Japo Fyatu Fala–––binafsi simjui –––ambaye wengi humuita mnene wa kiroho bila kumalizia, sawa na wengine wa aina yake, kuwa ni wa kujipa au kujipachika, amenifikirisha hata kunifyatua. Kwanza, nampongeza kwa ufyatu wake. Najaribu kumdurusu kwa sifa zake za utata alizoonyesha hivi karibuni. Huwa siandiki juu ya Mafyatu. Ila, leo, nimewiwa. Naufyatua mwiko niliojiwekea baada ya kusoma habari kuwa Fyatu tajwa amerejea Chandimu akitokea Chawalaji. Japo ni haki yake kuruka vyata, kwani katiba inaruhusu––– alinistua na kunitanza hadi nikafyatuka. Je, Fyatutajwa anakumbuka aliyosema aliposepa na sasa kujifyatua na kujirejesha baada ya kufyatuliwa na aliotoka kuwafyatua? Je, anajua kuwa na Mafyatu wana akili na kumbukumbu? Je, huu ni utoto au usanii kisiasa au? Nashindwa kujua. Hakuna kilichonigomba na kunifyatua kama sababu kinzani alizotoa na za kushangaza.
Sina ugomvi na wanasiasa wala watu wanaojitafutia riziki––––ila kwa kuwafanya wengine hamnazo–––hasa kwa kutumia kile ambacho marehemu Sam Sixx, microphone wa zamani wa njengo–––alichoita siasa za maji taka.
Wote tunayajua maji taka. Ni machafu. Yananuka. Pia, yanakera kiasi cha kutushughulisha kuyaondoa katika makazi yetu. Kama maji ni hivyo, siasa za maji taka, hali inakuwaje? Tunaweza kuzomea waitwao machawa lakini tukawashabikia maji taka ya kisiasa wanaohamahama kwa kutoa sababu zisizoingia kichwani.
Tujikumbushe. Fyatu tajwa alisepa miaka miwili iliyopoita. Kati ya mengi aliyosema ni kwamba Fyatuland hakukuwa na chata kama cha maulaji akikionya kutoshirikiana na wapingaji. Ajabu ya maajabu, ndani ya miaka miwili, ndoa imemshinda akaamua–––ila hata chembe ya aibu–––kuramba matapishi yake! Je, huy Fyatu anakumbuka aliyosema hapo juu na alichomaanisha au kulikuwa na namna?
Wapo wanaodai Fyatu tajwa alitumwa kufanya ‘kazi maalumu’–––ipi ambayo sasa ‘ameikamilisha’ na kurejea nyumbani! Ajabu. Hii ni kumpa mhusika sifa asizostahili. Kwa wanaojua namna baadhi ya wasanii walivyo nyemelezi hata matapeli, hakubaliani na hili. Kwani, linawanyima kuaminika hata kuheshimika sawa na mwingine kama yule aliyewahi kusema kuwa kazi yake ya uchunaji na utapeli ni bora kuliko urahis. Ajabu, alipopitishwa kwa rafu kugombea unene jimbo fulani, alisahau sijui alichosema na kupwakia matapishi yake huku akiimba kila sifa hata zisizokuwepo.
Kumjua Fyatu tajwa na wengine wa aina yake, turejee maneno yake hapo juu ukiyalinganisha na aliyosema ndoa ilipomshinda. Alinukuliwa akisema kuwa ameamua kuachana na chamaulaji kutokana na unyotoaji uliofanyika juzi! Lahaula! Je, kuanzia wakati huo–––kama kweli analiyachukia na kuyapinga–––alikuwa wapi? Alingoja nini au alikuwa akivuta kamba lau apate mradi? Je, ameamua kutumia unyotoaji tajwa kupata ujiko kama mwenzake ambaye–––alipopigwa chini–––kuushupalia? Je, kufyatuka na kusepa vinaleta suluhisho? Je, mauaji unyotoaji roho chanzo chake hakiwezi kuwa siasa za maji taka zilizojitenga na ukweli na kukumbatia uongo na uzushi? Ni jemedari gani hukimbia mapigano akidhani analeta suluhisho au ushindi? Natamani chata cha maulaji wafyatuke na kufichua walivyompokea, kumjua, kumchukulia, na kumtenza hadi ndoa ikamshinda akarejea alikokandia vibaya.
Hapa, kuna maswali muhimu. Je, Fyatu tajwa na wengine kama yeye wanafuata sera au vyeo na ulaji? Je, kwanini ameamua kuramba matapishi yake na kujigeuza maji taka baada ya
Kwa mtu wa kada ya Fyatu tajwa ya uchungaji kama siyo ‘uchunaji’, wengi walitegemea awe mkweli, mwenye maadili na si wa kusema hili leo na kesho, anajipiga mtama. Angeona lau hata aibu kuwa ni vibaya kwa Fyatu mzima tena ‘ wa God’ kuonekana kigeugeu, kizabazabina, na mtata kiasi cha kufanya siasa kuwa maji taka ambayo yakishachafuka, huwezi kuyarejesha kwenye usafi na usalama. Je, Fyatu tajwa, wenzake, waliompokea, na wamaomshabikia wanayajua haya au la? Je, anaweza kuaminika na kuheshimika tena ilhali akisema hili na kesho akasema kinyume chake kiasi cha kufanya wanaomsikiliza wasijue kati ya ukweli, uongo, na uzushi ni upi mbali na uchumia tumbo na usasi wa ngawira?
Japo si kosa kwa Chandimu kumpokea na kumrejesha kundini Fyatu tajwa, je, hii haionyeshi kuwa baadhi ya vyata ni kama maabara ambayo kazi yake ni kufanyiwa majaribio? Je wanajua maana ya kuwa hivyo? Japo, Fyatu huyu si wa kwanza wala mwisho kufanya siasa hizi zinaoanza kuzoeleka, kuna haja ya wapiga kura na wananchi kwa ujumla kuweka nukta na kukumbuka matendo na matamshi ya wote wanaotuaminisha kuwa wanatufaa wakati hawafai wala kujifaa.
Mwisho, kwa alichofyatua Fyatu, nashindwa kumuelewa wala kumpongeza zaidi ya kumpa pole. Maana, ana ndimi mbili. Isitoshe, kama ni upotezaji na unyotoaji roho, kwani, vilianza awamu jana? Je, ni unyotoaji roho gani ni muhimu kuliko mwingine tena chini ya chata lile lile? Je, Fyatu alikwenda kuwafyatua wenzake wakaishia kumfyatua? Maswali ni mengi kuliko majibu. Niwezacho kusema ni kutahadhari siasa za maji taka na wanasiasa maji taka.

Chanzo: Mwananchi, leo Jtano.
No comments:
Post a Comment