How the Berlin Conference Clung on Africa: What Africa Must Do

How the Berlin Conference Clung on Africa: What Africa Must Do

Thursday, 30 October 2014

Je araobaini ya Blaise Compaore imefika?




Palais Kosyam the state house of Burkinabe

Jenerali Honere Troure aliyetangaza kusimamia serikali ya mpito

Hali ilivyo ni kwamba Blaise Compaore imla wa taifa maskini la Bukinabe amefikia arobaini yake. Compaore alichukua madaraka mwaka 1987 baada ya kumpindua na kumuua rafiki yake rais Thomas Sankara aliyependwa na kusifika kwa usafi na uzalendo wake. Wengi walishangaa na kulaani kitendo hiki cha kinyama na hovyo kufanywa kwa rafiki. Hivyo, wengi wangependa na wanangoja kwa hamu kuona mwisho wa muuaji na fisadi huyu anayetuhumiwa kutumia viungo vya mazeruzeru kutambikia ili aendelee kukaa madarakani. Je jeshi la nchi hiyo litaungana na wananchi kuangusha imla wao? Je jeshi litatumia fursa hiyo kutwaa madaraka kama ilivyotokea Misri au kukaa kati kama ilivyotokea Tunisia? Je Compaore atafanikiwa kuzima nguvu ya umma? Je Burkinabe itafufua matumaini kuwa Afrika Kusini mwa Sahara (SSA) bado inaweza kufanya kile walichofanya wenzao wa Maghreb? Je kikinuka Burkina, nani atafuata, Chad, Sudan au Uganda? Natamani na Danganyika waamke na kuiondoa CCM kwa staili hii. Je kuna haya ya kukata tamaa? Lolote lawezekana? Tuzidi kuomba. Long live Burkina, Long live Thomas Sankara's spirit working in the people of Burkina. Kwa kinachoendelea, BONYEZA HAPA.

2 comments:

Anonymous said...

Bongo hawawezi hii
Waoga sana
Natamani ije Tanzania hii
Ntajisikia Nipo akhera

Ndugu Nkwazi N Mhango said...

Anon usemayo kweli ila wanaogopa bure hasa usawa huu ambapo ICC inawapatiliza wezi na wauaji wanaodhulumu watu wao. Wako wapi akina Chaz Taylor na Laurent Gbagbo aka Badboy?