The Chant of Savant

Thursday 25 April 2013

Angalia watawala wetu wanavyotula


Kuna taarifa kuwa viongozi wastaafu wanatengewa pesa nyingi kuliko baadhi ya wizara. Hii imefichuliwa na vyombo vya habari hivi karibuni. Wengi huwa tunajiuliza, kwanini watumishi wengine wa umma wanaostaafu wanaachwa wajifie huku viongozi na wake zao wakiendelea kutunyonya na kutanua huku sisi tukiteseka? Huu licha ya kuwa uroho na roho mbaya, ni ujambazi wa wazi unaofanywa na wanajiita wenye madaraka. Je ufisadi huu wa kimfumo ambao umegeuka ukoloni mamboleo ukitekelezwa na wakoloni weusi utakomeshwa na nani na lini kama siyo sisi na sasa? Je umma unaridhika na wizi huu wa mchana chini ya dhana ya viongozi wastaafu? Inashangaza na kusikitisha zaidi kukuta kwenye orodha ya viongozi wastaafu kuna watu kama Edward Lowassa ambaye aliachia madaraka bila kufikia muda unaopaswa kisheria ukiachia mbali kuondoka kwa kashfa iliyolisababisha taifa hasara ya mabilioni ya fedha. Inaumiza kukuta mijitu kama Benjamin Mkapa anayejulika wazi kujitwalia Machimbo ya Makaa ya Mawe ya Kiwira na mkewe aliyeliibia taifa kuendelea kuongezewa pesa itokanayo na kodi ya mlipa kodi maskini waliyemwibia. Je tumegeuka taifa la hovyo na kuridhika na hali hii? Tafakarini.
Kwa habari zaidi BOFYA hapa.

3 comments:

Mtwangio said...

Tatizo kubwa tangu kufa kwa Baba wa taifa wa nchi hiyo ambaye ameacha mfano bora kabisa wa uongozi wa kuihudumia nchi na wananchi kama ipasavyo bila ya yeye au familia yake kujilimbikizia mamali au kuwa miongoni mwa familia matajiri wa nchi yetu hii.Je nani leo anaweza kuthubutu kumuunyosha kidole Mwalimu Nyerere,mkewe,watoto wake au familia yake kwamba wamepora au kuuzaa rasilimali za nchi au kujilimbikizia mamali kama viongozi kuanzia awamu ya pili na kuendelea?

Tumeona nchi za mashariki ya kati viongozi wao achilia mbali kuwa na uroho wa madaraka ufisadi na kujitajirisha wao na familia zao lakini walifikia hatua ya kuona nchi hizo ni mali zao binafsi na familia zao na waramba viatu vyao hata wakafikia kuanza utarartibu wa kurithisha madaraka!!!!

Sasa kwa nchi yetu kuanzia awamu ya pili na kuendelea mantiki yao nisawa kabisa na matiki ile ya viongozi waliondolewa na wananchi(vijana)wa mashariki ya kati,nchi ni miliki yao wao familia zao na waramba viatu vyao na wameshafikia hatua ya kurithisha watoto wao madaraka katika kila panapohusuka kwamba ni madaraka.Na kwa vile taofauti yetu sisi na wananchi (vijana)wa mashariki ya kati hatupo tayari kufa kwa ajili ya nchi au kufa kwa ajili ya JUST CAUSE kwa serikali zetu kufanikiwa kutudharau,kutotujali,kutitia woga kwa kutumia vyombo vya usalama wa dola.Kwa hiyo ukiwa nafikra za kwamba viongozi na serikali hizi hazina masilahi na nchi na wananchi wao utasikia weee angalia mpango wako na familia yako!!!kwa kumalizia ni kwamba viongozi wetu wana roho mbayana sisi wenyewe wabongolalaland tuna roho mbaya tupo tayari kumuinua mgeni wa aina yoyote ile hata akitoka burundi ukiachilia mbali watawala wetu wa kiuchumi wahindi na waarabu kuliko kumuinua mzalendo mwenzie na kukosekana na sera ya uzalendo tumekuwa kweli ni wabongolalaland!

Ndugu Nkwazi N Mhango said...

Mtwangio you are right. Hakuna hata mmoja kwa sasa anaweza hata kumnyoshea mbwa wa mwalimu Nyerere achilia mbali Nyerere mwenyewe. Tulio nao ni majambazi wa kawaida tuliodhani ni wanasiasa kumbe siyo. Ila kama wananchi wataendelea kubweteka na kuona kama nchi ni mali ya watawala, kuna siku wataliwa wao wenyewe na wasimlaumu mtu. Laiti kungekuwa na nchi au kampuni inayotafuta watu wa kuuza kama ng'ombe watawala wetu wangetuuza kama mbuzi na kondoo. Inatisha so to speak.

Mtwangio said...

Tatizo kubwa nilionalo mimi kwa watanzania ni kwa watanzania wenyewe kupenda kupigania mapambano ya pembeni na kushikilia mabango katika kadhia ambazo hazina umuhimu kwao, badala ya kupigania mapambano halisi na muhimu ambayo yanamuhusu mtanzania mwenyewe kujikomboa kutokana na udhalimu wa wanasiasa na viongozi wetu.Watanzania hadi hii leo wanapigania udini na kuwa ishu muhimu kuliko maisha yao na kwa udini huu wao na viongozi wao wa kidini ambao tukianzia wa kanisa,viongozi amabao wanaona bora kupigania masilahi yao kwa kupitia kanisa na kulipigania kanisa dhidi ya masilahi ya nchi wanafumba macho kuwapigia makelele wanasiasa na viongozi wa nchi yetu na kuwaambia enough is enough! wapo wapi viongozi wa kanisa mafano wa akina Desmund Tutu au Mtikila?Upande wa viongozi wa kiisilamu pamoja na tofauti zao za kidini bado tu wanabigania ajenda za mabwana zao wa nje ambao ni wafadhili wao na wasiozipendelea kheri nchi zetu matokeo yake badala ya kuwakemea viongozi na wanasiasa wetu wakisema kwamba enough is enough wao na wale wenziwao kule zanzibar wamekuwa wachochezi wa kila fitina na wao ndio wapo mstari wa mbele kabisa wa kushika bango kwamba Mwalimu Nyerere ndio chanzo cha mabalaa ya nchi hii.Sikuweza kuamini niliposikia kwa masikio yangu linapotajwa jina la mwalimi Nyerere wahubiri wa dini hiyo na wafuasi wao wanaomba dua kwa Mungu wakisema"laanatullahu 'alayhi"yaani laana za bMungu zimshukie.kwa nini kusiwepo na viongozi wa kidini wa pande mbili zote hizo waliokuwa na mwamko wa wakashikamana na kupambana na wanasiasa na viongozi wetu ambao ni mafisadi majambazi wasioitakia nchi yetu kheri?Na badala yake wanalipulizia upepo bomu la fitina ya kidini.wakumbuke watanzania dini zote hizo kuu mbili ni dini za kuja yani ni dini za kigeni, mababu zetu kabla dini hizo za kigeni kuja walikua na dini zao na walikua wakiishi kwa kuheshimiana,usalama,upendo na amani hatukisikia wala kusoma katika historia ya dini za mababu zetu kwamba kulikua na fitina au vita vya kidini au kukataana kwa sababu ya kidini au kuitana majina yasiyostahiki kuitana kwa sababu za kidini lakini tangu tuzikumbatie dini hizi za kigeni imekua ni balaa moja kwa moja kwa nchi yetu.Nadhani wakati umeshafika wa viongozi wa kidini kuacha kupigania ajenda za nje na kupigania haki za waumini wao na kuipenda nchi yao.Mimi naongezea tu lakini umeliandikia hili na umeonya natumai kutakuwa na masikio yenye kusikia na ubongo wenye kuelewa.