The Chant of Savant

Friday 14 December 2012

Salma Kikwete na nyani na kundule



Watanzania Watakiwa Kujenga Utamaduni Wa Kujisomea Vitabu

Wengi wanajiuliza kwanini yeye haonyeshi mfano na badala yake anatumia muda mwingi kuzurura na mumewe? Kwanini hamshauri mmewe kuwafukuza mawaziri na watendaji wengi aliowateua wanaojulikana kughushi vyeti vya shahada? Je yeye ukiachia mbali kutumia WAMA kujipatia pesa amefanya nini binafsi kuongeza kiwango chake cha elimu?

Na: Heka Wanna na Shakila Galus,MAELEZO

MWENYEKITI wa WAMA Mama Salma Kikwete wito kwa wananchi tabia ya kujisomea vitambu na machapisho mbalimbali ili kujiongezea maarifa yatakayowawezesha kujiletea maendeleo.

Mama Kikwete alitoa kauli hiyo kwenye Makumbusho ya Taifa leo jijini Dar es salaam wakati wa uzinduzi wa makatba kwa ajili ya watoto na watu wazima.

Alisema kuwa elimu ndio silaha pekee ya kukabiliana na maadui watu ambao ni ujinga,maradhi na umaskini na hivyo kujiletea maendeleo.

Mama Kikwete aliongezea mbinu za kujiendeleza kimaisha zinapatikana pia kwa njia elimu kupitia vitabu na machapisho mbalimbali yanayopatikana kwenye maktaba mbalimbali ndani na nje ya Tanzania.

Alisema kuwa hiyo itasaidia katika kuongeza maarifa kwani kutakuwa na vitabu,kompyuta na mitambo ya mawasiliano ambayo itawawezesha watumiaji kupata elimu ya taaluma mbalimbali.

Aidha Mama Kikwete aliwasihi watumishi wa Makumbusho hiyo kuwa ni jukumu lao kutunza maktaba hiyo ili isaidie kukidhi malengo ya kuanzishwa kwake kwa kuandaa taratibu bora za kudhibiti matumizi yasiyo na tija ya maktaba ikiwemo upotevu machapisho na vitabu mbalimbali na uhalibifu wa vitabu unaofanywa na watu wasiotaka maendeleo.

Mwenyekiti huyo WAMA alimshukru Balozi wa Korea Kusini Young Shimo Dho kwa niaba ya nchi yake kwa msaada wa vitabu na vifaa mbalimbali kwa ajili ya maktaba hizo mbili .
Chanzo: Mjengwa Blog.

No comments: