How the Berlin Conference Clung on Africa: What Africa Must Do

How the Berlin Conference Clung on Africa: What Africa Must Do

Wednesday, 3 September 2014

Unafiki wa kukataa uraia pacha na ufisadi na rushwa


Kwa mujibu wa gazeti la  Nipashe ni kwamba kumbe wanaokatalia uraia pacha ni hao hao wanaotoa pasi za Tanzania kwa wahindi na wasomali huku wakiwa na pasi za zaidi ya nchi moja. Hata ukiangalia hoja walizotoa kupinga ni upuuzi, ujinga na roho mbaya tupu. Kwa habari zaidi BONYEZA HAPA.

6 comments:

Yasinta Ngonyani said...

JAMANI NIMESIKITIKA SANA KUSIKIA HII MAANA NILIKUWA NAISHUBIRI KWA HAMU SANA...

Anonymous said...

Pole Dada ya Yasinta!!! Tunayo Idara ya Diaspora na mratibu wetu husiwe na shaka kama una-tatizo tujulishe.!

Ndugu Nkwazi N Mhango said...

Da Yacinta pole sana. Ndivyo ilivyo. Hawa jamaa wanaendekeza tamaa na upofu kiasi cha kugawa pasi zetu kama njugu lakini wanatia mtima nyongo kwa wale wanaotaka uraia pacha. Hata hivyo ushahidi ni kwamba wanaouza taifa letu hawana uraia pacha vinginevyo waufiche. Sijui kama Kikwete, Chenge, Rugemalira, Lukaza, Rostam, Dr. Idris, Lowassa, Mkapa, Mwinyi na watoto zao wana uraia wa nchi mbili. Sijui kama Nyalandu bingwa wa ujangili, Ladislaus Komba,Mzindakaya, Diodorus Kamala na mafisadi wengine wengi wana uraia pacha.
Anon unaposema idara ya diaspora sikuelewi. Maana kama ni hii ya CCM tuliyoona ikikutana na mabwana zake haina lolote kwetu zaidi ya kutufunga kamba kwa maslahi binafsi hasa ikizingatiwa kuwa wengi wa wana diaspora wanaotambuliwa na kushirikiana na CCM ima ni watoto wa vigogo au wale walioshindwa maisha ughaibuni wakafakamia kutumiwa kama nepi.

Anonymous said...

Tumesema Idara ya Diaspora maana inatosha kwa nini mnaoishi huko ughaibuni tutakuwa tunawafanyia mikutano na diaspora wa hapa Dar pale serena.

Na hawa uliowataja ni waheshimiwa wetu tafadhali waache watufanyie kazi kufufua uchumi na kutunga katiba ya kutufikisha karne ya 22!

Ndugu Nkwazi N Mhango said...

Anon hapo juu huwezi kuwa serious. Kama uko serious basi ushauri wako ni bomu na haumsaidii yeyote. Naona unatetea status quo kwa vile ni wale wale wanaonufaika na jinai inayoendelea nyumbani ambapo mafisadi na majambazi wamekamata kani kiasi cha kuifanya nchi kuwa mali yao binafsi wakiamua watakavyo. Hoja ya watajwa hapo juu ni kujibu upuuzi kuwa uraia pacha utahatarisha usalama wa taifa ambao ulihatarishwa tangu zamani na hao watajwa hapo juu kama sehemu ya mtandao hatari wa kuhujumu taifa letu.

Anonymous said...

hupo Sahihi Mwalimu!!!