How the Berlin Conference Clung on Africa: What Africa Must Do
Tuesday, 12 November 2019
Happy Birthdate Mhe. Mkapa na Kuchapisha Kitabu cha Maisha Yako
Leo, Rais Mstaafu Mhe. Benjamin Mkapa ametimiza miaka 81. Si haba tunamshukuru Mungu kwa kumjalia afya na uhai. Muhimu, Mkapa ameadhimisha miaka yake 81 ya kuzaliwa kwa kuzidua kitabu cha maisha yake kiitwacho My Life My Purpose: Tanzanian President Remembers yaani, Lengo Langu Maisha Yangu: Rais wa Kitanzania Akumbuka. Kwa kuandika kitabu na kuanika historia yake Mhe Mkapa hakutenda haki bali kuchangia kwenye mchakato wa maendeleo ya taifa hasa kwa kukiri na kudurusu makosa yaliyofanyika chini ya utawala wake. Kwa wanaokumbuka, tulimshambulia Mkapa pale alipokosea tukanonekana wabaya. Sasa kwa vile Mhe Mkapa ameona makosa yake, kuyakiri ya kuyaongelea, ni wakati wa kumsamehe na kumpongeza akiwa ametoa somo la unyenyekevu na kuona mbali.
Hongera Mheshimiwa Mkapa kwa mchango wako adhimu kwa taifa lako. Hakika wewe ni shule kwa walio wengi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment