Kuna ndoa nyingi ambapo wanandoa wanaishi nyumba moja na kulala kitanda kimoja lakini hawaishi pamoja. Kimwili wako pamoja japo kiroho wako dunia tofauti. Wanaishi kwa pamoja ila si pamoja. Tuliwahi kugusia madhara ya mitandao na rununu. Mfano, unakuta mke au mume hana haki wala mamlaka ya kujua nywila ya simu ya mwenzake achia mbali kuweza kuishika au kuitumia. Kwanini? Kwa sababu kwenye simu husika kuna mambo ambayo mwenzi hapaswi kuyaona wala kuyajua.
Kama wanandoa, huwa tunashangaa inakuwaje? Binadamu yoyote timamu kiakili na kiumri ana siri moja inayokubalika kijamii. Nayo, ni kuficha uchi wake. Ni vichaa na watoto pekee wasioweza kufichi sehemu uhci wao. Waliobaki, hakuna kitu kigumu kufanya kama kutoka nje bila kujisitiri. Tena, husema uchi wa mnyama kwa vile ni wanyama tu wanaishi bila kuhitaji kujihifadhi. Hata nao ukiwaangalia kwa makini, hawako uchi.
Katika ndoa, hakupaswi kuwapo siri baina ya wanandoa. Kama wanaweza kuvuliana nguo, inakuwaje kwanini wasivuliane mioyo? Kama uko kwenye ndoa kama hii, ujue. Mnaishi nyumba moja, kulala kitanda kimoja, kumilki mali na watoto pamoja lakini hamko pamoja. Dhana ya kuishi pamoja inahusisha kuwa pamoja katika kila jambo liwe kubwa au dogo. Huwezi kumficha mwenzio au kuwa na siri zako ambazo hutaki mwenzio azijue mkawa pamoja. Hapana. Kwenye baadhi ya dini, wakati wa kula kiapo cha ndoa, wanandoa huambiwa kuwa wanaacha kuwa miili tofauti na kuungana na kuwa mwili mmoja. Ni mwili gani ambao kiungo chake kimoja kikiumia, sehemu nyingine hazihisi au kushiriki yale maumivu?
Ndoa siyo kama mashine ambayo inaweza kuwa na sehemu nyingi tofauti ambazo hazijuani wala kuwa na athari sawa. Magari ya siku hizi yana sensor kiasi cha kuwa mwili hai. Ndoa ni sawa na mwili uwe wa mtu, mnyama hata mti. Ukichuma jani kwenye mti, mwili mzima wa mti unahisi kitendo ulichofanya. Utafiti umeonyesha kuwa miti ina hisia. Kwa mujibu wa Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC, 2023) ulioripotiwa na Bethany Nichols uitwao Plants Have Feelings Too miti ina hisia. Ikiguswa inajua. Utafiti huu ulionyesha kuwa miti inapata hata msongo tokana na mazingira iliyomo. Mfano, miti aina ya Arabidopsis thaliana, ikiguswa inajua. Mfano, mwaka 2014, Heidi Appel na Reginald Cocroft wa Chuo Kikuu cha Missouri walichapisha ripoti ya kushangaza. Katika utafiti wao, kwa kutumia vifaa maalumu, walichezesha sauti ya viwavi wakila majani, upepo ukivuma, wadudu chavushi wakija kuchavu na mengine. Miti ilionyesha miitikio tofauti kulingana na sauti iliyochezwa.
Sasa tujiulize. Kama miti inaweza kuhisi, inakuwaje kwenye ndoa kuwa na siri binafsi kwenye mwili mmoja na sehemu mojawapo ya mwili isihisi au kujua?
Hivyo, tunapoongelea dhana ya kuishi pamoja na kuishi kwenye nyumba au kitanda kimoja, tuzingatie kuwa kuna uwezekano watu wawili wakalala kitanda kimoja lakini wakaishi kwenye dunia tofauti. Jambo hili hi hatari sana kwa wanandoa. Lina gharama kubwa. Maana, hakuna gharama na usumbufu kama kulinda na kutunza siri. Hii inapotekea, licha ya kumomonyoa upendo na kuzalisha mafarakano, huwaumiza wahusika kisaikolojia kiasi cha kukumbwa na hatari na magonjwa vitokanavyo na msongo wa mawazo ambao kwa sasa ni tishio la afya ya akili duniani.
Sasa, nini kifanyike? Mosi, wanandoa waanze kujichunguza kama wanaishi pamoja au wanaishi kwenye nyumba pamoja. Pili, wanandoa waanze kujifunza kuishi pamoja na si kuchangia nyumba na vitanda.
Tatu, wanaweza kuanza kwa majaribio. Matokeo watakayopata, yanaweza kuwapa la kuchagua ima kuendelea kuchangia nyumba na vitanda au kuanza kuishi pamoja.
Nne, kwa wale wanaochangia nyumba na vitanda wafahamu kuwa hizo siri wanazoficha na kulinda kwa gharama yoyote zitakuja kufichuka siku moja na wagundue kuwa walikuwa wakihadaa wakiamini wanawahadaa wengine. Hakuna kitu hatarishi na kigumu kama kuwa na kutunza siri. Mshaambwa. Duniani hakuna siri. Kama ipo, ipo kwa muda tu ila si milele. Kama chaji ya simu imeisha, mwaweza kuaziman? Kama hamuwezi, mnaishi tofauti.
Hilo ndilo somo la leo. Kwa wenye maoni mnaweza kutufikia kwa barua pepe nesaa1977@yahoo au nkwazigatsha@yahoo.com.
Chanzo: Mwananchi Leo Jpili.

No comments:
Post a Comment