The Chant of Savant

Wednesday 1 September 2010

Kwani Kikwete ana tatizo gani?




Hiyo dummy ya cheki imeandikwa dola laki mbili kwa maneno na dola 300,000 kwa namba. Je hapa Kikwete alipewa cheki ya dola ngapi? Mbili au tatu? God know how bogus this guy is.
Kwa wanaofuatilia utendaji mbovu wa rais Jakaya Kikwete, watakubaliana nami kuwa si mtu makini wala hajifunzi. Kama anajifunza basi ni mzito na mgumu wa kufanya hivyo na saa nyingine anajifunza kutojifunza kabisa. Hebu angalia hiyo picha hapo juu. Je unajifunza nini toka kwa rais wako anayemaliza muda wake akiwa amezungukwa na kila aina ya tuhuma kuanzia ufisadi hadi kutokuwa muaminifu katika ndoa?

Arusha alifungua hoteli iliyokuwa imevunja sheria. Mbeya amepewa kadi feki za CHADEMA. Hapa bado hatujagusia mama wa kashfa-kusaini mswaada uliokuwa doctored. Bado hatujagusia uchakachuaji wa mafuta na uraia wa Hussein Bashe ambao inasemekana Kikwete katumiwa na mwanae kumkomoa adui yake. Hapa bado hatujagusia suala la umri wa aliyekuwa mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM, Hamad Yusuf Masauni aliyepitishwa na Kikwete kwa kuingilia uchaguzi wa jumuia hiyo.

Hapa bado hatujagusia uteuzi wa mkuu wa wilaya mkoani Shinyanga na kumbatilisha siku iliyofuata. Hapa ikumbukwe. Bado hatujagusia upayukaji wake aliposema hivi karibuni kuwa ukiona misongamano ya magari barabarani ujue ni dalili za maisha bora.
Huyu ndiye Kikwete anayetaka kuwaingia watanzania mkenge kwa mara nyingine tena bila aibu.

Angalia mafisadi wakubwa ambao ni marafiki na washirika zake kama Rostam Azim, Edward Lowassa, Andrew Chenge, Jaffer Sabodo, Andy Chande, Benjamin Mkapa na wengine wanavyozidi kutesa huku umma ukiteseka. Angalia mwanae na mkewe wanavyomtumia kuichafua ikulu kwa kuifanya nyumba ya biashara tena ya aibu. Angalia uteuzi wake wenye utata wa kujaza nafasi mbali mbali.
Uliyachunguza na kuyajua yote ya Kikwete unapata kinyaa. Hakika Kikwete si kingine unachoweza kuelezea bali ajali ya kisiasa. Hivi unategemea mtu anayeshauriwa na mkewe, mwanae, waramba viatu kama Salva Rweyemamu, Yusuf Makamba na makapi kama Tamwe Hiza kweli awe na bao?
Hatumchulii. Yatafichuka mengi hasa pale watanzania watakapofanya kosa wakaridhia arejee madarakani iwe kwa kumchagua au kukubali kuibiwa kura.

Chanzo: Freethinking Unabii.

3 comments:

Anonymous said...

Tukipata free thinking kama hizi, hakika Tanzania itakuwa mbali. Nawalilia Watanzania wanaopoteza muda wao kutokana na njaa zao na kwenda kujaza mikutano ya huyu bwana kusikiliza upupu wake. Credibility ya Mh ni sifuri kabisa.

Anonymous said...

This man is really a bogus! he is disgusting! aaaghhhhhhrrrrr!

Anonymous said...

This man is really a bogus! he is disgusting! aaaghhhhhhrrrrr!