Utawala wa rais Jakaya
Kikwete utaingia kwenye vitabu vya historia kama utawala wa hovyo uliowahi
kuwapo nchini. Kwa kisingizio cha kuaga ughaibuni Kikwete amekuwa akipoteza
mamilioni ya shilingi eti kwenda kuaga nje utadhani ndiyo waliomchagua.
Anaondoka kesho kuelekea Australia kuaga baada ya kurejea juzi toka Uswizi
alikokwenda kuaga. Kama haitoshi na mkewe yupo Malaysia sijui naye anakwenda
kuaga au ndiyo hiyo tabia ya kuzurura waliyojizoesha.
Ngoja watoke madarakani
tuone kama watazurura kama walivyozoea. Kuna haja ya kubadili katiba kuzuia
upuuzi huu wa kuzurura na kuacha kazi zikilala nyumbani. Kwa miaka kumi Kikwete
ametuibia tu ukiachia mbali kulea na kushiriki ufisadi.
No comments:
Post a Comment