The Curse for Salvation

The Curse for Salvation

Thursday, 19 March 2026

The US must urgently learn from Africa

Evidencing how the US and the world struggling under eccentric convict felon Donnie Trumpet aka Mr. Tarriffman, I feel something is amiss. Considering how Donnie’s ‘Making America and the World Great’ with his wars and tariffs, I suggest that the US must abolish term limits to enable Donnie to rule forever. When I see Donnie, I see a monarch like Kaguuuta and others. Nevertheless, Donnie must blame himself for wasting precious time accusing Africans and other ‘shitholes’ of all sorts of racist hooeys without seeking advice from constitution tampers that Africa’s in hundreds.
            Before Trump’s re-election, the Federal Bureau of Investigation (FBI), at old hours, stormed Donnie’s Mar-a-Lago beautiful mansion. I was frozen. How do you send FBI sleuths to comb, swoop, and vandalise the home of the former and future President? Yes.                     According to Donnie then, the sleuths took some boxes from his mansion. When some of Donnie’s diehards spitefully thought his successor and predecessor, Joe Biden’s behind his predicaments, guess what? The then US Attorney General Merrick Garland whom Donnie appointed got the guts and heroically came forth and said he’s the one who decided to dispatch FBI to commit that sacrilege! Can any African director of whatever security outfit replicate this and survive?
        Donnie must blame himself on not conscripting his sons in the army and for not them high ranks to see to it that they protect their family rule. Erickie and Donnie Jr would make very beautiful soldiers God’s ever created. They’d be in the class of Keineruxxba and others whose fathers drafted in their private so-called national armies to protect their family rules. If there’s anything that Donnie perfected is nothing but appoint his Daughter’s husband, Jerry Kushnei his advisor who pulls more strings than his siblings-in-law.
        To perfect their ‘sacrilegious’ complot against Donnie and his empire and illegally and needlessly shame him, the FBI went in the middle of the night and disturbed the peace of the man and the first woman, who lives her American dream! Who, in Africa, can shamelessly go to the first house to search the residence of the biggest man or woman in the land under whatever pretexts and get away with murder? No officer worth his or her salt can search even big man’s or woman’s barns. Hajitaki huyu?
        Hear what Garland said. “I personally approved the decision to seek a search warrant in this matter” (USA Today,11 August, 2022). When asked about the kind offence Donnie might had committed, Garland said that there “probable cause”, yada, yada, yada that Donnie might have committed a crime. How can a god commit a crime like possessing hush-hush materials while he or she knows everything about the country since it’s under her/his control?                 Donnie called the assault on Mar-a-Lago a pure witch hunt. Wow! How do you turn a President into a witch then hunt him  or her? In Africa, it’s unthinkable and doesn’t add up for the President to break any law while s/he’s above the law, the law, and the constitution. Americans need to go to Africa to learn jurisprudence and its interpretations. Their sanity has petered out.
        If Donnie were an African President, he’d have abolished the FBI. I’ve never understood why the US kept the President who controls the country like his private estate and can appoint his kids, wife, courtiers, and friends as he deems fit to help him milk, sorry, run his estate known as country aka banana republic to be precise. Is the US becoming a banana republic in its own light for the lack of respect to its leader let alone familicracy and nepotism?
        How on earth can a sane person or organisation suspect the President, his family, or networks of any criminality? Why do Americans disrespect their leaders by denying them the infallibility and right to be above the law like their sacrosanct African colleagues? Who bewitched Americans in the first place? 
        Garland said that’s looking for classified documents it believed Donnie took from the White Home when he lost an election that he’s never conceded up until now. As President, the country and everything belong to him or her. This is the biggest lesson Africa needs to teach the US. 
    To borrow a ‘nugget of wisdom’ from Doctor Professor Emeritus Idi Amin, Americans need to learn to love and respect their leaders but not to shame them. Poor Donnie! What’ll he do after his last term in office?
Source: The Citizen, Thursday today.

Wednesday, 18 March 2026

Fyatu anapomkumbuka Fyatu Joni Kanywaji Makufuli



Nkwingwa, ng’wadila Bhabha,
Najua unanisikia hata kama hutanijibu. Katika kumbukizi hili, mafyatu wenzako tunakukumbuka kinamna. Wapo wanaokulilia na wanaoshangilia kutegemea na hali. Leo, sitachonga sana bali kufyatuka.
            Kwanza, wasalimiwa na mafyatu wako wote na wananzengo. Tunakumiss kifyatu.
            Pili, pole kwa sababu, kama ulivyokuwa ukisema, kuna mafyatu utawashangaa. Ungerudi, ungejinyotoa roho namna mambo yalivyovurugika. Mfano, mafyatu na majipu uliyokuwa ukiyatumbua yalisharejeshwa na yanazidi kutanuka na kutanua. Juzi, wapigaji wa mwendofasta waliachiwa.
            Tatu, unaweza kufyatua vibao mafyatu, tena uliowaamini na kutengeza. Si ulisema kuwa watakaofyatua Bwagamoyo ni mataahira na mazwazwa. Kumbe uliwajua! Ungekuwepo, nadhani eheee,  kingeleweka. Hata hivyo, ujue. Simba akifariki, panya hutafuna ngozi yake. Ndviyo ilivyotokea. Yale ambayo hukuwahi kudhani yangetokea, yeshatokea zamani. Mafyatu waliogoma kufyatuka wakafyatua sasa wanafyatuliwa kama hawana akili nzuri.
            Nne, ungerejea, kabla ya kujinyotoa na kufyatua watu mbanta, ugepata kichaa. Maana, wengi uliodhania wafuasi wako sasa wanaimba ngonjera na nyimbo za kukukandia na kukukana. Juzi, nilisikia mmoja uliyemtoa mikoani na kumpa kipaza sauti akisema eti wewe hukukusanya gold! Si alirambishwa asali, wengi siyo walikusaliti tu, bali wanapmbana kulihalli usahaurike kana kwamba hukuwahi kuwapo na kutisha.
            Tano, mwaka jana kuna mafyatu waitwao ‘mamluki’ walikinukisha wote tukanuka hadi kufyatuana shaba. Wengine walifanyiwa kale ka mchezo ulikoacha. Wasiojulikana bado wapo. Waliwafyatua, kuwapoteza na wengine kuwanyotoa roho. Shaba zilitembea mitaani usipime.
Sita, walitokea mabeberu wakatuma mamluki wakatuonea wivu na kuja kuvuruga amani yetu. Walitutaimu siku ya uchaguzi wa amani na mshikamano. Walitaka kuuvuruga tukawavuruga ile mbaya tena kifyatufyatu. Siku hiyo, amani ilivugika hadi shaba zikageuka lugha pekee. Mwaka jana mwezi wa kumi tarehe 29 haitasahaulika kwa mafyatu siku walipokinukisha hawa mamluki hadi kisiwa cha amani kikageuka kisiwa cha vita na umwagaji damu ambavyo havikuwahi kutokea.
            Saba, pamoja hila na wivu wao, tunamshukuru Mungu, rahis wetu alishinda kwa asilimia 98. Mbili zilizobaki ziliibiwa na wapingaji wachoyo wa madaraka. Baada ya kukinukisha na kufyatuana, sorry, kuwafyatua mamluki, tuliunda tume ya kujichunguza lau tujue nani alizembea hadi kikanuka. Wapo mabeberu waliotucheka na kutuzodoa kuwa tunawezaje kujichunguza. Hebo! Bila kujichunguza, utawezaje kujisuta. Hawa walitaka tuite wengine watuchunguze halafu watusute wakati tunaweza kufyatua vyote viwili, yaani kujichunguza na kujisuta na kuwatuliza mafyatu waliofyatuliwa tokana na uzwazwa wao wa kukataa kufyatuka wakafyatua hadi wakafyatuliwa.
            Nane, nadhani unakumbuka wale mafyatu wa akina yero kule Ngolongolo. Walishafyatuliwa zamani gani. siku hizi wako ugosini wakijifunza kukata vikalio na kuacha na ngoma zao za kurukaruka. Ilibidi tuwafyatue ili kupisha uwekaji ili kujiongezea kipato.
            Tisa, kabla sijasahau, ule uwanja wako wa home ulishadoda. Sikujua kuwa wewe ndo ulikuwa bidhaa kuu iliiyokuwa ikiupa shavu! Baada ya kuondoka si kila kitu kiliondoka. Naomba unisamehe. Usidhani nilikufyatua ua kukusaliti. Hapana. Hata ile biashara yangu ya hoteli niliyokuwa nimefungua Chato niliishafunga baada ya kukosa wateja. Napanga kuihamishia kule Kizinkazi ambako siku hizi ndiko kunatesa. You know what I mean.
            Kumi, japo ulizuia watoi wako kushiriki siasa, siku hizi Jessie ni mheshi wa viti maalum. Tangu ulipoondoka aligeuka maalum kiasi cha kupewa kiti maalum tokana umaalum wake utokanao na wako.  
            Kumi na moja, unakumbuka ile kauli mbiu yako ya kutetea wanyonge? Tangu uondoke na unyonge ulikufuata hadi unatendewa kinyonge. Siku hizi, hakuna mnyonge hata mmoja. Ila wanyongaji bado wapo hasa wale maadui wa amani na mshimano wetu kama wale tuliowafyatua walipotaka kuvuruga uchaguzi wetu kwa vurugu badala ya kufanya hivyo kwa amani na mshikamano. Tuliwashika kwa mshikamano na kuwatia adabu kwa amani.
            Baada ya kuondoa unyonge, wapo waliopagawa hadi wakageuka machawa. Zamani chawa walikuwa wadudu. Siku hizi uchawa au kuwa chawa ni sawa na kuwa superstaa. Tuna machawa kila aina. Wako wa maza, wa faza, hata chawa wa machawa. Kuna machawa wadogo, wakubwa, wanene, walikonda na wengine kama hao. Pia, wapo wanaojipendekeza, kujikomba, kujituma, kutumwa na wa kila aina.
            Kabla sijasahau,  nadhani swahiba yako Rao aka Jaduong Maduong yule wa kaya ya jirani wakimuita baba mshaonana au hajafika. Si naye aliwageuka Gen Ziro w akule walipokinukisha akajiunga na Kasongeyeye mobali nangai. Acha afyatuliwe kuwa alijigeuza msaliti. Alisononeka hadi akaresha namba akiwa amechafuka. Kuna mafyatu wanaodai kuwa alifyatuka kwa sababu ya usaliti uliosababisha umwagaji damu.
Kabla ya kusahau, wajua? Si kwa Joji kichaka walimchagua chizi aitwaye Donnie Tarampu. We, acha ainyooshe dunia. Ninavyochonga, yupo anazipiga na waajemi kiasi cha kupandisha wese. Ila anazidi kuzidiwa pumzi hadi anaomba nimpe tafu.
            Mwisho, kuna busara ambayo sikuielewa ila leo naielewe. Kumbe asikuwepo na lake halipo! Kumbe hata kupe anaweza kuwa mkubwa na mwenye maguvu kuliko tembo aliyemnenepesha hadi akawa hivyo huku tembo akigeuzwa mdogo kuliko inzi. Du! Kumbe naota mchana!
Chanzo: Mwananchi Jtano leo.

Sunday, 15 March 2026

Yawezekana kufanikisha ndoa na mengine

Katika maisha ya binadamu, kuna mambo mengi ya kufanya na kutofanya. Kwa vile hii ni safu ya ndoa, leo, tutaangalia mafanikio na maanguko katika ndoa. Hapa, kuna swali huwa linatushughulisha sisi kama wanandoa tena wa muda si haba. Je, inakuwaje baadhi ya wanandoa huweza kufanikisha mambo yanayowashinda wengi katika ndoa wakati wengine wakishindwa kabisa japo wana mafanikio mengine nje ya ndoa?
            Inakuwaje mtu anakuwa kiongozi, msomi, au tajiri kubwa lakini anashindwa ndoa? Je, ni kupanga au majaliwa au ni kuonyesha namna ambavyo binadamu haawezi kupata vyote? Katika kudurusu hali hii, tutaanza mfano wa Malkia wa Uingereza marehemu Elizabeth (21 Aprili 1926 – 8 Septemba 2022). Huyu mama, tokana na usiri wake, hatuwezi kusema kuwa tunaijua ndoa yake vilivyo.
            Hata hivyo, kwa juu inajulikana. Pamoja na matatizo ya hapa na pale, Malkia alibainisha kuwa ndoa inaweza kuwa na mafanikio katika mambo ambayo wengi huwashinda hata kusababisha wawe na ndoa zenye changamoto na mazonge tokana na baadhi ya mafanikio yao.            
             Tunadhani Elizabth ni mmoja katika wachache waliokaa kwenye ndoa na mafanikio ya kiutawala kwa miaka mingi karibia kuliko wote. Kwani, aliishi kwenye ndoa kwa takriban miaka 74 na kwenye utawala kwa takriban miaka 64. Hii ni kutokana na baadhi ya matatizo ya wahusika kuwa kikwazo kwa ndoa zao kutokana na majukumu kiasi cha kutokuwa na muda wa kuimarisha ndoa yao.
        Je, huwaje kunakuwapo watu waliofanikiwa kitaaluma, kiuchumi, na mengine lakini wakashindwa katika ndoa? Pia, kwanini kuna watu waliofeli katika mambo mengine lakini wakafanikiwa katika ndoa?  Siri hapa ni nini? Mfano, unakuta mtu ni tajiri lakini maskini wa ndoa. Mwingine ni msomi wa kupigiwa mfano lakini asiye na ndoa au kama anayo, inayumbayumba au kukosa ladha na raha. 
               Wapo matajiri wa kuitwa utajiri lakini hawamo katika ndoa au ndoa zao zimevunjika. Jikumbushe watu waliofanikiwa kama vile Mfalme Charles wa Uingereza, Bill Gates, Donald Trump, Jeff Bizos na wengine ambao ni watu waliofanikiwa katika nyanja mbali mbali lakini ndoa ziliwashinda hadi zikavunjika au kuwa na maskandali kila uchao. Walinganishe hawa waliofanikiwa na watu wa daraja lao kama vile Tadashi Yanai tajiri mkubwa Japan, Warren Buffet, Zhong Shanshan tajiri mkubwa wa China, na wengine ambao ni matajiri wenye ndoa za kupigiwa mfano. Je, kuna siri gani katika kushinda na au kumudu taasisi tata lakini nyeti ya ndoa?
            Pia, lipo kundi la mabilionea ambao hawajawahi kuoa au kuolewa kama vile Andreas von Bechtolsheim, Diane Hendricks, Elon Musk, Oprah Winfrey, Michael Bloomberg, na wengine. Je, tatizo ni nini? Utakuta mtu maskini au asiye msomi ana ndoa imara kuliko ya tajiri ilhali wasomi na matajiri zinawashinda. Nenda mbele zaidi. Utakuta mama mrembo asiye na ndoa ilhali yule asiye mrembo anayo tena imara. Inakuwaje matajiri, wasomi, na warembo japo si wote wasiolewe lakini maskini, wasiosoma, na wasio warembo wakaolewa na kuishi kwenye ndoa imaara? Hapa kuna fumbo vile vile somo. 
        Jiulize. Ni wamama tena matajiri au wasomi aka mishangazi japo hatupendi kushabikia neno hili wangapi wanaishi bila ndoa tena wengine wakitamani au kutangaza kutaka kuolewa wasiolewe? Wakati huo huo, unaweza kumkuta muuza baa akiwa kaolewa na anafaidi ndoa!
        Je, hapa, tatizo ni wahusika au jamii? Nini suluhu ya kadhia hii? Maswali haya chokonozi na tekenyeshi kifikra yanajibiwa na the American Boys and Men (2025) ambalo linabainisha kuwa ni asilimia 50 tu ya wanawake wasomi wanaoolewa tena na wasomi wenzao. Nusu ya idadi iliyobaki, huolewa na watu wasio wasomi. Waliobaki wanabakia bila ndoa.
           Tumalizie. Ni wangapi unaowajua wanaojikuta katika hali hii tuliyodurusu? Je baadhi ya mafanikio ni chanzo cha maanguko katika ndoa na baadhi ya maanguko ni chanzo cha mafanikio katika ndoa? Ama kweli wahenga walinena kuwa Mungu hawezi kukupa au kukunyima vyote. Anakupa hiki au hivi na kukunyima vingine. Je, wewe kati ya mafanikio ya vitu na ndoa, unaridhika au kuchagua kipi? Kila la heri wanandoa na watalajiwa wote.              
Chanzo: Mwananchi Jpili leo.

Wednesday, 11 March 2026

Kwanini watoi wanaonewa bure?

Japo sijui umri wala sura zenu, kwa walengwao mjijuao, nitakuiteni waheshimiwa msiojulikana mnaofanya mambo yanayojulikana tena ya kuudhi. Nawapa shikamoo kama ishara ya heshima ila siyo kuwazeesha bali kuwasifia na kuwafurahisheni msiniteke, kunipoteza, hata kunidedisha kama wale wenzangu. Juzi, nilisikitika sana na kushangaa. Nilihuzunika na kuchukia namna wengine wanavyokasirika na kufyatuka kiasi cha kupayuka na kufyatua waliokuwa wakifyatua kwa vile walidai nanyi mliwafyatua. Cha mno, nilisikitika na kuogopa sana. Ni pale nilipoona mliowazunguka na kuwatumikia wakizuga na kuzugana badala ya kuwashauri wakaamua kujishauri.
        Wapendwa na waogopwa tena mlioko juu, kwanza, nikiri. Najua kayani tuna watoi watundu waliokosa adabu, wavuta bangi wanaodaiwa kupenda njuluku kiasi cha kuhongwa na kutaka kubomoa hata kuchoma moto kaya yetu pekee waliyotuachia baba na babu.
        Nimehuzunishwa na kushangazwa na wazushao kuwa hawa watoto watundu walihongwa tena na mbuzi dume wachome kaya moto. Wapi ushahidi? Ilinishangaza sana kuona mafyatu wazima wakifanya mambo ya kikumbaff kiaisi. Yawezekana wamefanya hivyo kutokana kuwa mafyatu wanaoweza kufyatuka na kufyatua lolote ima kugoma au kugopa kuwafyatua tukafyatuana kikaeleweka. Sijui ni kwa sababu ya uzushi au kutaka kukwepa lawama.
        Kuna niliowasikia runingani na kuwaona redioni baada ya watoi watundu kufyatuka, kufyatua na kukukera, hawataki fyatu yoyote alalamike wala kuulizia hatma yao. Wapo waliolalama na kulaani sana wapanzi walioshindwa kuwafunza watoi wao adabu hadi wakaikosa na kutishia kutuumiza wote kayani. Katu, sikubaliani na hii dhana, dhuluma, na rongorongo uchwara. 
Nadhani kama wangesoma na kucheza na watoi wa maza wa kuwazaa mwenyewe tena munene wenye tabia nzuri na mafanikio, hakika, nao wangekuwa nayo. Kama wangeshirikishwa na maza wa kambo kwenye kamati ya uendeshaji wa kaya yao kama wake hadi hata warume wao, yote yasingetokea. Hayo leo tuyaache.
        Kingine nijuacho, hawa watoi watundu wengi wanatoka shule za Kayumba. Kama wangesoma intaneshno na Kimombo media, wasingekuwa watundu hivi bali kama kuku wa kitasha. Wangekuwa wamezaliwa kwenye hos za bei mbaya, wasingekuwa na utundu wala utukutu bali utanuaji tena wa dezo. Hivyo, nadhani sababu ya watoi kuwa watundu hadi wakataka kuchoma kaya ni ukapuku wa madingi zao. Mtoi anayelala kwenye ngwarangwara akielekea shulee hawezi kuwa na adabu wala tabia. Hawezi kuwa sawa na wale wanaoendeshwa kwenye midude ya bei mbaya ambayo ni full viyoyozi kama wa wanene. Hawezi huyu maskini. Ni kama tunawaonea au hatuwaelewi. Kama tunawaelewa, basi hatuelewi, hawatuelewi na hatuelewani.
Wapendwa, nilishangaa kusikia eti watoi watundu walitaka kuharibu kaya yetu ilhali ilishaharibiwa baada ya kupigwa mnada na ndugu zetu wenye uchu wa njuluku tena wahongwao peremende, udohoudoho, na upuuzi mwingine. Nani zwazwa awahonge njuluku watoi wachome kaya ambayo si yao tena? Au ni wale wenye tabia za mbuzi dume? Nadhani hata mbuzi wanajua kuwa kaya yetu ya urithi ilishapigwa mnada. Hata hivyo, tukiwa wakweli, nani ahongwi nyumbani kwetu? Muonyesheni ili watoi waende kwake wajifunze. Mnakumbuka yule baba aliyetuacha alivyowahi kusema. Kuna kuwa lile shamba la Bwagamoyo lisiuzwe vinginevyo watakavyofanya hivyo wawe machizi na mataahira wasiojua ukubwa na manufaa yake. Je, halikuuzwa?
Yule baba japo alikuwa na yake kama ukali kupita kiasi hata ukatili kiasi cha kuwachapa wenzetu hadi wakatekwa, wakapotea, na kufa, pia, alikuwa na uzuri wake. Nakumbuka. Hakuwahi kupendelea watoi wake na kuwaumiza watoi wa kufikia kama ilivyo. Sikumbuki kuona mtoi wake hata mkwewe au mkamwana kwenye kamati yake ya kuongoza kaya. Kwa hili, sitaacha kumkumbuka mbali na kupambana na wale vidokozi waliokuwa wakiiba na kuramba sukari na kufanya wengine tunywe uji wenye chumvi.
Juzi, kuna watoi wakorofi walivunja vikombe na kupiga mateke sufuria na mambo mengine. Bahati mbaya, wale walinzi wetu si waliwaunguza mikono eti wakiwaadhibu! 
Mpaka nifyatukapo, wapo waliokimbia kiasi cha kutojulikana walipo. Wapo wanaodai kuwa waliuawa na miili yao kutupwa mbali pasipojulikana kama wale wasiojulikana japo wanatenda jinai na ukatili vinavyojulikana. Wazushi walizua na kuzusha kuwa wale walinzi waliwaua na kuwatupa baharini ilhali maza yao akiangalia na kuwalaumu.
        Juzi, nilipita kijiweni. Niliyosikia yanatisha. Kumbe watoi watundu wenzao wanasema lazima walinzi washikwe na kushikishwa adabu hadi wawaonyeshe wenzao au miili yao badala ya kujitoa ufahamu na kukaa kimya kana kwamba waliopotea ni wadudu. Wanataka kujua nani alimuamuru kuua watoi wachanga tena kwa kuonyesha utoto wao. Mashambenga na wabaya wanazoza wazi kuwa kuwa kuna ubaguzi hasa kuwaacha walinzi wawaue kwa vile ni wana wa kufikia.
        Nani kawalipa nani na wangapi, nini, kiasi, na lini ili apate nini na kwanini? Je, ‘vyombo’ vilikuwa wapi? Tumuamini na kutomwamini nani?
Chanzo: Mwananchi Jtano leo.

Sunday, 8 March 2026

talaka yenu inawafundisha nini watoto wenu?


Si mara ya kwanza wala ya mwisho kujadili talaka. Leo, tutadurusu talaka na madhara kwa watoto wa watalaka. Japo talaka ni jambo la kuhuzunisha, kwa watoto wa watalaka wenye busara na wanaojua na kuchukia madhara ya talaka, linaweza kuwa funzo kubwa katika maisha yao. Hata hivyo, inategemea na wahusika. Wapo wanaoweza kuchukia talaka na kuhakikisha watakapokuwa na kufunga ndoa, hawatapenda kupitia waliyopitia. Pia, wapo, hatujui tuwaiteje wanaoweza kuona talaka kama jambo la kawaida.
Tutatoa mfano wa rafiki yetu toka Jimboni Darfur, Sudan. Huyu bwana ana mke mmoja. Kanada, ndoa za mitala  haziruhusiwi. Ajabu, huwa halali kitanda chumba wala kitanda kimoja na mkewe. Siku moja walitutembelea kama familia ya kulala kwetu. Ilipofika wakati wa kulala, tuliwaandalia chumba mke na mume Pia, kuwaandalia watoto wao vyumba viwili tofauti. Bila hili wala lile, wanandoa walituita kona. Walisema vyumba vitatu tulivyowatengea vilikua vingi. Walihitaji viwili tu. Tulishangaa. 
Tuliuliza kwanini wakati walikuwa wana watoto jinsia tofauti ambao tusingewalaza chumba kimoja. Walijibu kuwa watoto wa kike wangelala na mama yao, na wa kiume wangelala chumba kimoja na baba yao. Hatukuwapinga. Ila tuliwashangaa.
Zamu yetu ilipofika kuwatembelea, walitupangia vyumba viwili badala ya vitatu. Walitushangaa tulipouliza ni kwanini? Marafiki hawa walisema kuwa, kawaida, hawalali mke na mume pamoja. Tulishangaa hakuna mfano.
Hata hivyo, katika kuwadurusu kujua ni kwanini hawalali chumba wala kitanda kimoja, mume alijibu kuwa walikuta wazazi wao wakiwa na utaratibu huo. Katika kuzidi kuwadurusu, tulishangaa kugundua kuwa wazazi tajwa walikuwa na wake wengi. Hivyo, kwa kuzingatia kuwa waliishi kwenye vijumba vidogo vilivyojengwa sehemu moja ndani ya boma moja. Baba alikuwa na kijumba chake ambapo kila aliyemhitaji huenda kwa zamu kupata chakula cha usiku.
Tulizidi kushangaa ni kwanini wawili hawa waliamua kulala mbalimbali wakati ndoa yao ilikuwa ya mke mmoja. Jibu tulilopewa ni “tulikuta hali hii.”
Je, tukirejea kwenye talaka, hii inafundisha nini? 
Funzo la kwanza ni kwamba watoto, mara nyingi, huathiriwa na matendo na tabia za wazazi.
Pili, tuligundua kuwa kuna mambo watoto hufuata bila kuyapinga wala kuyadurusu na kujua maana na sababu zake.
Hivyo, basi, linapokuja suala la talaka, yawezekana kabisa watoto wa wataliki wakaona ni jambo la kawaida kiasi cha kutoona madhara yake kwao.
Kama tulivyogusia hapo juu, pia wapo wanaoweza kuichukia talaka wakaitahadhari katika maisha yao ya utu uzima. Maana, hata katika kisa cha marafiki zetu hapo juu, tuliambiwa kuwa wapo Wadarfur wanaolala kitanda kimoja na wake zao hasa wawapo kwenye nchi kama Kanada zisizoruhusu mitala. Tuliwabana na kuwauliza ni kwanini hawa hawafuati mila. Majibu yalikuwa tofauti. Walisema hii ni kutokana na usomi au kuiigiza ukristo na uzungu.
Je, ukiachia mafunzo tuliyotaja hapo juu, wewe unajifunza nini? Unawahukumuje hawa wanaofuata mila bila kuhoji? Je, wewe unayo mila gani uliyorithi kwa wazazi wako ambayo yaweza kuwa hasi na bado ukaifuata au ukaikataa?
Tukiachia mbali madhara ya kimahusiano, talaka yaweza kuwa chanzo cha ukosefu wa amani na raha kwa watoto. Kwani, huishi kwenye mvutano wa nani wawe naye baina ya wazazi wawili walioachana. Tunaye rafiki yetu ambaye ni tajiri wa kupigiwa mfano. Huyu baba alitalikiwa na mkewe. Wanao watoto wanne wa kike wawili na wa kiume wawili watu wazima. Kati yao, ni mmoja tu ameolewa. Katika maongezi naye mara nyingi, huwa anasema kuwa Watoto wake watatu ambao hawajaoa wala kuolewa huwa hawapendi kujadili suala la ndoa na yeye.
Pia, Watoto wake huwa wanaepuka kutaja majina ya baba au mama yao wala mambo yao kulingana wako nan ani. Jambo hili, haliwaathiri Watoto tu bali hata baba yao. Kwani, siku zote ana wasiwasi kuwa talaka yao imewaathiri vibaya watoto wao. Hayo ni machache tunayoambiwa. Kwa mujibu wa wataalamu wa mahusiano, ndoa, na saikolojia, yapo mengi hata ya kiakili na kiafya kwa ujumla kama msongo wa mawazo, chuki zisizo na sababu, hasira, upweke, na mengine mengi.
Ni vizuri kujua. Talaka ni hatari.
Chanzo: Mwananchi Jpilil leo.

Tuesday, 3 March 2026

Nitapiga marufuku kuzaa fyatuland


 Siku hizi, mambo kuwa si mambo. Maisha yamekuwa magumu. Napanga kutangaza sera ya kuzuia mafyatu kufyatua watoi japo kwa muda. Naona yule anatikisa kichwa akidhani mibangi imenifyatua hadi nikafyatua kitu hiki kifyatufyatu. Hapana. Nina sababu nuzuhu za kufanya hivyo. Twende kwenye hoja. Napanga kupiga marufuku kufyatua watoi hadi mambo yatakaporekebika na kufaa. Hivyo, zifuatazo ni sababu za kufanya hivyo.

Mosi, hakuna uhuru wa kufikiri kwa sasa. Hivyo, sitaki mafyatu wafyatue watoi mazezeta au wakaokataa uzezeta na kuishia kupatilizwa kama siyo kutekwa, kupotezwa, na kunyotolewa roho. Nani anataka mtoi wake atekwe au kupotezwa kwa kujiingiza kwenye dhambi ya kufikiri hadi anaishia kupinga?
        Pili, katika utafiti wangu binafsi wa kifyatu, nimegundua kuwa watoi wanazaliwa na msongo wa mawazo ambao huwazeesha hata kabla ya kuacha ziwa tokana na misongamano ya karibu kila kitu. Wanaamka usiku wa manane na kwenda skuli na kurejea home. Pia, wanabanwa kwenye ngwarangwara, madarasani, na kila mahali. Hapa, sijagusia wanavyobanwa kwenye mbavu za mbwa za kupanga. Funga kazi ni pale wengi wanapobanana hata vitandani au kwenye makochi walalamo. Kwani, hayapo? 
Hii huwasababishia woga wanapoona ngwarangwara na tukutuku vikivunja sheria mchana kweupe. Wanapata msongo wa mawazo zaidi wanapovuka barabara kwa kuogopa kugongwa na hawa wavunja sheria wasioshikishwa adabu. Hii inawaathiri kiakili na kimwili. Hivyo, kuendelea kuwafyatua ni kufyatua kaya yenye changamoto kubwa kiakili na kimwili. Nani analitaka hili? 
    Mfano, katika pitapita yangu kwenye miji mingi ya Fyatuland, niligundua kuwa kuna makelele ya kuua fyatu. Bahati mbaya yameruhusiwa chini ya visingizio kama vile biashara, kuburudisha, kuhubiri, kupayuka tu, ving’ora, na uhuru wa kila fyatu kuwa navyo.
        Tatu, sitaki mafyatu wafyatue vitoi vitakavyobanwa kama wao. Zamani tukifyatuka na kupayuka tulivyotaka. Siku hizi, fanya hivyo, ufyatuliwe kama siyo na maisha, basi watoi wenyewe hasa usawa huu ambapo adabu na maadili vimetoweka kama siyo kutekwa, kupotezwa, na kufishwa.
        Mbali na mibanano ya kimiwili, ipo ya kiakili. Usipojikomba, kusifu, na kuabudia, unakuwa hatarini. Dawa ni kukaa kimya. Nayo ni ugonjwa. Maana, mawazo hujaa na kuvia kichwani kiasi cha kuchizika taratibu. Maisha gani haya? Sijui kwanini hawa wanaotubana hawajui kuwa tusipoongea tunaishia kuchanganyikiwa baada ya kuchanganywa na wachanganyaji tokana na kuchanganya mambo!
        Nne, kwanini kufyatua watoi watakaofyatuliwa na umaskini usababishwao na upigaji njuluku za mafyatu ambao husababisha msongo wa chuki, hasira, na kichaa hata kutaka kujinyotoa roho? Wakati tukiminywa tusiongee, wapo wanaotupigia makelele wakitutisha au kuwasifia watubanao! Siku hizi, hata mimba zinabanwa ima tokana na ukosefu wa madawa, vifaa, na rushua. Hakiji kitegemezi hadi njuluku ikutoke!
        Tano, utafiti umegundua kuwa sababu na shida zote vimeungana. Baada ya hizo sababu hapo juu, kuna hili suala la msuguano wa kimawazo ambapo kutofautiana kumegeuka kosa la jinai. Huu nao huchangia sana matatizo tajwa hapo juu. Cha mno, hili husababisha matatizo mengi kiasi cha waathirika kuishi kwa kutegemea visungura kama njia ya kujiliwaza, kujipoza, na kusahau matatizo. 
Hili nalo limeongeza matatizo mengine kama utegemezi wa urahibu, udokozi, wizi, jinai, ukosefu wa maadili, adabu, aibu na mengine kama hayo. Hii imefanya nifyatuke ahead of time. Katika kufanya hivyo, nimegundua kuwa baada ya hayo matatizo na mazabe hapo juu, waathirika wataanza kutegemea vipanya hadi paka wawachukie kwa kusababisha ushindani pale bei ya visungura itakapopaa. 
Hii pia ina madhara yake. Watoi na waathirika wengine wataanza kubet ili watengeneze njuluku wasijue wajinga ndiyo waliwao! Nani aliwahi kuukwaa kwa kubet kama siyo kuishiwa akili na ubunifu? Baya zaidi, jinai hii imehalalishwa na kuonekana kama uwekaji wakati ni uchukuaji utokanao na uoza na uzwazwa wa kimfumo?
        Sita, nimeamua kuchukua uamuzi huu ili kuwaepusha mafyatu kufyatua vitoi vilivyojaa chuki, hasira, kukata tamaa, na mengine mengi tena yasiyo na sababu za msingi zaidi ya ubinafsi, uchoyo, upofu, na uzwazwa? Nani anapenda ajenge jamii ya woga kiasi cha mafyatu kufikia hata kuogopa vivuli vyao kama kule kwa wadanganyika? Nani anapenda kuwa na jamii hata inayoogopa wasiojulikana wala visivyojulikana? Nani anapenda kujenga jamii ambayo haina utaratibu unaoeleweka hadi fyatu akiona ndata wanaopaswa kumlinda anazimia kwa mashaka na woga?
        Saba, nimegundua kuwa hali tajwa hapo juu hufanya mafyatu ima wageuke au wafikiri kama wadudu. Hujasikia wanaojiita chawa, funza, kunguni, hadi luba? Kesho, sitashangaa wakijiita au kuitwa minyoo kama siyo virusi.
        Nane, wale wasioweza kugeuzwa wadudu, waweza kuwa majambawazi. Tokana na kukosa matumaini, mipango bora, na ubunifu, watoi ima hujiingiza kwenye uchangu hata ushoga kama siyo jinai za kila aina. Nani anataka ajenge kaya ya jinai usawa huu ambapo mapilato nao wamesongwa kiasi cha kutoa adhabu kama hawana akili nzuri? Hapa, sijaongelea ndata ambao nao siku hizi wamegeuka miungu tokana na kuwalinda miungu wanene kwenye jinai yao.
        Du! Nimesemaje! Kama ninabanwa na kusongwa na jinamizi!
Chanzo: Mwananchi Jtano leo.

Sunday, 1 March 2026

Msifanye ndoa yenu kuwa maabala

Tunaamini wengi wa wasomaji wetu wanaijua maabala. Maabala ni mahali ambapo hufanyika majaribio ili kupata nyenzo na ujuzi wa kufaa katika maisha. Japo si maabala zote, mara nyingi, maabala zimalizapo kazi zake au hata kutoleta matunda au kufikia malengo yaliyotarajiwa hufungwa. Ni maabala za taasisi za kielimu za kisayansi ambazo daima huendelea kuwepo.
Kama ada yetu, leo, tutadurusu na kuongelea ndoa na wanandoa. Tutakita kwenye namna wanaofanya kosa kubwa na kukubali kujigeuza au kugeuzwa maabala. Kwa watu wa Pwani wanajua neno chuo au vyuo. Kuna baadhi ya makabila ambayo ndoa zao ni kama maabala. Mama au baba anaingia kwenye ndoa na kuivunja na kudandia nyingine. Hapa, ndipo dhana ya chuo inapoanzia. Utamsikia mama akiulizwa “chuo changapi hiki? bimaana ni ndoa ya ngapi.
Pamoja na kuwa mila iliyokubalika kuoa na kuolewa na kuachika, si jambo jema kwa binadamu. Lina madhara mengi kibinafsi, kijamii, kimwili, kiakili, kiuchumi hata kimaisha Je, hii husababishwa na nini? Hatuna jibu moja wala jibu rahisi. Yapo mengi yanayosababisha umaabala huu. Moja, yaweza kuwa kuingia kwenye ndoa bila kufanya utafiti na kuielewa mila na shurti zake.
Pili, ni tabia ya wahusika. Wapo wanaokwapukia na kupwakia ndoa bila kujiandaa au kuandaliwa. Zamani, kulikuwa na taasisi za Kiafrika za kuwaandaa watarajiwa kuingia kwenye ndoa. Ziliitwa jando kwa wanaume na unyago kwa wanawake. Taasisi hizi zilitofautiana baina ya makabila. Tofauti hii ilitokana na utofauti wa mazingira na mila za jamii husika. Hata hivyo, zilifanana kwa kitu kimoja kikuu. Vijana wa kike na kiume walipelekwa sehemu maalumu na kufunzwa na kufundwa na makungwi namna ya kuishi katika ndoa.
Katika jando na unyago, yapo makabila ambayo yalitahiri vijana wa kiume na mengine hata wa kike. Kutahiri wanawake, kuna madhara makubwa kimwili na kiakili. Hivyo, zama hizi, mila hii imepitwa na wakati.
Kwa ufupi, katika jando na unyago, wahusika walifunzwa na kufundwa juu ya namna ya kuwa watu wazima wake na waume. Walifundishwa miiko ya ndoa na mambo mengine muhimu ili kuwasaidia kuishi maisha ya ndoa kwa furaha na ufanisi. Hata hivyo, siku hizi vijana wanafundwa na mitandao ambapo mambo mengi ya hovyo na uongo hufundishwa na wale wanaotaka kupata wafuasi ili wapate fedha.
Hata hivyo, baada ya ujio wa dini za kigeni, taasisi hii adhimu na muhimu iliuawa na kudharaulika kiasi cha kusababisha madhara makubwa kwa taasisi ya ndoa. Ni bahati mbaya. Si wengi wanashuku wala kuhoji uvamizi huu wa kimila ambao kimsingi, si chochote bali ukoloni kama ukoloni mwingine wenye lengo la kuwabadilisha wahusika ili kuwatawala na kuwanyonya.
Tatu, ni msukumo wa jamii iliyoacha maadili yake na kupwakia maadili ya kigeni bila kuyajua vizuri na athari zake hasi kwa walengwa. Mfano, siku hizi mabinti wengi hawajifunzi kunga za nyumba kama vile heshima, mapishi, usafi, uvumilivu, usiri, na mengine mengi ambayo zamani, yalithaminiwa sana. 
Nne, kukua kwa teknolojia. Tangu kuibuka kwa matumizi ya mtandao, mabinti wengi hawana nafasi ya kujifunza stadi za maisha. Mfano, wapo wasiojua kupika kabisa. Wanachofanya ni kwenda kwenye mitandao na kutafuta recipes za mapishi au mapishi, hatuna Kiswahili chake.
    Kama tujuavyo, japo binadamu ana uwezo mkubwa wa kujifunza, si mara zote huelewa anachofundishwa. Huweza kuelewa anachofundishwa kupitia kurudiarudia ndiposa huelewa na kukubuhu. Mapishi yatokanayo na kujifunza pindipo mhusika atakapo kupika hayamuweki kwenye nafasi nzuri ya kuyamudu. Kuna usemi kuwa njia ya kuingia kwenye moyo wa mwanaume hupitia tumboni. Hivyo, chakula kina nafasi kubwa katika kuimarisha au kudhoofisha ndoa.
Hata hivyo, tokana na usasa, stadi za mapishi zinaonekana kama jambo la zamani. Hapa, ndipo umaabala unapoanzia na kutamalaki. Pia, tunashauri jamii ianze kurejea mila na utamaduni vya zamani vinavyofaa na kuacha visivyofaa. Hii itasaidia kuepusha ndoa na wanandoa kuishia kuwa maabala na kujenga jamii ya kimaabala ambayo haidumu.
Chanzo: Mewananchi Jpili leo.