawe ya umri au jinsia. Magenge haya yamejisahau kiasi cha kujifanya wenye zizi wakati yako mgongoni mwa ng’ombe. Je, kosa hapa ni la makupe tu au na wale wanaonyamazia ufisadi huu wa kimfumo?

Ingawa vita ya kunguru ni neema ya panzi, juzi sikufurahishwa na tamko la makupe waliotaka eti kulikumbusha lisirikali liwafunge midomo CHAKUDEMA kisiwaamshe wachovu na walevi kupamba na ufisi na ufisadi. Kama wengeshamubuliana wao kwa wao ningewaandikia nyimbo za kuwasifu. Lakini kuanza kuzuia ukombozi wa walevi wameniudhi sana.

Sitaacha kuwauliza kila mara. Mnaongea kama nani wakati ajenda yenu ni njaa na ufisi? Kagombeeni kwenye uchaguzi muone kama ni rahisi kama mnavyodhani hata kama mnatumia sayansi yenu ya uchakachuaji.

Ni ukupe kiasi gani jitu zima kudandia mgongoni mwa mtu halafu linajiona lenyewe ndiyo lenyewe.

Kilichonikera zaidi ni kuona hawa wadudu wakipayuka wakati wakilaumu wengine kupayuka. Kwani kupayuka vibaya kama unajua unachopayuka?

Bila aibu eti yanasema kuna wana genge wanaopayuka payuka mambo ya siri ya ulaji kwenye magazeti ya udaku. Eti makupe haya yanasema hawa jamaa wanyamaze yanyonye maana ni zamu yake kunyonya.

Mbona yenyewe yamekwenda kupayukia kwenye magazeti hayo hayo kama kweli siyo minyani kutoona mikalio yake?

Hii mitoto ya Chitukuko cha Amai M’ Bongolaland kimenikera sana. Nimekereka nusu ya kujifunga mabomu na kulipua mtu. Yaani Bongolaland imekuwa kaya ya vitukuko na vituko siyo? Leo CCAM. Kesho MAWA (Maualaji ya Washirika wa Bedroom wa Madingi). Jana Fursa Sawa kwa Wezi Wote (Equal Opportunity for First Thieves)!

Hawa jamaa wa Umoja wa Vikupe wa Chama Cha Mafisadi (UV-CCM msikosee na kuifananisha hii na UV-CCM ya chama tawala. Ni bahati mbaya vifupi vimefanana) wamenikera sana. Sasa natoa onyo. Wakiendelea na utaahira wao nitaenda zangu Kandahar kufanya mazoezi ya kuja kuwabinladen haraka sana iwezekanavyo kabla hawajavimbiwa. Maana naona wamekula wamelewa wamejisahau sana.

Kwanza, huu si wakati wa kuogopa mtu tena mtu mwenyewe wa kudandia madaraka ya mume au baba. Nawashauri CHAKUDEMA waendelee kudema, kutesa na kunema. Msiogope kitu wala mtu hata kama ni mtoto wa mkubwa. Utaogopaje wakati madevu Mureno Okampo yupo? Kwanza nilisoma naye na kufundisha naye sheria pale Chuo Kikuu cha Havard.

Hivyo, nikimtonya kuwa kuna majambazis yanataka kuhujumu demokrasia kwa kuanzisha ghasia atakuja haraka na kuwasukumizia lupango. Waulize manyang’au wa pale jirani wanavyohaha kumuepuka hata kwa kupiga kampeni za kimataifa za upuuzi.

Tena nimekumbuka. Ngoja nichukue fursa hii kuwalaani wale wapambavu waliotaka eti kuandamana kulaani majeshi ya Uropa kumpa kichapo Mlamali Kashafi. Eti mazezeta haya yanasema eti wanaoshambuliwa ni waislamu!

Je, hao wapinzani wa Kashafi ni wakristo kule Benghazi? Wangejua Kashafi mwenyewe anavyowakandia aliposema eti watu wanataka kumpindua ili waanzishe serikali za kiislamu, wasingefanya upuuzi huu tena mchana. Hapa uislamu uko wapi na kwanini uislamu?

Mbona hatuwaoni mkiandamana kumtaka Gbagbo Badboy akitoe baada ya kushindwa kuchakachua uchaguzi? This, if anything, is but double standard and megalomania. Samahani naongea kimombo kwa vile Mwenambago amepanda.

Kashafi mwenyewe mnayemtetea si muafrika kama mnavyodhani. Hivi hamkusikia hivi karibuni akiwaambia wamanga kuwa kuanzia sasa Libia si nchi ya kimanga bali ya kimakonde? Hii ni baada ya umoja wa wamanga kuruhusu Kashafi achapwe na watasha.

Bila shaka hawa ni al-Qaeda. Maana Kashafi anasema wapinzani wake ni maajenti wa al-Qaeda. Inaonekana hawa jamaa, kama UVCCM hawasomi magazeti.

Hawajui Kashafi alivyowanyea wapinzani wake kwa kuwapakazia kuwa ni al-Qaeda na wala unga walioghilibiwa kumpindua kiongozi mpendwa asiyependwa!

Hakuna watu walevi kama wabongolalalanders. Jana mlitaarifiwa kuwa uuzaji wa Seliteli umeiingizia Bongolalaland tobo la dola 308,000,000 sawa na madafu 500,000,000,000 hamuandamani. Mnaendelea kujikomba kwa akina Kashafi ili wawatupie rupia mbili! Je, nyie si mataahira?

Hamkuandamana kuwalaani Duwanzi na washirika wao wenye madaraka walipopanga kujilipa madafu 94,000,000,000 tena kwa kuwaweka kizani kama mimende!

Nani aliwaroga nyie walevi? Acheni ulevi mtaliwa mnajiona. Hata hivyo, sorry, nimekosea. Mliwe mara ngapi iwapo mnaliwa kila uchao usiku na mchana. Huko nyuma hamkuwa hivi sijui mmeingiliwa na nani?

Ngoja nivuke barabara kabla ya mataa kuzima hawa vichaa wa daladala wasijenigeuza past tense!
Chanzo:Tanzania Daima machi 30, 2011.

Sunday, 27 March 2011

Madege VS ubakaji Libya



Picha kwa hisani ya BBC


Taarifa za hivi karibuni zimeripoti kuwa imla wa Libya Muamar Gadaffi ameanza kutumia mbinu haramu kupambana na wapinzani. Ubakaji ni silaha ambayo ameigundua na kuanza kuitumia dhidi ya watu wake. Hii ni baada ya kudhoofishwa na mashambulizi ya washirika ambayo yamesababisha Gadaffi kupoteza miji yote aliyokuwa ameiteka hivi karibuni.
Madai ya ubakaji kutumika kama silaha yamethibitishwa na madaktari Suleiman Refadi na Abdul Rahim Aquila Najib waliowatibu wahanga wa jinai hii.

Jinai hii ilifichuka baada ya Iman al-Obaidi aliyebakwa na watu zaidi ya watano kujitokeza na kumwaga mtama.
Ingawa Gadaffi alikuwa akiwalaumu al-Qaeda kuwa nyuma ya upinzani, ameanza kutumia mbinu za al-Qaeda. Amekuwa akiwahimiza walibya kujitoa mhanga kwa kuwa taifa la kiislamu limevamiwa.
Baadhi ya maiti za wanajeshi wa Gadaffi zilizopatikana kwenye mji wa Ajdabiya zilikutwa zikiwa na kondomu pamoja na viagra.
Je mwanzo wa mwisho wa Gadaffi umewadia?

Friday, 25 March 2011

Serikali ya Kanada yaangushwa kwa kudanganya



Serikali ya kihafidhina ya wachache ya Kanada ikiongozwa na waziri mkuu Stephen Harper imedondoshwa leo. Kosa lake kubwa uongo kwa umma na bunge. Kiongozi wa upinzani Michael Ignatieff aliitisha kura ya kutokuwa na imani na serikali na kuungwa mkono kati ya wabunge 156-145 hivyo kuashiria kutoungwa mkono kwa serikali. Hivi karibuni baadhi ya wakubwa wa chama cha Conservative cha Harper walikabiliwa na shutuma mbali mbali za hongo, uongo na usiri kiasi cha serikali kupoteza mvuto. Kwa habari zaidi BONYEZA HAPA

"Matajiri" wanavyodhalilisha watawala waroho







Zuma amwagiwa pombe
Kituko kilitokea hivi karibuni nchini Afrika Kusini ambapo rais Jacob Zuma alimwagiwa pombe na mwananchi mmoja. Zuma ambaye anasifika kwa kupenda vimwana na matanuzi alipatwa na mkasa huu mjini Durban nchini mwake.
Japo yaweza kuchukuliwa kama bahati mbaya, huu ni ushahidi kuwa watawala wetu wanajifanyia mambo hovyo hovyo hasa kutokana na kujiingiza kwenye shughuli zinazoweza kuhatarisha usalama na hata madaraka yao.
Inakuwaje kiongozi wa nchi ajikute kwenye mazingira rahisi kumwagiwa pombe? Kuna siku watanaswa vibao kutokana na kuwa na shughuli haramu za siri. Kwa habari zaidi, BONYEZA HAPA

Wednesday, 23 March 2011

Kumbe Shehe Mkuu haoni na ni fisadi!


Mtu anaweza kuwa na jina hata wadhifa mkubwa lakini akafanya mambo madogo. Hii imejidhihirisha baada ya Shehe Mkuu Issa Simba kujitokeza hadharani na kulaani maandamano yanayofanywa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kuhamasisha wananchi kukataa ufisadi na kuboresha maisha yao.
Vikundi vingi vya kiislamu vimekuwa vikilalamika kuwa BAKWATA ni nyumba ndogo ya
CCM. Sasa ukweli umedhihirika kwa maneno ya Simba. Hivi karibuni alikaririwa akisema: “Sisemi ni wanasiasa wa wapi wanaochochea maandamano hayo kwa kuwa kila mmoja anajionea mwenyewe, wao badala ya kutetea amani wanageuka na kuwa wavurugaji wakubwa wa amani,”
Kweli huyu mtu ana macho asiyeona ufisadi wa kutisha unaofanywa na serikali na CCM? Je amepofushwa nani-upendeleo wa kodi au ulinzi anaopewa na CCM?
Je maneno kama haya yalitegemewa kutolewa na mtu mwenye hadhi ya shehe mkuu? Je shehe mkuu hajui kuwa ufisadi na madhara yake havijui dini? Je CCM inashambuliwa kutokana na mwenyekiti wa kuwa mwislamu au fisadi? Huyu bwana anahitaji kuelimishwa kama huu ndiyo uwezo wake wa kufikiri kiasi cha kujipayukia bila kujali wadhifa na nafasi yake. Kwa ufupi ni kwamba shehe mkuu licha ya kujidhalilisha kwa umri na hadhi yake, ametangaza wazi alivyo shirika na mafisadi. Hana tofauti na akina Augustine Mrema, Ibrahim Lipumba, Maalim Seif Hamad na waganga njaa wengine. Je waislamu watakubali kutumiwa hivi?

Nini kitafuata baada ya Loliondo?

Hakuna ubishi. Ambilike Mwasapile sasa ni jina kubwa Tanzania. Hii ni kutokana na bwana mchungaji wa kanisa la KKKT kuwavuta wengi kutokana na kile anachoita “dawa” yenye kutibu magonjwa mengi yaliyoshindikana. Je anatibu kweli au ni ombwe letu la kufikiri? Ni mapema kutathmini. Yeye anadai alioteshwa na Mungu awatibu wenye shida. Kwanini sasa na si kabla?

Ingawa madai kama haya si mapya kwa watu wenye tabia ya kumtumia Mungu kupata mlo wao, kidogo ni ya ajabu. Je ni kweli Mungu ameona ukweli wa mambo kuwa watanzania ni wagonjwa na hakuna mamlaka zenye kuwapa huduma kuondokana na hili? Je kwanini Watanzania na si mataifa mengine? Je ni kwa vile watanzania ni wacha Mungu kuliko wengine? Je kuna namna ya usanii kama baadhi ya watu wanavyoanza kustuka? Je kweli kuna Mungu nyuma ya hili au ni kwa vile Mungu haonekani na hawezi kukanusha bali anatumiwa? Je hii ni kutokana na ukweli kuwa watanzania ni wepesi wa kuamini kila kitu? Maswali ni mengi kuliko majibu.

Kwa vile wengi wanaonyesha kuamini huduma za Mwasapile, hakuna jinsi ya kuweza kuwazuia wasiende au kuwastua. Maana ni uhuru wao kikatiba hata kama wanachoamini kisingekuwa na maana yoyote. Lakini pamoja na hilo, tujiulize. Baada ya sifa za babu kupungua na kuzoeleka, nini kitafuata? Je tushughulikie “magonjwa” na kusahau mengine? Tunauliza swali hili kutokana na kugundua kuwa kama nchi na hata jamii, tumetelekeza mijadala muhimu na bongo zetu na kujiingiza kwenye imani za ajabu. Je huu si ushahidi tosha wa ugonjwa wa jamii husika?

Kinachosumbua sana ni ukweli kuwa na watawala wetu wametugeuza wapuuzi kwa kujifanya wanashabikia tunachoshabikia kiasi cha baadhi ya wanasiasa kutumia fursa hii kujionyesha kama watu wema na wenye kutoa misaada! Je hii nayo si rushwa ya namna yake? Maana, wagonjwa hawana miiko. Hawawezi kuuliza hayo maelfu na hata mamilioni yanayotumika kusafirisha wagonjwa yamepatikana kihalali au kulipiwa kodi. Je huku si kutumia ujinga na matatizo ya wananchi kujipatia umaarufu?

Kila uchao tunasoma ushuhuda wenye kutia shaka wa “walitibiwa” na dawa ya babu. Je ni kweli wamepona au wengine wanatumia fursa hii kuendelea kutuzuga tusijadili hoja za muhimu kama kuendelea kuwekwa kizani au wanafuata mkumbo? Je baada ya ukweli kudhihiri, nini kitafuata? Je tutarudi kwenye kujadili masuala muhimu kama Dowans au kurukia kumshutumu na kumlaumu babu kwa kutuchelewesha na hata kutudanganya?

Ukiondoa Tanzania, hakuna nchi duniani unayoweza kuishawishi kuwa dawa za kuota zaweza kutibu ugonjwa kama Ukimwi ambao umeshindikana miaka mingi. Ni Tanzania tu ambapo mtu anaweza kuamka na kujiita Profesa, shehe, mchungaji, askofu na mamlaka yasifanye kitu. Nani atafanya nini iwapo wanaopaswa kufanya hivyo nao ni wasanii wenye shahada za kughushi japo si wote? Nani ana muda na masuala ya maadili iwapo fasheni ya tawala za kisasa ni madili? Kila mtu yuko bize na ugonjwa wake na hata babu yake na dawa yake! Kesho usishangae akatokea mtu akidai ameota ndoto kuwa katiba ibadilishwe na kuongeza muda wa mihula ya urais au hata kuvunja muungano.

Kwa vile tu jamii ya wagonjwa na wepesi wa kuamini, akitokea mtu wa namna hii atafanikiwa. Atashindwaje kufanikiwa iwapo kila siku unawasikia wapuuzi wakidai tuombee amani? Amani haiji kwa kuomba bali kutenda haki. Ajabu, wababaishaji hawa bado wanaitwa viongozi wa kiroho wakati ni viongozi waroho!

Atashindwaje iwapo tuna sifa kubwa ya kuwekeza kwenye umbea na imani za kusadikika? Ingawa kwenye uwekezaji mwingi kuna rushwa, kuna uwezekano kuwa wawekezaji wengi waliotuingiza mjini kama Richmond, waliwapata watawala wetu kirahisi kutokana na tabia hii ya kuamini kila upuuzi hata uwe wa wazi.

Sishangai ni kwanini uchumi wa Tanzania kwa miongo yote umekuwa ukimilkiwa na wageni hasa kutoka bara Asia. Sababu ni rahisi. Ni kuamini kuwa wenzetu wanajua biashara kuliko sisi wakati biashara yenyewe si nyingine bali kutumiwa na watawala wezi kuficha siri zao. Anayebishia hili akamuulize mzee Idd Simba ambaye licha ya kuwa mchumi na mwanasiasa mashuhuri, ana uzoefu wa kutosha. Alipoandika kitabu chake juu ya wazawa alikaripiwa na kunyamazishwa kutokana na kuwagusa pabaya watawala.

Tuhitimishe kwa kuuliza tena na tena. Je baada ya ukweli wa Loliondo kujulikana, kitafuata nini? Je Loliondo ni zaidi ya matatizo yetu sugu kama vile mgao, kulanguliwa umeme, ufisadi na ubabaishaji?

Chanzo: Tanzania Daima Machi 22, 2011.

Baada ya Dowanis, geshi la polishi

Ngoja niimbe wimbo wangu kipenzi wa kumfuata bwana kwa kuwaua kondoo wake.

Mbuye mkhale nawo

Mbuye mkhale nawo moyo wanga

Ndifunitsa, ndifunitsa

Ndifunitsa kuyenda naye

Ndifunitsa ndifunitsa kumtsata

Ndimukonda ndimtsata ndifunitsa

My desire is to follow lord

My desire is to punish cowards

My desire is to make more money

Make more money buy selling cowards

Cowards of Bongolalaland

Mwili moyo mwili zones

Hizi bangi nazo! Tangu lini mvuta bangi akamtukuza Mungu? Hata hivyo acha nijisifu kama bwana Paulo aliyejiita mwanafunzi wa Yesu ingawa ushahidi ni kwamba hakumuona Yesu. Heri mimi namsifu Mungu na mibangi yangu kuliko Njaa Kaya Kikwekwe na vikwekwe wenzake wanavyotukuza na kuwaabudia mafisadi ambao wamegeuka miungu wao.

Baada ya kuwabimiza mkenge walevi kwa habari na vituko vya Loriyondo, nahisi wameanza kuzoea na kustukia janja yangu. Lazima niandae mkakati wa kuendelea kuwatwisha mkenge ama kujiandaa kuwatia adabu kama watastuka na kuamua kufanya kweli.

Najua wengi waliokwenda kwa babu huenda walipata habari zangu kuwa nami nilikwenda kule kupata kikombe ili kuimarisha afya yangu ugogoro kama Lyatongolwa. Laiti waandishi wa uongo wangeandika habari za wote tuliokwenda kwa babu mbona waliotupa ulaji wangekufa kwa presha ya ugonjwa wa moyo! Ya Loriyondo tuyaache ingawa ukweli umedhihiri kuwa wabongolalalanders karibu wote ni wagonjwa isipokuwa mzee Mpayukaji Nabii wa kweli kwa walevi.

Kwa vile za mwizi ni arobaini na njia ya mwongo ni fupi, niko kwenye harakati ya kuimarisha geshi la polishi ili kuwakong’ota walevi baada ya kuisha ganzi ya Loriyondo. Muhimu, mie si serikali. Hivyo geshi langu ni vibaka wa mtaani ambao nitawatumia kuwachapa walevi wenye kidomodomo. Najua baada ya hapo watataka kujua hatima ya Duwanzi. Duwanzi ni mradi wa kijiwe wa kununua mkaa wa kuchemshia kahawa. Kwa ufupi ni kwamba mradi huu ulikula njuluku nyingi za kijiwe lakini mkaa hakuonekana kijiweni kiasi cha walevi kukosa kahawa na kashata.

Mimi kwa kushirikiana na Mbwamwitu aka Ewassa, Kibaka aka Rostitamu na washikaji wengine, tulichota njuluku kiduchu kwa ajili ya kununua kula za kura. Si unajua walevi, bila kuwatembezea kitu kidogo hawakupi kula wala kura. Bila kura ya kula utakulaje? Kwa vile mtindo ni kula na kulipa, wao wanasota na shida ya kukosa kahawa na kashata nasi tunatanua kwa kulipana vinono. Zamu yetu kulipa ikifika bila kuwa na geshi lenye la vibaka na vifaa vya kuwachapia yaani visu na nondo tunaweza kujikuta wanatu-mubarak Mungu pisha mbali.

Kutokana na utaalamu wangu wa kuepukana na majanga niliyotengeneza mwenyewe, juzi nilipata simu toka kwa Mkuu mwenyewe wa Kaya akiomba anukuu mbinu zangu ili kuwanyamazisha wanakaya ambao nao wataamka na kudai mambo ya kiza baada ya kustukia ulaji wa Loriyondo. Kwanza nionye. Wewe unayosema haya hakikisha unasoma kimya kimya na ukimaliza chana gazeti na usimwambie yeyote hata mshirika wako wa bedroom. This is top secret which is classified for national security. Najua wengi wanajua kuwa Njaa mwenyewe huwa ananigwaya. Lakini mara chache chache huniomba ushauri kishikaji. Juzi tulikutana mitaa ya Bwagamoyo akaomba nimpe mbinu ya kupambana na wapuuzi wanaotaka pesa ya Dowanis isilipwe.

Kama mkuu wa kijiwe, ifuatayo ni mipango ya kuhakikisha tunaendelea kuwaibia walevi na kuwatawala niliyompa Njaa Kaya Kikwekwe mwana wa Khal.

Mosi, Kununua mitambo mipya ya kuwachapa wapingaji hasa wanafunzi wa vyoo vikuu wanaotishia ulaji wa wakubwa. Wanasahau kuwa sisi na wakubwa ni chama tawala au bullying, sorry, ruling party kwa kiingereza cha mitaani? Najua kuna wahuni wanatuita lulling, looting, goofing, gooning, luring, fucking, screwing, fisadi’s ass-kising-and-licking party na majina mengine mengi tu.

Eti yanadai tulisoma bure. Ndiyo tulisoma bure. Nanyi mnataka kusoma bure? Tuwasomeshe bure wezi waongozeke hadi kutuibia siyo? Kwani nyinyi ni sisi? Sisi wajanja na kusoma bure sahau. Hatuna njuluku ya kuchezea hata mkidhani kujilipa kupitia Dowanis ni makosa si mjinyotoe roho na si ya kutuletea fujo? Jamani hamkuona uchafuzi ulivyopukutisha njuluku zetu? Hamjui pesa tunayolipa ililiwa na wazazi wenu tuliowakirimu? Shauri yenu. Kama hamjui, jueni.

Inabidi muelewe. Mnapoingilia ulaji wetu mnavunja amani ya kaya ambayo kimsing ni sisi si nyinyi.

Hivyo, kwa kujua umuhimu wa geshi la Polishi, nilipendekeza jamaa awangeze mshahara kwa kutembeza kichapo kila watakiwapo. Nilipendekeza wale genge la Fanya Fyoko Ukome (FFU) walipwe sawa na wakuu wa wilaya. Pia waadikiwe barua na vyeti vya shukrani kwa kufanya kweli kule AR.

Mbinu nyingine niliyotoa ni kuhakikisha vigogo wanakwenda Loriyondo kwa zamu kila mara ili habari zao zizidi kuwalewesha wabongolalalanders washikilie kujadili afya za vigogo na kusahau mambo ya msingi hasa Dowanis.

Ingawa mkuu alishakwenda kwa babu, nilimshauri, akiona wabongolalalanders wanaanza kustuka, aende. Mara hii aende bila kificho na kuwambia wazi kuwa anakwenda kule kunywa kikombe kwa ajili ya watu wote ambao wana magonjwa ya kutisha hasa woga, kusahau, kuridhika, kudanganyika, kujisahau na kutokuwa na vipaumbele.

Hili likifanyika, litasaidia kujenga chuki baina ya babu na matapeli wengine waliokuwa wakiwahadaa wabongolalalanders kwa maombi ya uongo na kuwatoa njuluku. Hawa hawatanyamaza. Lazima wataanza kuzoza mbovu dhidi ya babu kiasi cha vyombo vya habari kupata udaku wa kuandika na kusahau habari za Dowanis. Upo hapa mshirika? Kutokana na ubingwa wangu wa intelijensia, juzi CIA walinitumia barua wakiomba sana niwe mkurugenzi wao nikachuna. Nilipenda sana niwe dingi wao lakini sikuona sababu ya kwenda kupunguza umaarufu wa ndugu yangu, rafiki yangu Baraka Obama. Ingekuwa wakati wa Joji Kichaka ningekwenda kumtibulia. Lakini kwa vile huyu bwana mdogo ni mtoto wa schoolmate wangu niliamua kuwatolea nje.

Kuhusu mikakati yote niliyompa jamaa, naona nisitaje yote mkastuka na kumbwaga kama Mubarak. Hivyo kwa wale watakaotaka kujua zaidi ili wajue jinsi ya kupambana naye, namba yangu ya simu ni 0700,000111999.

Najua watakuja niwape mbinu mbadala za kupambana na hili kama watakuwa tayari kulipia huduma yangu. Sina njuluku ya kulipia choo ngoja ninonihino hapa kabla mgambo wa jiji hawajanidaka.
Chanzo: Tanzania Daima Machi 22, 2011.

Sunday, 20 March 2011

January Makamba mnafiki au mtafuta umaarufu?


Kwa mtu aliyesikia mawazo ya January Makamba mbunge wa Bumbuli (CCM) ambaye ni mtoto wa katibu mkuu wa CCM, Yusuf Makamba anashangaa. Ametoa video yake akiwalaumu baba zake chini ya kile alichokiita "Letter to my Fathers".
Wachambuzi wengi wanashangaa kwanini ametumia neno fathers badala ya kuwataja hao anaowalenga kama kweli si mwoga au mtafuta sifa? Isitoshe, anawalaumu hao baba zake kwa unazi na unafiki wakati yeye akiufanya kwa kutetea Dowans.
Ajabu anasikika akilaani kubadili mitaala, demokrasia ya majaribio, huduma mbovu, watu kupenda ukwasi wakati yeye ni tunda la uchafu huu!
Anasikika akiongea kizalendo wakati moyoni ni msaliti na fisadi wa kawaida. Je analenga kuwanasa watanzania wamuone kama mkombozi wakati ni mtoto wa fisadi tu? Je watanzania wataingia mkenge huu? Najua January hana ubavu wa kunijibu lau kwa kutoa maoni hapa. Nimeishawasiliana naye bila majibu. Je January kapata huu ufunuo lini?
Je January Makamba anatafuta mtaji wa kisiasa baada ya kugundua baba yake anaishiwa na kuzidi kuzama au ni mbabaishaji na msanii wa kawaida? Je January si tunda la ufisadi? Mtoto wa nyoka ni nyoka.Je bado January anaendelea na ulevi ule ule wa kudhani watanzania ni mataahira? Kwanini asijiondoe CCM kama kweli anadhamiria anachosema na kusema anachodhamiria?
Kusikia ufufuo wake
, Bonyeza hapa

Friday, 18 March 2011

Kwa wapenzi wa kuruka kwa ndege


Kuna viwanja vya ndege duniani vyenye sifa mbali mbali. Vipo vya kutisha kutua na kupaa kutokana na vilipojengwa. Kuna vifupi na vingine kuwa juu ima ya miamba au theruji. Katika kuvivinjari utajionea mwenyewe ukweli wa hayo yote. Kwa habari zaidi. Bonyesha hapa
Chanzo: Yahoo Travel

Wednesday, 16 March 2011

Dakta, Kanali, Kapteni Rubani Jakaya Kikwete


Baada ya kuchoka shahada za ubwete, sasa rais Jakaya Kikwete amejiongezea elimu nyingine-urubani.Sijui wale waliozoea kumwita Daktari watanza kumuita dakta rubani JK? Picha hii nimeipata kupitia Jamii Forums. Hata kama ni utani, kuna ukweli kuhusiana na uzembe wa serikali ya Kikwete na milipuko ya mara kwa mara ya mabomu yawe ya silaha au ufisadi. Je hii imekaaje?

Tumegeuka jamii ya mataahiri na wanyama!

Nani angeamini, katika karne ya 21 pamoja na ahadi kemkem za maisha bora kwa wote, mahindi matano yangemuua mtu? Hii imetokea na si mara ya kwanza wala ya mwisho. Kuna watoto ima wamekatwa vidole hata kuuawa kwa kuiba shilingi mia mbili na matukio mengine kama haya ya kutisha na kusikitisha.

Kisa cha kutisha kilichoripotiwa hivi karibuni na gazeti la Tanzania Daima kuwa mjane Suzana Karumbete (64) alipigwa hadi kukata roho kutokana na kudhaniwa kuiba mahindi matano, kinatisha na kuhuzunisha sana. Na laity kama kisa hiki kingesimuliwa na mtu binafsi, si ajabu msikilizaji angedhani ni uongo wa kawaida.

Ukweli ni kwamba hii aibu imetokea huko Karukekere tarafa ya Kenkyombyo wilayani Bunda mkoani Mara. Kwa vile hili ni tukio ambalo linapaswa kushughulikiwa na polisi, hatutaingia undani wa kisa hiki. Badala yake tutazama kwenye unyama huu unaoanza kuzoeleka.

Hatujui watanzania hasa viongozi waliojitwisha jukumu la kuleta maisha bora kwa wote kwa hiari yao, kama wanasoma magazeti, wanajisikiaje? Kama tukitumia silka ya utu hii ni aibu na pigo kwa jamii nzima ya kitanzania ambayo imegeuka kama mbwa mwenye uchu anayekula vitoto vyake.

Haiingiia akilini kuamini kuwa tuna watanzania tena vijana wanaoweza kukosa utu na akili kiasi cha kuua mjane mwenye miaka 64 ambaye pigo la kuondokewa na mume linatosha kututikisa mioyoni mwetu kama kweli tungekuwa binadamu.

Taarifa kuhusiana na kashfa hii kwa taifa zinasema eti watuhumiwa wengine wamepewa nafasi ya kutoroka huku waliokamatwa wakibakizwa kwa mwenyekiti wa kitongoji utadhani yeye ni polisi! Utawala wa sheria hapa uko wapi iwapo hata kanuni na taratibu ya kawaida isiyohitaji mtu kuwa wakili inavunjwa kienyeji nab ado tunavumiliana? Namna hhii kwanini wazungu wasiendelee kutuchukulia kama wanyama wenye sura za binadamu? Ajabu ya maajabu, tangu tukio hili kuripotiwa si waziri wala mkuu wa mkoa amejitokeza kulaani!

Wakati kashfa hii ikizidi kuchanja mbuga unasoma habari kuwa mbunge toka eneo hili ambaye ni waziri anapata muda wa kutoleana vitisho na vyama ya upinzani vinavyoandamana dhidi ya kukithiri kwa maovu kama haya! Je huyu naye ni binadamu mwenye kufaa kuwakilisha wanadamu wenzake au wanyama kama yeye?

Ajabu nyingine ni kwamba tukio hili linatokea jirani na kwa shujaa na mfano wa kitaifa Mwl. Julius Nyerere. Je polisi na utawala wa wilaya na mkoa mkoani Mara ni wa nini kama uonevu kama huu unafanyika? Hawa wanalipwa kwa kazi ipi iwapo nyadhifa zao zinatumika kunyamazia maovu ambayo tulipigania uhuru kuyateketeza? Mtu mzima na mwenye kuhitaji msaada wa jamii anauawa eti kaiba mahindi matano bado tunavaa suti na kujiita viongozi!

Hapa tunaongelea mjane mmoja. Bado ndugu zetu wenye ulemavu wa ngozi, vibaka na vichanga wanaouawa kikatili kila uchao. Ajabu wanasiasa bado wanatoa ahadi za maisha bora na utawala wa sheria!

Je ni matusi kusema kuwa jamii yetu ni mbaya na hovyo kuliko hata ya mahayawani wa mbugani Serengeti? Je Suzana Karumbete siyo suto na kashfa kwetu? Je hadi wauawe ndugu wa watawala ndipo tutastuka? Je marehemu angekuwa polisi au ndugu yake au tuseme mkuu wa mkoa hata rais hali ingekuwaje? Je huu si ubaguzi wa wazi?

Kwanini tumejirahisi hivi kiasi cha kuwa watumwa wa maovu na ubinafsi visivyo na tija kwa vizazi vijavyo? Mtu anayeua mjane wa miaka 64 kwa kusingiziwa kuiba mahindi matano angekuwa na akili si angekwenda kupambana na mafisadi wanaoiba mabilioni? Kwa vile mtu wa namna hii hana akili, hajijui wala kumjua adui yake!

Je huu si mgogoro tosha kijamii na kitaifa? Ajabu tunapata mshipa wa kwenda eti kusuluhisha matatizo ya wenzetu wakati tunayo yetu makubwa! Kwanini wahusika hawajisuti na kutumia japo akili ya kawaida (common sense)?

Kuna nini mkoani Mara? Maana mwaka jana mtoto Matiko Mwita (7) anayesoma shule ya msingi Abainamo wilayani Tarime mkoani Mara eti aliunguzwa mikono yake kwa kudokoa samaki. Hii ni baada ya mtoto kuachwa bila chakula kiasi cha kuamua kudokoa samaki. Je mhusika amefanywa nini ili liwe somo kwa wengine? Kwanini tusitumie jicho kwa jicho kwa watu kama hawa wasio na huruma?

Tuhamie sehemu nyingine. Mwaka 2009 Aden Raphael (35) wa Kijiji cha Ivalalila, Wilaya ya Makete, mkoani Iringa alimuua mkewe Roida Sanga (30) kwa kukata na na jembe kichwani baada ya kunyimwa chakula.

"Mtuhumiwa huyo baada ya kurudi nyumbani alimtaka mkewe ampe chakula na baada ya mkewe kumweleza ukweli kuwa chakula kilikuwa hakipo kutokana na kukosa fedha za kununulia, alianza kumshushia kipigo kabla ya kuchukua jembe na kuanza kumkata kichwani mara mbili hadi kufa,” alinukuliwa kamanda wa polisi wa mkoa Evarist Mangalla.

Je tatizo ni la hawa wauaji au jamii kwa ujumla hasa watawala?

Miaka mitatu kabla ya tukio hili hapo juu Emmanuel Julian [28], mkazi wa Dihinda, Turiani, Morogoro alimchinja mkewe eti kwa kuchukua shilingi 500! Tunajaribu kutoa mrorongo huu ili wahusika waone walivyoiangusha jamii iliyowaamini madaraka. Maisha bora yako wapi?

Na hiyo mifano hapo juu ni tone katika bahari. Karibu kila mkoa nchini una visa vya kikatili na kihayawani kama hivi. Je hapa hayawani ni wale wanaotenda unyama au wale walioaminiwa madaraka wakayatumia kuchumia na kutetea ufisadi? Kwanini tumejirahisi kiasi cha kugeuka jamii ya mahayawani? Kama tuna uchungu na maisha yetu kwanini tusipambane na maadui wa kweli badala ya akina mama na watoto?
Chanzo: Dira ya Mtanzania Machi 14, 2011.

Njoo kwangu msiende Loriyondo

MUNGU anatupenda hasa walevi Eimeeen. Bongolalaland imebarikiwa kupata tabibu asiye na kifani dunia nzima, Amiin. Baada ya kutokewa na God na kuniamuru nianzishe dhehebu la The Holiest and Highest Mighty Tarbenacle (THHMT), nimeamua kutoa huduma ya utatuzi wa matatizo mbali mbali bure.

Kuna wahuni wamelipa jina la utani dhehebu langu tukufu lililodhamiria kuondoa matatizo ya walevi. Wanaliita Tuamke Haraka Haraka Matatizo Tuondoshe. Kwa kiasi fulani hawajakosea. Maana dhehebu hili ndiye mkombozi wa pekee awezaye kuwafikisha walevi kwenye nchi ya ulabu na bangi bila wasi wasi baada ya wasanii kuwaahidi hili wakaishia kuwauza utumwani mwa wachukuaji, wachakachuaji na mafisadi. Tuachane na haya ya watani.

Seriously, nimejitenga na wivu, chuki na njaa kama Zaa-kalia Ka-Tortoise ambaye amenukiliwa akilalamika kuwa usanii wake umekosa walaji baada ya kuibuka kwa babu. Babu kakonga roho yangu kuwafichua matapeli wanaomtumia Mungu kuwaibia walevi. Mie nasema wazi. Simchukii babu. Maana wajinga ndio waliwao. Akinipiku kwa kuvuta umati wa wachovu, sitalalamika bali kwenda kuuza nyanya.

Mimi ni tofauti na hawa waota ndoto. Nimemuenga God kwa maninga yangu mawili. Hivyo, tiba yangu si ya kubangaiza wala nini, niaminini.

Baada ya kuona watu hasa vigogo wanavyohenyeka kwenda Loriyondo na ugogoro na utata uliojitokeza kutokana na tiba wanayofuata kule, hatimaye, God amesikia kilio chenu.

Amenituma niwasaidieni. Msiulize tuliongea au kukutana linin a wapi. Hili haliwahusu. Amenipa mamlaka niyatumie lau kujipatia raha hata senti kidogo nikitaka.

Vigogo msiogope kuja kwangu. Hata kama mmeishaikanyaga miwaya nitatunza siri zenu ilmradi tukatiane chochote kitu. Mie siruhusu mle peke yenu ndiyo maana God amenituma kwenu.

Nimeamua kutibu matatizo yote ili kuwaonea hasa huruma vigogo ambao wameonekana wakihaha kwenda kule. Anwani yangu ni simpo. Alhaj, mtakatifu, maulana, nguli, gwiji,mchunaji, sorry mchungaji wa wachungaji, daktari wa madaktari, shehe wa mashehe, mtakatifu Mpayukaji Msemahovyo mjukuu wa mzee Waambie Waelewe, MB, MBA, MSc, DM, PhD, DD, LLD, MPHDM, kwa Mfugadog Bongo, Bongolalaland.

Mnaziona shahada zangu? Si za kughushi. Mie nimesoma sana na si mchunaji bali mchungaji wala si shehena bali shehe.

Mungu amenipa karama hii baada ya kugundua kuwa wabongolalaland ni wagonjwa wa roho, akili na mwili. Hivyo aliona ni bora kumtafuta mtu muadilifu na mwelevu kama mimi.

Mimi siyo kama wale matapeli wanaojivisha uchungaji na ushehena wa kujipachika na uombezi wa kuibiana na kuhadaana. Mimi sitibii njaa wala kutaka sifa. Situmii luninga, magazeti ya udaku wala radio kutangaza huduma yangu. Pia ninayo dawa ya kuzuia TAKUKURU kukukamata hata ukichukua kitu kikubwa. Nina zindiko la kuwazuia walevi kukustukia unapowaliza.

Mie si mpenzi wa kujisifu. Mimi ni kama brigedia Al Adui wa Duwanzi, sipendi sifa. Ila ukweli ni kwamba ni mimi yule yule aliyewapa zindiko kina Dowans, Kagoda, Richmond, IPTL, Net Group, EPA, Zumbe wa mauaji ya Kirosa na wengine wengi tu.

Mjapo kwangu mnatoka ukiwa kile Wajapani huita shin Jin Rui au viumbe wapya. Mie silazimishi uwe na imani. Wala sitaki uwe na kile wahindi huita satyagaraha. Uje ukiwa dasht e kavir au dasht e lut (chumvi au mchanga) mie nitakutibu uwe binadamu. Samahani kwa kuongea kijepu na kigabacholi. Nimewahi kuishi kule. Au niongee kihawaii?

Anyway, mkitoka kwangu mtakuwa wapya na kuambiana heri ya mwaka mpya au Hau'oli Makahiki Hou. Nasema “Uyavutha Umlilo” kwa wale ndugu zangu wazulu au moto wawaka; mtakuja. Tuachane na lugha za watu.

Natenda miujiza ambayo haijawahi kutendwa na yeyote popote juu ya nchini, chini ya bahari na angani. Kwa mfano, nina dawa ambayo ukiinyunyizia nyumbani umeme unawaka na unaepukana na kulanguliwa na Tanidowanesco.

Natibu ukimwi, umaskini, mgao wa umeme, ugumba wa aina zote hata wa mawazo, hofu, matatizo ya kupata mume, kuongeza upendo, kuondosha nuksi na mikosi, kushinda uchaguzi, kukinga maandamano, kuzuia kuvunjika kwa amani, msongo wa roho, presha na chuki dawa hiyo moja.

Nina uwezo wa kuongeza uwezo wa kufikiri, kujiamini, kuridhika, kuvumilia hata kama unaliwa, kuona visivyoonekana na kupanua utajiri.

Pia natibu magonjwa ya migawanyiko, mitandao, msongo wa mawazo, kuzuia kushitakiwa ukighushi vyeti, kuzuia kustukiwa ukichakachua iwe pesa au uchaguzi na mengine kama hayo.

Kuhakikisha praivesi (faragha) yenu inatunzwa, nitatibia vigogo na akina mama uani na chumbani. Nifafanue.

Vigogo wa kiume nawatibia uani na akina mama wawe vigogo au la natibia Guest House. Hili ni sharti nililopewa na God. Najua bila kutoa maelezo mtaanza kuguna na kuuliza kunani.

Kwa akina mama, kama una sura mbaya au ni mzee utatibiwa na vigogo uani. Kama ni kidosho, nimeagizwa nikutibie Guest House ili kuondoa nuksi. Nadhani naeleweka. Pia tiba hii lazima ifanyike usiku kizani ili shetani asiweze kukuona na kukuweka alama na kulipiza kisasi.

Sababu nyingine ya kutibia uani ni kuepuka wezi kuiba teknolojia yangu, pia kuhakikisha wadaku wa magazeti na runinga hawapati picha za vigogo wanaoumwa hasa Ukimwi na ufisadi na kuwaanika. Pia akina mama wazee hawaogopi kiza ni watu wazima.

Wanafunzi hasa wa vyuo vikuu wanaotaka kupata mikopo haraka na kushinda mitihani yao waje kwangu haraka. Wafanyabiashara wakubwa na wawekezaji wanaohofia mikataba yao au ukwepaji kodi wao kugunduliwa na kushitakiwa hata kufilisiwa njooni haraka.

Wale walioshindikana yaani ambao wanahisi hawawezi kuolewa au kuzaa waje haraka. Wanasiasa hawana haja ya kwenda Bwagamoyo kwa mambo ya uchaguzi. Waje kwangu watashinda hata kama hawana sifa. Chama kinachotishiwa kunyang’anywa ulaji kifanye haraka.

Sitaki niseme mengi. Nadhani mmeona ukweli wangu. Hivyo nategemea mtamiminika kwangu badala ya kwenda Loriyondo.

Wajinga ndio waliwao. Naona kinokia kinalonga. Huenda wameanza kujiingiza. Haloo profesa mtakatifu hapa!

Chanzo: Tanzania Daima Machi 16, 20011

Sunday, 13 March 2011

Unamjua Bilionea asiye na nyumba wala gari?

Je ungekuwa wewe ungefanyaje?

Chuck Feeney angekuwa mtanzania au mkenya angeambiwa ni chizi. Ni bilionea ambaye ameupata ukwasi wake bila kuibia serikali wala kudhulumu bali kuchapa kazi. Ni bilionea ambaye ameishatoa msaada tena akitaka asijulikane wa yapata $ 4,000,000,000. Ni mtu wa ajabu kwa viwango vya kawaida. Maana hana makuu wala hana gari na hupenda kusafiri kwa usafiri wa kawaida wa umma. Laiti tungepata mtu kama huyu kuwekeza kwenye ikulu yetu ningempigia debe bila kuombwa.

Wakati nguli huyu mkwasi anaishi kama binadamu wa kawaida, tuna wezi na majambazi wanaonenepeshwa na jasho letu kupitia kodi wanaofanya makufuru kama alivyofanya hivi karibuni waziri Lazaro Nyalandu mbunge maskini na limbukeni wa Singida aliyetaka watanzania kutumia usafiri wa anga waendapo mikoani asijue kwa walio wengi kula yao ni shida tupu.
Bofya usome zaidi habari za bilionea Feeney Pia kwa habari zaidi Bonyeza hapa
Ukitaka kumjua Biionea mdogo kuliko wote soma hapa

Saturday, 12 March 2011

Kapayukaji katimiza nusu mwaka





Kapayukaji kanakaribia kumaliza nusu mwaka hata kama hakajapayuka. Hii ni picha yake ya sasa. Tunazidi kumshukuru Mungu azidi kukawezesha kaje kupayuka baadaye na kuchukua mikoba.

Wajua jiji lenye mabilionea kuliko majiji mengine?


Penye miti hakuna wajenzi. Nani angejua kuwa Moscow ingeipindua New York hata Tokyo na London kwa kuwa na mabilionea? Usishange ikafuatia Dar es Salaam kama wezi wetu wataamua kufichua utajiri wao waliochuma kupitia ufisadi. Hayo ndiyo maajabu ya dunia yetu.Kwa habari zaid, Bofya hapa

Thursday, 10 March 2011

Kikwete na Mkapa watunukiwa shahada ya aina yake



Kwa vile watawala wetu ni wapenzi wa shahada za dezo zitolewazo na vyuo vyenye kutia kila aina ya shaka, wana IT wamewatunuku shahada hii ya aina yake. Hata kama ni utani, inawasilisha picha na taswira halisi ya yaliyoko nyuma ya pazia kwa watawala wetu.

Wednesday, 9 March 2011

“If Gadaffi is right “drug addicts” soon will free Africa”



Though it can be regarded as buffoonish, the idea that protesters in Libya are drugged young and jobless people sometimes makes sense. Even if this is not the case in Libya, there is a naked truth behind this.

When Muamar Gadaffi was cornered, he employed mercenaries in duped or dumped cops from South to thwart what he called duped and drugged youths. This happened when his praise singers went feral. Power is sweet. He had to do something even if it meant killing his own people he swore to defend. This is Africa where power, even cattle for some, have more meaning and value than bin-Adams.

An African potentate can use all tricks in books to put down revolts and riots in his country so as to survive.

Unprecedented wave of changes in Libya has caused mayhem. The flamboyant Gadaffi we used to know and admire, all of the sudden, disappeared so as to be replaced by erratic, lunatic and megalomaniac one. After going a little bit funny in the head, Gadaffi ordered the air force to bomb his country and countrymen and women.

From the blue, his son Al Seif Al Islam (the Sword of Islam) became second in command. He warned Libyans of Islamic caliphates the “aggressors” aim at forming, after toppling his father, before his father implicated Al Qaeda. Many were buffled. How could the guy whose father used to dish money out for the “good cause” of Islam utter such words!

Remember it’s the same Gadaffi who once asserted that the Bible was doctored thus fake and everybody is supposed to become Muslim. This is the guy that opens every occasion using Bismillahi Rahmanir Rahim. What double standard!

We witnessed the son of tyrant gimpingly yelling in the broad daylight. Where does he get locus standi? The much-guarded secret of dictatorship and one-family show laid bare opened for everybody to see.

While the bloodbath was going on in Libya, once again, AU proved its uselessness by not taking any action with regards to imbroglio and chaos in Libya. No doubts African Union (AU) has no difference from any caricature or toothless dog. As days go by, AU loses its meaning not to refer to reputation. If anything, AU has become but a project that causes a lot of sufferings for poor people in African countries.

When African rulers congregate at this shoptalk venue, they are paid per diem from their treasuries. This hard-earned money would help to alleviate the suffering the hoi polloi are facing. Farther on, they have even invited their wives-first ladies who, along with them, convene to do top shoptalk.

Ironically, when African rulers flocks Addis-Ababa, they do so under the pretext of discussing Africa’s problems whilst they are unable to tackle and address theirs at home. They failed even to realize the major aim of the formation of AU-unification of Africa. Where is the unification if South Sudan can secede?

Many question the sincerity and ability of African rulers.

Many African countries are ruled by dictators, thieves, ballot riggers and what not. Most of them are hated more than those already booted out as we witnessed in Egypt and Tunisia.

Farther on, many mistakenly thought that AU would play a pivot role thanks to what’s going on in Africa. One would think that AU, for example, would be the first entity to condemn what is going on in Libya. Sadly though, this did not happen.

Who will face Gadaffi that’s using mercenaries and his private army to butcher his own people? Gadaffi is felling his people openly whilst his counterparts, though not all, are doing secretly.

The day Gadaffi unleashed his terror and brutality, many goofed thinking AU would convene an ad hoc meeting to deal with the chicken eating its eggs. But nay, they feared he’d reveal their hidden scars. For most of them have been queuing on his door seeking favours and assistance. They are in his pocket apart from behaving like him. So if his power is petered out, they are the loser who will have no where to putter.

When Libyans decided to take on their megalomaniac longtime butcher, they wrongly hoped international community would timely lend them a hand. This did not happen sadly though. Instead, western powers whitewashed the whole thing by issuing harsh words of condemnations without taking any action! Too little too late. Mere words can nary break the bone.

What Libyans did not know for sure is the fact that the west is more interested in oil than the innocent blood that the errant tyrant is currently shedding. It is business as usual. Many have restrained their tongues fearing that if Gadaffi survives they might lose business deals.

Back to African potentates, who will point finger on Gadaffi whilst they are all dirty? Who will condemn his employment of mercenaries to kill and bomb his people?

More on Gadaffi’s assertion, if it is true that drugged young people can support anybody, Africa should brace herself for more troubles. For there are much unharnessed manpower in jobless, drugged youths and what not.

When Liberian butcher, Charles Taylor employed this lugubrious method the world did not take note. It was repeated in Congo by Denis Sassou Ngweso. Now it is at work in Libya, no surprise. This means every punk with a fat purse can employ jobless and drugged youths to take power or clinging unto it.

The other side of the coin is good. If all wretched Africans especially paupers, jobless and forgotten ones can gang up together to take on the regime torturing them, it will be real emancipation.

To conclude, it must be noted. Those that want to remain in power in Africa, they must make sure that they fight drugs and unemployment. Failure to this, they are authoring their own downfall for not tackling the duo. For their enemies will employ them to topple them.

For mercenaries can come and mess around making a killing by killing enemies (people) as it is happening in Libya. Sadly though is the involvement of Kenyans. This tarnishes the reputation of East Africa.
Source: Afro Spear March 8, 2011.

Fujo na vurugu vitaletwa na CCM


Wimbi la mapinduzi kaskazini mwa Afrika lilipaswa kuwaogofya watawala wababaishaji na wezi barani. Lakini ajabu bado kuna watu tena wanaoonekana na kudhaniwa kuwa wazima wanafanya mzaha na mambo ya kitoto na maisha ya watu waliowaamini. Wanacheza makida makida na maisha ya watu wanaowawezesha kuishi kupitia kodi zao!

Hakika hawa ni viumbe wasio na shukrani wala mshipa wa utu.

Maandamano yalipowang’oa watawala wa Misri na Tunisia, mlevi mmoja wa madaraka Muamar Gadaffi alisema yaliyotekea kwenye nchi tajwa yasingeweza kutokea nchini mwake.

Mungu si binadamu. Hazikupita wiki hata mbili mlevi huyu akajikuta kwenye matata tena makubwa kuliko ya waliomtangulia kupigwa teke.

Tumeanza na matukio ya Maghreb kuonyesha kuwa umma ukiamua kila kitu kinawezekana na waota mchana wanatimuliwa kama mbwa koko.

Hii maana yake ni kwamba maandamano yanayoendelea yakiongozwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) yanapaswa kuungwa mkono. Ingawa walevi wa madaraka wanataka kuwageuza watanzania mabwege kwa kusema eti CHADEMA inalenga kupeleka nchi pabaya. Ni ajabu! Hivi kati ya CCM na CHADEMA nani ameishaipeleka nchi kubaya?

Tuchukue fursa hii kumkumbusha rais Jakaya Kikwete aliyehutubia taifa na kukaririwa akiwalaani CHADEMA mahali ambapo alipaswa kulaaniwa yeye na genge lake.

Hivi CHADEMA kusema kuwa malipo ya Dowans ya mabilioni ya shilingi ni jambo la kuipeleka nchi pabaya au kulipa? Hivi kulaani na kupinga kulanguliwa umeme ni kuipeleka nchi pabaya? Kweli kupinga mgao wa umeme wa miaka nenda rudi ni kuipeleka nchi pabaya? Kama hivyo ndivyo basi huku “kuipeleka nchi pabaya” ni kwema kuliko alikokwishaiuza nchi Kikwete.

Kikwete anapaswa kutambua kuwa mambo yafuatayo asipoyashughulikia yatamuondoa madarakani na si CHADEMA:

Mosi, kunkandamiza haki za wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu.

Pili, mauaji ya raia wasio na hatia. Rejea mauaji ya Arusha, milipuko ya mabomu kule Gongo la Mboto na Mbagala.

Tatu, kupanda kwa gharama za maisha na kuzidi kushamiri kwa ufisadi unaokingiwa kifua na Kikwete huyu huyu. Hapa hujagusa mfumko wa bei na kupanda kwa gharama za maisha.

Nne, kuendelea kupunjwa, kunyonywa na kudanganywa wa wafanyakazi.

Tano, ukosefu wa ajira na mazingira mabovu ya kazi.

Sita, kuendelea kuingia mikataba ya kijambazi kwenye maeneo mbali mbali.

Saba, Kikwete kuendelea kukumbatia na kuwalinda mafisadi na watuhumiwa wa kashfa mbali mbali kama vile kughushi vyeti vya kitaaluma.

Saba, kujuana na kulindana. Rejea kutoshughulikiwa kashfa ya watoto wa vigogo waliogundulika kuajiriwa Bank of Tanzania (BoT) kwa mazingira yenye utata. Hili unaweza kuliona hata kwenye baraza la mawaziri ambamo kuwa watu kama Hussein Mwinyi na Emanuel J Nchimbi, au wakuu wa wilaya, Nape Nnauye, Rehema J Nchimbi, na nyadhifa nyingine hasa kwenye balozi zetu nje.

Nane, matumizi mabaya ya pesa ya umma. Rejea kuandamana karibu kila mahali ughaibuni na mkewe na kuficha majina ya wanaoandamana naye huko.

Tisa, kutoa ahadi za uongo. Rejea ahadi ya maisha bora kugeuka maisha balaa kwa watanzania. Yako wapi maisha bora? jibu, hata akina Nyerere, Mwinyi na Mkapa hawakutatua matatizo yote. Hivi ndivyo alivyonukuliwa Kikwete akisema wakati wa kuishambulia CHADEMA.

Kumi, kuunda uongo na uhasama kwa kutumia udini ambao haupo bali kuzushwa na serikali ya Kikwete.

Kukimbia matatizo ya ndani kwa kisingizio cha migogoro ya kimataifa. Rejea Kikwete alivyokimbilia Mauritania wakati wa msiba wa wahanga wa milipuko ya mabomu ya Gongo la Mboto. Alishindwa hata kutangaza siku moja ya maombolezo kitaifa ukiachia mbali kutowajibika!

Kumi na moja, kuchakachua uchaguzi na noti mpya.

Kumi na mbili, kuendelea kugawa raslimali zetu na kuzidi kuingia mikataba ya uwekezaji ya kijambazi mipya kama huu unaoanza kupigiwa chapuo wa Dowans II.

Sababu za wananchi kutoogopa kuingia mitaani kupambana na ufisadi na ikiwezekana kumlazimisha Kikwete ama atimize wajibu na ahadi zake au aachie ngazi:

Mosi, kutokana na ukali wa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) hakuna mtawala mwenye ubavu kwa sasa anayeweza kuua halaiki. Kwa woga wa hili na yaliyotendeka Arusha, Kikwete hana jeuri ya kuamrisha mauaji mitaani.

Pili, kubadili msimam kwa Marekani kwa kuacha kuunga mkono wezi na maimla barani Afrika. Kuingia kwa Barack Obama na makosa aliyotenda George Bush, Marekani imeamua kuacha wananchi walete ukombozi wao bila kuingilia kuokoa watawala. Tumeliona hili Libya.

Tatu ni wananchi kuelewa kuwa anachosema Kikwete kuwa CHADEMA inatishia amani ni tafsiri yake kuwa ama watanzania ni wapumbavu au amani ni wao na genge lake kula watakavyo huku umma ukizidi kuteketea. Hili ni tusi kwa watanzania. Ina maana watanzania hawajui maana ya haki, vurugu na amani hadi Kikwete awafundishe? Je kama CHADEMA ingekuwa tishio kwa amani watanzania ni wapumbavu waikubali badala ya kuilaani?

Kama kuna mtu anayetishia kuvunjika amani Tanzania si mwingine bali Kikwete na chama chake ambao wanawachokoza wananchi kwa kufanya maisha yao yawe magumu halafu wanakuja na porojo za kitoto. Huwezi kuwa na amani bila haki wala utulivu bila uadilifu. Wasibweteke na kipindi walichokaa madarakani wakihomola. Hata akina Hosni Mubarak na Zine al Abidine Ben Ali waliwahi kupitia mpito huu wasijue ndiyo wimbi la kuwakumba lilikuwa lawangoja. Ni bora Kikwete na wakwasi wenzake wakasoma alama za nyakati. Kama kuna anayevunja Tanzania si mwingine bali Kikwete na CCM kwa kuwadhulumu na kuwaweka rehani watanzania.
Chanzo: Tanzania Daima Machi 9, 2001.

Unataka kupitisha bwimbwi airport?

Mwenzenu nimepata zali la mentali. Washitiri wangu wamenisukia kupiga mzigo njia panda ya kwenda ulaya ilmradi niruhusu mabomu yao yapite nami nipitishe yangu au kupewa cha juu changu na kuwa bwenyenye na bopari.

Ukiwa na bwimbi au magendo nyingine we nitonye. Unanikatia changu unapitisha bwimbwi lako au mabomu bila kulipa hata hiyo kodi. Unaenda kuwauzia watoto wetu mie hiyo hainihusu. Unaenda kudhamini wanasiasa mafisadi kupata mtaji wa kuingia madarakani ili waibe mimi hainihusu. Mie nachukua changu mapema wajao watajaza wenyewe. Watajijejei na kujilaumu kwanini walizaliwa na mentali kama mimi na mpenda fweza kuliko utu.

Bongolalaland ni nchi nzuri sana. Ukighushu shahada unateuliwa kwenye kabineti. Ukikwapua banki kuu unafungwa miaka miwili halafu unaachiwa na kuja kutumia kama huna akili nzuri.

Tuongee mambo ya zali la mentali na jinsi wachovu tunavyolala makapuku na kuamka mabopari. Unaweza kuamini kuwa mzee mzima nimepata mshitiri akaniunga na immagireisheni ya uhamiaji? Sitamtaja jina. Maana hata wale walioingizwa kukuu na mafisiahadi hawawataji washitiri wao.

Jamaa yangu ambaye amefanya kazi hapa kwa takribani miaka mitano ana majumba magari na akaunti nono. Huyu jamaa tulikuwa tunasota wote kijiweni kabla ya shangazi yake kuwekwa nyumba ndogo na waziri wa nonihino. Nasikia huyu shangazi mtu aliunganishiwa na yule mama mwenye kusimamia kampuni la kuchimba gesi ambaye ni nyumba ndogo ya dingi wa kaya. Huyu bi mkubwa anaitwa mama Raha---no too much. Nadhani kimeishaeleweka. Ambaye hajanipatapata atajaza jaza mwenyewe.

Baada ya kukutana naye nikiwa nimepigika si ndiyo akanipa hii laini. Laini yenyewe ilikuwa simpo tu. Kama niko tayari kutafutiwa kazi na kufanya kazi ya kupitisha mabomu yaani bwimbwi la wahusika niseme. Mwenzenu sikujivunga. Hilo ndilo zali langu la mentali. Siku hizi kama huna mkubwa au jina kubwa ujue umekwisha.

Mwanzoni nilianza kujivunga nikisema hii ni kuhujumu kaya. Nikiwa nashangaa shangaa jamaa si alinitolea laivu kuwa mimi ni nani iwapo watu tena waheshimiwa wanafanya kazi chafu kama yule kijana wa mkubwa fulani aliyenyaka ubunge hivi karibuni anayetetea Dowanis kuliko hata walevi waliompigia kula.

Baada ya kuona sielewi somo alinipa dozi ya mwisho iliyonifyatua hadi nikageuka ghafla kuwa mbweha wakati nilikuwa simba kabla ya hapo. Alinipa stori ambayo nadhani kila msomaji anainyaka. Ni stori ya watu waliouza mama zao, ndugu zao hata makaburi ya babu zao na bado wakaendelea kuwaamanisha walevi kuwa watawapeleka kwenye nchi ya asali na maziwa, ulabu na mibange! Ajabu walevi hawajastukia usalata huu!

Aliponipa mfano huu mbona akili ilizibuka nikachangamkia tenda ya kuhujumu kaya yangu mwenyewe! Naomba Mungu siku moja yasitokee yaliyomtokea Kibaraak kule Masri maana sitakuwa na pa kujificha. Maana siku hizi walevi kwenye baadhi ya kaya wamechetuka kweli kweli.

Kila siku naomba amani na utulivu visitoweke ili niweze kuendelea kutanua hata kama walevi wanatanuliwa na dhiki. Amani na utulivu maana yake ni kwa wenye njuluku kuwatumia makapuku. Hii ndiyo amani ya kaya tunayoimbiwa kila uchao na wenye amani ya kuhomola watakavyo. Amani ni ukoo wa wateule kula hata bila kunawa kwa miguu na mikono wakitapika kama mainzi lakini bila kubughudhiwa. Mungu akupe nini unapojikuta kwenye kundi hili la wateule hata kama ni wachafu kama pig?

Juzi nilicheka rafiki yangu mmoja aliyeletewa shahada ya kughushi alipotoa wazo moja kali sana. Alisema ili kutumia shahada yake vizuri basi angeanza kujiita Kalumekenge Malisera Ewassa Kimdunge.

Mwanzoni sikuelewa mantiki ya kubadili jina. Kumbe ukiwa na jina kubwa na shahada kubwa hata kama ni ya kughushi unapata ulaji na hakuna mtu wa kukufikisha kwa pilato. Ingekuwa hivyo mbona wale jamaa waliotuhumiwa kughushi wangekuwa weshaozea Keko kama si Segerea? Haya tuyaache.

Nina miezi sita tangu nianze kibarua hiki almas. Nimeishapunyua njuluku namalizie hekalu langu kifungua mimba maeneo ya Salasala. Mchuma wa kukogea wachovu ninao tena mjapanizi. Akaunti yangu si haba. Ina mimba tena mapacha. Nina akaunti karibu kila benki hapa Bongo. Nyumba zangu ndogo zote nina mpango wa kuzijengea mabangaluu ya kukata na umma.

Uchovu una madhara yake sawa na kuukata. Tangu zinitembelee washikaji hawabanduki kila ninapokwenda kukata kilaji. Ninaandamana na msururu wa walaji utadhani name ni rais! Ama kweli siku Sir God akikurememba hakuandikii email wala kukubipu. Yeye anatwanga tu na unaona mambo yake. Ila tuache utani. Wakati mwingine heri huzaa shari kama shari iwezavyo kuzaa heri. Nisipokufa kwa ngoma au ulabu basi nitaishi hadi miaka 150.

Maana tangu zinitembelee nawabadilisha kama barabara. Pamoja na kutokuwa handsome, bado napendwa. Sijui napendwa mimi au pochi, hili kwa sasa halinishughulishi. Sasa hivi najinoma na vimwana kuliko hata jamaa yangu Lihumba wa Bunch of Thieves. Hata hivyo napaswa kutumia ili kuondoa mawazo kutokana na njia inayonipatia hii pesa haramu ya kuchuuza ndugu zangu.

Unaweza kuamini kuwa safari zangu siyo zile za Sumbawanga na Mbamba Bay. Siku hizi name napanda pipa kwenda kwa maza kutanua kinomanoma na dogo dogo zangu kama Njaa Kaya.

Name humua kujivuvumua kutuliza hasira zitokanazo na kutumiwa kufanya kazi chafu ya salata. Unadhani bila kulewa hii dhambi si itakunyotoa roho. Hivi ni roho ngapi zinaangamia kutokana na kibarua changu kipya cha kuruhusu bwimbi liingizwe kayani huku jamaa zangu magabacholi wakivusha dola kama hawana akili nzuri?

Nimesahau kuwapa mchapo mmoja wa neema zangu. Nina mpango wa kununua jumba Dubai ili kuwekeza huko. Mambo yakichafuka hapa naishia umangani na kwenda kujinoma kwenye mali zangu kama akina Dadi Balaaali.

Kituko cha mwisho, je ulimuona Vasco da Gama alivyokwenda kujinoma baada ya mibomu kudedisha walevi badala ya kutangaza lau siku moja ya kuadhimisha kikaya achia mbali kukaa matanga?

Naona pipa linatua toka Pakstani. Ngoja niwahi getini kupitisha shehena.

Kulaleki! Nimejikwaa!
Chanzo: Tanzania Daima Machi 9, 2011.

Tuesday, 8 March 2011

Muluzi naye amfuata Chirac mahakamani


Habari zilizotufikia ni kwamba rais wa zamani wa Malawi Bakili Elson Muluzi amefikishwa mahakamani kujibu tuhuma za kutumia vibaya madaraka na ufisadi.Anakabiliwa na shitaka la kutumia vibaya dola za kimarekani 11,000,000.

Nchini Kenya bado wananchi wangetaka kumuona imla wao wa zamani Daniel arap Moi akifikishwa mahakamani kwa kuhujumu nchi hiyo. Kwa Tanzania wimbo ni ule ule. Benjamin Mkapa swahiba wa Muluzi naye anapaswa kufikishwa mahakamani.

Inafurahisha kuona nchi za kiafrika nazo zinaanza kuamka na kupambana na watawala wezi. Kwa habari zaidi
, BOFYA HAPA

Monday, 7 March 2011

Ingekuwa Ufaransa Kikwete na Mkapa wasingekufuru


Rais wa zamani wa Ufaransa Jacques Chirac (78), amefikishwa mahakamani kujibu tuhuma za uhujumu na ufisadi kabla ya kuwa na akiwa madarakani.

Mwanzoni wanasheria walipotaka kumshitaki alijificha nyuma ya kinga. Lakini kadiri siku zilivyoyoyoma, Chirac alijikuta kweupe uso kwa uso na mkono wa sheria na aibu ya umma aliouibia.

Laiti Tanzania tungekuwa na mfumo wenye akili kama wa Ufaransa, Jakaya Kikwete na Benjamin Mkapa wangemalizia muda wao Segerea au Ukonnga kutokana na madudu waliyotenda wakiwa madarakani hasa Dowans, EPA, IPTL, Meremeta, Net Group Solution, SUKITA,Mwananchi Gold,Richmond, Kagoda, Kiwira, Radar na ndege ya rais, nyumba za umma,Songasna mengine mengi ambayo bado yako nyuma ya pazia. Huenda mambo yatabadilika huko tuendako. Tuombe Mungu haki itendeke bila kuangalia uso wala ukoo wa mtu. Kwa habari zaidi
, bofya hapa

Sunday, 6 March 2011

Hivi hapa nani anafanana na Savimbi?





Nimesoma habari ya ajabu kwenye gazeti la Serikali ambapo mlevi mmoja wa madaraka John Chiligati amemlinganisha katibu mkuu wa CHADEMA, Wibrod Slaa na gaidi wa Angola Jonas Savimbi. Kwa habari zaidi, Bofya hapa

Friday, 4 March 2011

Kumbe tumeishafika Tahrir sema hatujui tu!







Hizi ni picha za nyomi ya CHADEMa kule Katoro eneo dogo tu! Jamani tunangoja nini kwenda kumtimua Mubarak wetu? Saa ya Ukombozi ni sasa. Jamani hakuna haja ya kulalamika wakati uwezo, nia, kasi, ari, nguvu na sababu tunavyo.

Tusiogope chochote. Maana hata Njaa Kaya mwenyewe keshatishika kiasi cha kulalamika. Hawezi kutufanya kitu kwa kuogopa Luis Moreno-Ocampo kiboko ya watawala wapuuzi.

Ahadi za maisha bora Afrika ni kwa hawa



Soma kisa hiki cha kusikitisha ambapo mtoto wa rais mwizi anamilki mali ambazo hata Barack Obama na ukoo wake wote hawawezi kumilki.

Ni kisa kirefu kinachohitaji kusomwa ili kujua jinsi watawala wetu walivyo wala watu.Sababu ya jamaa huyo hapo juu kuwa tajiri na waziri ni moja tu- baba yake ni rais.

Kwa wanaofuatilia blog hii watakumbuka kisa cha January Makamba kushangaa alivyoukwaa ubunge na anavyoutumia kuitetea Dowans badala ya wapiga kura. Kusoma kisa chote, tafhali. Bofya hapa

Thursday, 3 March 2011

Bado mmilki wa Dowans ni Rostam Aziz na mabosi wake



Kujikanganya kwa brigedia Suleiman Al Adawi anayedaiwa kuwa mmilki wa kampuni tata ya Dowans ni ushahidi mwingine kuwa huyu jamaa si mmilki halisi wa Dowans bali msanii wa kawaida tu.

Al Adawi ambaye kumbe amegundulika kuwa ni Mzanzibari mwenye utata juu ya alivyopata nyumba zake za Zanzibar, hashawishi kuwa mmilki wa Dowans.

Kuna sababu lukuki za kuamini kwa Dowans ni mali ya Rostam.

Rejea Al Adawi kuwahi kuikana na kutamani apewe Dowans bure kama ilivyotokea hivi karibuni alipokuja kusafisha ufisadi kwa kisingizio cha ubilionea usiojulikana alivyoupata.

Je ni sababu gani zilizofanya kuikana kampuni “yake.” Ni mtu gani asiye kichaa anaweza kukana kampuni yake tena inayodai mabilioni ya shilingi? Je utajiri wa Al Adawi ni kiasi gani hadi kuwa na jeuri ya kukana mali na biashara yenye zaidi ya dola 300,000,000? Maana ukiangalia thamani ya mitambo ya Dowans na pesa wanayodai kama fidia ni pesa nyingi tu ambayo hata Bill Gates hana uwezo wa kuikana hasa inapokuwa ni mali yake hasa na si usanii kama huu tunaofanyiwa mchana na wapuuzi wachache.

Jiulize swali jingine. Serikali na Tanesco wamekana kumwalika. Je amealikwa na nani kuja kufanya usanii wake? Je kama serikali haikumualika kwanini isimkamate hata kwa makosa ya kujipatia nyumba za umma kinyume cha sheria na taratibu? Maana inasemekana Al Adawi ana nyumba mbili Zanzibar alizonunua kimagendo kwa kusaidiwa na kiongozi mmoja mstaafu wa Zanzibar.

Turejee kwa Dowans. Je tuamini lipi kati ya kuikana na kudai ni yake? Hili swali linamkabili hata aliyemleta tuseme bosi wake anayejifanya kuwa mfanyakazi wake yaani Rostam.

Rostam amewahi kukana kuijua, kuimilki wala kuwa na uhusiano na Dowans tena mbele ya bunge. Kimsingi,Rostam alilidanganya bunge jambo ambalo ni kosa la jinai. Je kwanini bunge halimchukulii hatua? Je bunge la namna hili halijawekwa rumenya na mafisadi?

Je madai kuwa spika wa sasa Anna Makinda alichaguliwa na mafisadi ili kuepuka kuchaguliwa kiboko yao spika wa zamani Samuel Sitta hayapati uzito na mashiko hapa? Nitashangaa kama bunge na spika watakaa kimya bila kushughulikia kashfa hii mpya ya Rostam kulidanganya bunge. Na bila spika kulishughulikia hili wengi wataendelea kuamini yale yaliyovuma wakati alipoteuliwa kugombea uspika kuwa alikuwa chaguo la mafisadi. Rejea baadhi ya vyombo vya habari viliporipoti kuwa ni Rostam aliyekwenda kumshawishi Makinda agombee na wote wawili wasikanushe. Je wakati wa Makinda kulipa fadhila ndiyo umefika kwa kukalia kashfa hii?

Kwanini Makinda aweze kumtimua mbunge wa Arusha (CHADEMA) kwa kudai kuwa waziri mkuu Mizengo Pinda alilidanya bunge lakini akae kimya bunge lake linapodanganywa?

Tuache mchezo na maisha yetu na vizazi vyetu. Tuzidi kuwabana wahusika ili tujue ukweli. Je ukweli ni upi kati ya huu wanaotwambia sasa na ule waliotwambia siku za nyuma wakiikana Dowans. Rostam aliwahi kusema kuwa haijui Dowans achilia mbali kuimilki kupitia Powers of Attorney. Je uongo na ukweli ni upi?

Kwanini Rostam na brigedia wake waliikana Dowans halafu baadaye wakaja kuikubali na kuitumikia? Kwanini hawasemi kuwa nao wanatumika na mkubwa asiyependa kujulikana kuliibia taifa? Hata hivyo, wao wana uchungu gani iwapo wana kwao kwingine pa kukimbilia mambo yakichacha? Hata wanaomtumia nao hawana akili nzuri ikizingatiwa kuwa wengi kama wao wameadhirika baada ya mambo yao kufichuka. Nani alijua kuwa uoza, kwa mfano wa Benjamin Mkapa wa Kiwira ungegundulika baada ya kuachia madaraka?

Sababu nyingine ni kwanini brigedia aliogopa kupigwa picha? Je alijua kuwa akipigwa picha wanaoumfahamu watamuumbua kama inavyoendelea kubainika kuwa kumbe alisoma Zanzibar? Hakik, kama alivyodai kuwa hapendi sifa, kama ni kweli, basi huyu jamaa ni mfanyabiashara wa kwanza kutopenda sifa. Hata hivyo huku ni kujidanganya. Kama hakutaka kujulikana basi asingetaka hata jina lake lijulikane.

Sababu nyingine ni kubainika kuwa kumbe aliyekwenda Marekani kuileta Dowans ni mfanyakazi wa Rostam aitwayeHenry Surtees. Pia ukiangalia mgongano wa maslahi na matumizi mabaya ya cheo, Rostam hawezi kukwepa kuwa na hatia ya kutumia vibaya madaraka yake kichama chini ya kile mahakama ya kimataifa ilichoiita ushawishi mkubwa.

Sababu nyingine ni ile hali ya Rostam eti kupewa power of attorney hata kabla ya kampuni yenyewe kuanzishwa. Kisheria hii ni batili kama wanasheria wetu wataacha kutumia njaa kutetea kesi. No contract or agreement can be entered over nonexistant entity. Haiwezekani mtu au watu kuingia mkataba juu ya kitu ambacho hakipo. Kitu kama hakipo hakipo hivyo hakiwezi kumilkiwa hadi kiwepo.

Sababu nyingine ni kugundulika kuwa Dowans haina biashara nchini Costa Rica inakodaiwa kuzaliwa ukiachia mbali sheria za nchi hii kuruhusu usajili wa makampuni ya kitapeli.

Bila wahusika kujibu hoja na maswali yaliyoulizwa hapo juu pamoja na mengine, bado tutaendelea kuamini kuwa Dowans ni mali ya wakubwa wanaowatumia kina Rostam kuficha uoza wao. Vinginevyo hadi hapa, bado Dowans ni mali ya Rostam na siyo hawa wasanii anaotuletea wakashindwa hata kuitetea kampuni wanayodai ni yao.
Chanzo: Dira ya Mtanzania Februari 2011.

Wednesday, 2 March 2011

Kwanini Kikwete anapenda kuficha anaoandamanao nje?


Sijui ni mazoea au niseme haki. Rais wa nchi anapokuwa ziarani nje ya nchi, ni vizuri umma ukajulisha waliomo kwenye ujumbe wake.

Tulizoea kusoma majina ya waliondamana na rais nje ya nchi awamu zote zilizopita.
Tangu rais Jakaya Kikwete aingie madarakani na kuanza kuandamana na watu wanaotia shaka kwenye ziara zake, kumekuwa na ufichaji wa orodha ya watu wanaoandamana naye nje ya nchi. Je anaficha nini kama hakuna namna? Mchezo mzima ulianza baada ya kipindi fulani vyombo vya habari kustukia Kikwete kuandamana na wana familia yake kwenye mkutano wa umoja wa mataifa huko New York kwa gharama ya mlipa kodi maskini.

Walipakodi wanaomwezesha kufanya haya matanuzi wanapaswa kujua anaoandamana nao rais ili kama kuna wasiofaa aelezwe hivyo sivyo.

Wachambuzi chunguzeni tujue sababu ya Kikwete kuficha majina ya watu anaoandamana nao kwenye msafara nje aendapo kufanya u-Vasco da Gama.

Kumbe na PhD ya mwana wa Gadaffi ni feki!


Mambo yanazidi kuwa mabaya kwa utawala na familia ya imla wa Libya Muamar Gadaffi. Baada ya kuwa ukingoni mwa madaraka aliyodumu nayo miaka 42, sasa kuna taarifa kuwa London School of Economics nayo imeingia kashfa kutokana na kuruhusu mtoto wa Gadaffi, Seif al Islam kupata shahada ya juu ya PhD kwa njia zinazotia shaka.

Hata hivyo wengi tunajiuliza. Ni kwanini hili lionekane sasa baada ya magharibi kukosana na utawala wa baba yake anayesadiki wamemsaliti? Kwa habari zaidi
bonyeza hapa.