Aja Mali (28) (si jinale halisi) alibuni na kuingia ndoa iliyogeuka ndoana iliyomnasa vilivyo. Kijana huyu wa kihindi aliingia Marekani kwa mkataba wa kazi wa muda mfupi. Alifanya kazi vizuri. Hata hivyo, alijua fika. Muda aliokuwa amekubaliwa ungeisha, visa yake ya muda pia ingeisha. Hivyo, aliamua kufanya kitu ambacho kingemuwezesha kuendelea kuishi majuu asijue mwisho wake.
Kwa kutumia ujana na uzoefu wake, Aji, aliamua kumpenda mama mzee Linnie (60) (si jinale halisi) ikilinganishwa na umri wake. Fanya hesabu ujue tofauti ya kiumri. Kweli, shida haina adabu. Kwa vile Aja alidhamiria kufanikisha mpango wake wa kuendelea kuishi majuu, hakukata tamaa wala kufikiri mara mbili. Baada ya mapenzi kunoga japo kinafiki, Aja alifunga ndoa na Linnie mama tajiri mwenye nyumba na akiba si haba. Linnie aliongeza jina la Aja kwenye akaunti yake ya benki na kuifanya iwe ya pamoja.
Kama haitoshi,Aja alimuomba mkewe mama aka mshangazi amdhamini kuendelea kuishi majuu. Mke hakukataa. Wanguwangu, alianza utaratibu wa kumdhamini apate kibali cha kudumu cha kuishi majuu. Mwanzoni, mapenzi yalikuwa motomoto. Wawili walipenda. Hata hivyo, binti mtu, ndugu, na marafiki hata majirani walishuku ndoa hii ambayo kwao ilionekana ya ajabu. Wapo waliosema kuwa Aja alifuata utajiri wa Linnie. Pia, wapo waliosema wazi kuwa Linnie naye alitaka kutumia shida na uhitaji wa Aja kumnyonya kingono. Kimsingi, ndoa hii ilikuwa kama mchezo wa karata tatu. Kila mmoja, alikuwa na lake akitaka kumtumia mwenzake kiasi cha kutumiana. Na kweli, walitumiana kabla ya ukweli kufichuka na ndoa kuingia doa.
Hakupita muda, Aja alianza kuhamisha fedha Kwenda kwenye akaunti yake binafsi. Alianza kuongea kwenye simu kwa muda mrefu kwa kikwao tena akiwa nje ya chumba cha kulala. Hii ni baada ya Aja kujiridhisha kuwa mpango wa kumdhamini ulikuwa karibu kukamilika. Bila hili wala hili, hali hii ilimhuzunisha Linnie. Lakini alijipa moyo. Taratibu, ufa katika ndoa doa ulianza kupanuka. Aja alianza kukosa mawasiliano na ukaribu na Linnie. Linnie alianza kushuku kitu. Ila alijipa moyo kuwa mambo yangetengamaa asijue yasinge.
Bila simile wala woga, Aja alimkabili Linnie na kumueleza kuwa baada ya kukamilika udhamini wa kuishi majuu, angehama nyumbani kwa Linnie. Hili, kwa Linnie lilikuwa pigo lililomliza kiasi cha kusema lolote na liwe. Badala ya kumuomba asitekeleze azima yake, Linnie naye aliamua kujibu mapigo kivyake once and for all.
Bila kumstua Aja, Linnie alipanga mpango wa kumkomesha Aja. Baada ya kujiridhisha kuwa mpango wake usingefanikiwa kama alivyoupanga, Linnie aliamua kufanya vitu vyake. Wakati Linnie aliyekuwa ameishakata mawasiliano na binti yake kipenzi na wengine waliomzunguka kujua maji ndo yalikuwa yakimwagika mikononi mwake, aliamua liwalo na liwe na kweli lilikuwa. Hakumstua Aja wala kumuonyesha mabadiliko yoyote. Aliendelea kuwa mke hata kama ni wa kuigiza hasa ikizingatiwa wawili hawa hawakuwa na lolote waliofanana wala kufaana zaidi ya kutumiana.
Aja aliendelea kwenda kazini asubuhi na mapema na kurudi jioni kama kawaida. Huko nyuma, Linnie alirejesha mawasiliano na binti yake bila kumueleza sababu wala masahibu yake na kimwana wake. Alipiga konde moyo na kuamua kufanya kitu. Kwa vile mabadiliko ya Aja yalikuwa yamemletea ugonjwa wa kukosa usingizi hadi kwenda kwa daktari wake aliyemuandikia vidonge vya usingizi, aliamua kuvitumia zaidi ya alivyopaswa.
Aja aliporudi siku ya siku, alimuuliza Linnie juu ya udhamini. Linnie ambaye alishaukatiza wala hakumpasha kilichokuwa kikijiri. Kama kawaida ya watasha. Atakukumbatia kwa furaha halafu akudunge kisu mgongoni. Alimuandalia kila kitu mumewe. Kumbe kwenye chakula cha Aja Linnie ashajaza vidonge vya usingizi. Aja, bila ajizi, alikula msosi asijue ulikuwa ushadukuliwa.
Muda haukupita. Aja alijihisi usingizi. Alidhani ni uchovu wa kawaida. Taratibu alipanda kitandani mwao lau ajilaze kwa muda.
Linnie aliyekuwa akisubiri ndege anase mtegoni, alichukua mto na kumziba hewa Aja hadi akakata roho usingizini. Chapchap alimpigia simu bintiye na kumpa inshu nzima. Binti alikuja na kumsaidia mamaye kuingiza mwili kwenye gari na kwenda kuutupa kwenye sehemu ya kutupia mabaki kiwanda jirani. Hivyo, ndivyo ndoa ilivyogeuka ndoana na kumnasa aliyeitega. Yapo mengi. Nafasi haitoshi.

Chanzo: Mwananchi Jpili jana.
No comments:
Post a Comment