How the Berlin Conference Clung on Africa: What Africa Must Do
Friday, 16 June 2017
Adui Magufuli si Magazeti bali Yeye Mwenyewe
Kufungiwa kwa gazeti la Mawio ni ushahidi kuwa rais John Magufuli hapendi kukosolewa wala hana nia ya kupambana na ufisadi kama anavyojitapa. Gazeti hili lilifungiwa baada ya kuripoti habari toka bungeni ambapo baadhi ya wabunge toka upinzani walipendekeza marais wastaafu Jakaya Kikwete na Benjamin Mkapa ambao wanajulikana dhahiri kwa kuingiza Tanzania kwenye matatizo ya kiuchumi tokana na tamaa zao. Wanaojua historia ya ufisadi Tanzania, wanajua kuwa na Magufuli ni sehemu ya mfumo wa kifisadi ambao alitaka kuukabili. Hata hivyo, kwa hali ilivyo, ni kwmba Magufuli punde tu atarudi kwenye mfumo na kuwa mmojawapo kama alivyokuwa. Vinginevyo, asingepoteza muda kuwalinda wahalifu wanaojulikana hata kama wana madaraka makubwa tu. Nadhani hapa tatizo ni kwa Magufuli kuamua kuwatumikia wateule badala ya watawaliwa. Je anahofia yake naye yasifumliwe hasa ikizingatiwa kuwa si msafi kama anavyoonekana? Rejea utwaliwaji wa nyumba za umma wakati akiwa waziri husika ukiachia mbali kashfa ya hivi karibuni ya mabilioni yaliyopotea kwenye wizara yake ya mwisho.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment