Wachukuaji, wezi na makuwadi wao wamekuwa wakificha dhahabu na madude mengine na kuyasafirisha ughaibuni huku walevi–sijui wa ujinga au upumbavu kama siyo ulevi wao–wakishuhudia kana kwamba hamnazo wasiojua faida ya madini husika. They opened and offered everything cheaply. Where did get the oomph to commit this goof? What cheap shrimps that they’re!
Tokana na wizi huu wa kikatili, napanga kuwekeza kwenye smelter au kinu cha kuchenjua haya madude ili kaya iendelee. Kaya imeliwa mbele na nyuma kiasi cha kugeuka kichwa cha mwendawazimu tokana na wendawazimu waliofanya uendawazimu wa kuruhusu ujambazi huu kwa miaka takriban 20. Hapa Ben Nkapa atantambua.
Napanga kuwa na sehemu ya kuchenjua vichwa vyote vilivyohusika kufanya mdudu haya hili nipembue na kujua kujua madudu yaliyojaa vichwani ili nipate namna ya kuwatibu. Hapa lazima nimshauri dokta Kanywaji kuwatumbua bila kuangalia sura wala vyeo wale wote walivyowahi kushika kiasi cha kuruhusu utapeli huu wa kichangudoa kimaadili. Hawa lazima nichunguze akili zao kuona zimekeketwa au kunajisiwa kiasi gani. Walitumia akili gani, zaidi ya masaburi, kuuza madini kama peremende? Wanadhani mzee Mchonga aliyegoma kuyagema ili kungoja wabongo wakomae kielimu alikuwa juha kama wao.
Najua mradi huu utaniingizia minjuluku hadi niwe miongoni mwa mabilionea halali wa kaya yetu ambao si wanufaika wa kuwanyonya wala kuwaibia walevi kama yule wa Richmond anayeitwa bilionea wakati ni jambazi. Hapa sijaongelea yule gabacholi mtoto ambaye kampuni za baba yake zinasifika kuwanyanyapaa, kuwanyonya hata kuwabagua wafanyakazi wa Kiswahili lakini–tokana na ulevi na utaahira wa walevi–bado wanamwita bilionea wakati ni kibaka wa kawaida.
Tokana na kuwa na smelter yangu iitwayo Mlevi Smelter, naamini haja jamaa zangu wa DRC na kwingineko wanakopigwa na kufanyiwa kitu mbaya wataleta madude yao niyachenjue na kunusuru chumi zao.
Juzi nilisikia Akasia wakipinga uchunguzi wa maprofesa wenzangu kuwa ulikuza mambo.kwani hawajui kuwa tunajua kuwa walikuwa wakijifanya wanapata dhahabu kidogo wakati wakiificha nyingi kwenye michanga? Sasa kiboko yenu mtanikoma. Nakwenda zangu kuongea na mshikaji wangu Putin anipe smelter nikawakomesha wapumbavu nyie. Mnajiita wawekezaji wakati ni wachukuaji! Kumbaffuni kabisa. Mshindwe na mlegee kabla sijawalegeza. Na hapa sitakuwa na cha mswalie Mtume wala nini. nitawashughulikia mbele nyuma kushoto kulia hadi mnakoma. Juzi kihiyo mmoja alinishangaza kuwa si rahisi kununua smelter tena kwa kaya! Wow! Hiyo smelter ya dola milioni 500 maniona dili wakati kaya ina mradi mkubwa kama wa kujenga reli? Nyinyi ni wavivu wa kufikiri kama mzee wa uvivu wa kufikiri aliyeanzisha sheria ya kugawa madini hapo mwaka 1998. Ukimuona na bichwa kubwa utadhani anazo kumbe hovyo! Jitu linakuwa vivu la kufikiri halafu linawatukana walevi eti ni wavivu wa kufikiri. Sasa hapa nani mvivu wa kufikiri kati ya walevi na waandishi wa umbea huyu mjinga aliwaita wavivu wa kufikiri asijue ataishia kuwa bingwa uvivu wa kufikiri.
Kuna milevi kwenye kaya yetu hata ukiinyonga au kuipiga risasi wala huna hasara. Minyimana hii yenye sura ya binadamu haipaswa hata kula. Kwani, si binadamu. Na hivyo, haistahili kufaidi haki za bindamu. Kuna mikumbaff ina sura kama yetu lakini si binadamu. Bahati mbaya mingine inaitwa miheshimiwa huku mingine ikilipwa hata mirupurupu ya kustaafu utadhani iliwahi kufanya kazi yoyote zaidi ya kuuza walevi na madini na raslimali zao. Ama kweli, mijitu kama hii ni mitoto si riziki na stahiki yao ni lupango. Tuna mimobutu na misani abacha kibao kayani huku mingine ikichekacheka hovyo na mingine kujifanya zinachemka na kuongea na kupokoma bila kukoma kumbe mivivu ya kufikiri. Ningekuwa dokta Kanywaji, kuna mijamaa tena mizee mizima ingeozea lupango kama siyo kuiramba shaba. Hebu fikiri; tangu mwaka 1998 kaya imekuwa ikifanyiwa kitu mbaya kana kwamba haina viumbe wenye ubongo.
Juzi si nikaenda kwenye kaya ya manyang’au kukuta eti yakitangaza kuwa yanazalisha tanzanite! Kama nitashangaashangaa kuleta smelter, siwezi kushangaa haya manyang’au kuileta na kuanza kuilangua kaya yetu.
Kabla ya kusahau, nimesema nitakuwa n aka-smelter kadogo ka kuchenjua vichwa. Nitaanza na cha profwedheha Muongo, Kajuamlo, Denjaman Makapi, Njaa Kaya Kitwitwi, Dan son of Jonah, Joni Ngereza, Ni Zero Kadamage na mibunga mingine inayojulikana kuasisi ujambazi na uhujumu huu wa kaya. Nikimaliza hapa lazima na majambazi ya Kagoda, Richmond, Escrow, EPA, Sukita, Mwananchi Gold, Meremeta, bomba la gesi na madude mengine nakula vichwa vyao na kuvichenjua.
Kabla ya kwenda kupata kanywaji, ngoja nitoe ujumbe wa ujumla. Abyssus, abyssus invocat au kuzimu huita kuzimu. Hivyo, wahusika, especially daktari Kanywaji, lazima wahusika walipie madhambi yao bila kujali kama wao ni makaburi au majipu. Mie nakwenda kuleta smelter ili kuokoa utajiri wa walevi.
Chanzo: Nipashe Jumamosi leo.
No comments:
Post a Comment