vya habari viliripoti jana kuwa rais Jakaya Kikwete alimuokoa teja mmoja maarufu Ray C. Baada ya kufichuka kwa habari hizi ambazo wengi wameona kama ni "roho" nzuri ya mheshimiwa rais, nimeonelea nirejeshe kadhia nyingine itokanayo na mihadarati ambayo ni kifo cha kutatanisha cha mbunge wa CCM Amina Chifupa baada ya kushupalia biashara hii. Je kwanini rais hakuingilia kati kumuokoa? Wengi watashangaa rais angemwokoaje wakati hakuwa teja. Nimaanishacho ni kwamba je rais anahitaji kuokoa mateja mmoja mmoja tena maarufu au wote kwa kuwakamata wauza mihadarati ambao alitwambia mwaka 2006 kuwa ana orodha yao? Je Kikwete anatumia kadhia ya Ray C kujitafutia umaarufu wa bei nafuu au ameshauriwa vibaya? Je Kikwete yuko serious kupambana na mihadarati au ni usanii wa kawaida? Je mbinu anayotumia Kikwete inaweza kuleta suluhu kwa tatizo au kuwa sehemu ya tatizo? Je wasio "masupastaa" wataokolewa na nani? Je Kikwete alidhamiria kumsaidia Ray C au kutumia umaarufu wake kujionyesha kama mtu anayejali? Je wewe msomaji unampa ushauri gani ili apambane na tatizo lenyewe badala ya mashina kama ilivyotokea kwa Ray C?