How the Berlin Conference Clung on Africa: What Africa Must Do

How the Berlin Conference Clung on Africa: What Africa Must Do

Tuesday, 24 April 2018

Magufuli watambue na watunzi na wachapishaji vitabu nchini

Mzee Yussuf 'Big Daddy': Mfahamu Sitti bint Saad mwanamke ...

Tokana na elimu kutelekezwa baada ya kuibuka njia rahisi za kutengeneza fedha kama vile uuzaji wa mihadarati, sanaa hata wizi wa fedha za umma, utamaduni wa kusoma na kujielimisha nchini vilipungua. Rejea mbiu aliyopiga rais mstaafu Benjamin Mkapa akitaka uwepo mdaharo wa kitaifa kuhusiana na kufa kwa elimu nchini japo naye ni sehemu ya tatizo.
Kwa waliosoma miaka ya themanini kabla na baadaye kidogo, watakumbuka namna taifa lilivyokuwa na hamasa ya kusoma hata kutunga vitabu. Nakumbuka vitabu kama vile Adili na Nduguze, Tendehogo, Kusadikika, Things Fall Apart, The River Between, Songs of Lawino and Ocol na vingine vingi ambapo vingi hasa vya kiingereza vilitoka nje ya nchi. Sijui kwa sasa hali ikoje baada ya kuja watu wasio na uchungu na elimu visheni wala uwezo wa kufikiri sawa sawa na kuizamisha elimu yetu. Ni juzi tu nilikuwa nasoma malalamiko kuwa kuna vitabu dhaifu vikifundishwa mashuleni tokana na watunzi kuwa na watu wao waliovipitisha bila kujali ubora wa vitabu husika. Huu ni ufisadi wa kiakili ambao ni mbaya zaidi ya huu wa kiuchumi. Kwani, tunaharibu uwezo wa vizazi vijavyo kufikiri na kutatua matatizo yake.
Inashangaza kuona taifa letu linazama kielimu wakati wenzetu wanaruka sie tukitamani kutembea. Mie ninayeandika nimeishatunga vitabu zaidi ya 15 vitatu kwa Kiswahili na vilivyobaki kwa kiingereza. Vitabu vyangu vimegawanyika kwenye makundi makuu matatu yaani ushairi wa kiingereza, vitabu vya watoto na vilivyobaki vya kiada kwa ngazi ya vyuo vikuu. Mpaka ninapoandika, baadhi ya vitabu vyangu vimeishaombwa kutumika kwenye vyuo vikuu Afrika Kusini na Zimbabwe. Sitaki nijisifu, muda niliotumia kuandika vitabu husika ni mfupi yaani ndani ya miaka tisa ukiachia mbali vingine vingi ambavyo havijachapishwa.
Je wizara husika iko tayari kuanza upya kuangalia ubora wa vitabu vinavyoteuliwa kufundishwa mashuleni? Je vyuo vyetu vinafuatilia wasomi wa kitanzania wa ndani na nje ambao wameiva kiasi cha kuzalisha taaluma kupitia machapisho na vitabu ili kuangalia namna ya kutumia kazi zao nyumbani? Je nani anaona thamani ya tunu hii ya mtanzania? Ajabu, kuna vitabu toka Ulaya na hata Nigeria lakini sijui kama kuna msomi anayejipa muda kuvidurusu na kupendekeza vitumike nyumbani? Tatizo ni nini? Kwanza, siko Tanzania; sina mtu wizarani wala siko tayari kuhonga au kupigia debe vitabu vyangu. Mzee Pius Ngeze mchapishaji wangu amejaribu hadi amechoka. Ajabu, wakati vitabu kama hivi vinaozea kwenye makabrasha au kufaidiwa na nchi nyingine, watanzania wenzangu wanalisha takataka kama vile vitabu vilivyogunduliwa vikiwa na makosa mia kidogo! Kwanini? Ufisadi wa kiakili na kulhali. Tatizo kubwa ni fitina kama alivyolieleza wazi wazi rais Magufuli.
Pili, wachapashaji wetu wengi wako kwenye hali mbaya baada ya serikali kutotumia kazi zao hasa wale ambao wamechapisha vitabu vyenye kudidhi matakwa ya kielimu na kitaaluman nchini. Bila kutumia kazi zao na kuruhusu kazi dhaifu zilichapishwa na watu kwa makusudi ya kuingiza mkenge serikali, tunaua wachapishaji wetu ukiachia mbali watunzi. Tukiendelea hivi, kuna uwezekano tukaja kununua hata vitabu vya Kiswahili toka nchi zisizojua lugha hii vizuri wakati chimbuko lake ni Tanzania. Si hilo tu, tusipothamini kazi za watu wetu, nani atazithamini?
Hata hivyo, bado kuna watanzania wenye kujua thamani ya utanzania na usomi. Msomaji wangu mmoja aitwaye Sirili Akko wa Arusha pamoja na jaji mkuu wa mstaafu wa Kenya Willy Mutunga, PhD, walitambua umuhimu wangu kiasi cha kuomba kila kitabu kinapotoka niwatumie nakala. Ajabu ya maajabu, hata wachapishaji wa Kitanzania ukiwasiliana nao hata hawajibu ukiachia mchapishaji wangu TEPU Ltd ambao wamefanya kazi kubwa kunishawishi nichapishe nao. Vitabu vyangu kwa sasa vinachapishwa Kameruni na Marekani kwa vile ‘havina kiki’ Tanzania. Sijui hata kitabu changu cha Best and West African Presidents ambamo rais John Pombe Magufuli ni rais bora pekee aliyeko madarakani na hai, zaidi ya kuwa Arusha wa kwa Akko kimeishasoma hata kujulikana nchini. So sad; too bad.
Sitaki nionekane kama najipigia debe. Kwa kizazi cha sasa, sijui kama kuna mtanzania ameandika vitabu vya kiada kwa kiasi na kasi kama vyangu. Wachapishaji wangu wote hawajawahi kuniona wala mimi kuwaona zaidi ya kuvutiwa na kazi zangu. Mfano, nilitambulishwa Kameruni na profesa wa kizimbabwe Munyaradzi Mawere ambaye naye sijawahi kuonana naye. Ameishaniomba niende kufundisha kwenye chuo chake cha the Great Zimbabwe University, si mara moja wala mbili. Nimeishachangia chapters nyingi kwenye vitabu vyake ukiachia mbali kuwa na mradi wa pamoja wa kutunga kitabu cha the Manifesto of Africa pamoja ukiachia mbali kile ninachoandika na profesa Eliakim Sibanda pia kutoka Zimbabwe anayefundisha hapa Kanada kitabu kingine.
Kama ambavyo rais John Pombe Magufuli amekuwa akisisitizia uchapakazi na uzalendo, namshauri aangalie kadhia hii kizalendo na kitaaluma kama mwana taaluma pia.
Chanzo: Tanzania Daima, Aprili, 2018.

No comments: