The Chant of Savant

Thursday 8 April 2010

Pole mama Salma Kikwete


Mpendwa mama Salma Kikwete,
Kwanza nakusalimu na kukutakia shughuli na afya nje. Pili nakupa pole kwa yaliyokukuta-yaani msafara wako kunusurika kugongwa na lori lililodhaniwa kuwa lilikuwa likiwakimbia polisi kutokana na kubeba bidhaa za magendo. Hii ilitokea kule Musoma ulipokwenda kuwapigia magoti wakurya waache kuchinjana. Ila hapa kuna kitu kimoja. Hawa watu hawachinjani kutokana na roho mbaya au imani za ushirikina bali ukapa. Bila kubadili aina ya uchumi wao watauana sana hata uwapigie magoti hadi yachubuke hawataacha.

Kusema ukweli nilipata taarifa za kunusurika kwako katika ajali hii kwa mstuko mkubwa. Nilijiuliza. “Sasa tunakwenda wapi kama hata msafara wa mke wa mwenye nchi unavamiwa na dudu kubwa kama lile?” Hata hivyo, sikushangaa. Huu ndiyo ukweli wa maisha wanayoishi watu tuliowaahidi kuwapeleka Kanani wakajikuta wakizidi kutokomea Misri. Maana wamepigika kweli kweli ingawa sisi tunaotanua hatutaki kukubaliana na hili. Maana kwao riziki ni lazima mtu avunje sheria. Huenda hii inatokana na wakubwa kujisahau na kuhomola na kutumia vibaya kama tulivyoshuhudia juzi kwenye sakata la Kagoda na Richmond ambapo wakubwa wasio na roho na wenye roho mbaya na uchu wa fisi waliamua kuua kashfa hizi ili kuwanusuru wenzao.

Sikupenda kuandika waraka huu. Nimelazimika kutokana na mapenzi yangu kwako na taifa hasa shughuli unazofanya ingawa haziwafurahishi wengine. Maana kuna wanaosema eti umeaanza kumpigia kampeni mumeo hata kabla ya kipenga cha kufanya hivyo kupulizwa jambao ambalo napinga. Watu hawa wasio na adabu wanahoji ni kwanini sasa wewe, mumeo hata mwanao muonekane mikoani mkitoa misaada na nasaha wakati miaka minne iliyopita hamkufanya hivyo? Wengine wanasema eti ni rushwa! Tangu lini wazito kama nyinyi mkatoa rushwa? Hayo ni maswali yao na roho mbaya zao. Mie huwa nawambia kuwa mbwa wa mfalme naye siku zote ni mfalme wa mbwa wote.

Wapo wanaohoji bajeti inapotoka pesa ya kulipia ziara zako wanazosema zinahusisha misururu mirefu ya mashangingi. Eti wanasema kufanya hivyo ni kuchafua mazingira na kuwaongezea mzigo walipa kodi na kujipachika madaraka usiyo kuwa nayo kikatiba. Wengine wanasema eti ni matumizi mabaya ya ofisi ya mumeo eti kwa vile walimchagua yeye na kumwapisha yeye peke yake! Hawa wanakosa hoja na hawana adabu. Hawajui wewe ni mke wa rais hivyo una chembechembe za urais? Wengine wanasema eti unatumia hata ndege ya mumeo iliyonunuliwa kwa mabilioni ya Mkapa sambamba na rada wanayosema ni feki. Mie huko siko. Wapuuzi hawa wanataka utumie lini iwapo kutesa ni kwa zamu?

Mama, kusema ukweli hawa wanaokuandama wananiudhi kiasi cha kutamani kumtoa mtu roho kama siyo kugopa kunyea debe. Maana wanahoji vitu visivyo na maana. Eti wanauliza ni kwanini ulianzisha NGO yaWAMA (Wanawake na Maendeleo) baada ya mumeo kuwa rais na si kabla? Hawajui kama ungeianzisha kabla isingepata wafadhili?

Hawa naona hawana akili. Hivi hawaoni WAMA ilivyoleta maendeleo kwa wanawake wa Tanzania? Hawajui kuwa kulala watano kwenye kitanda kimoja wakati wa kujifungua pale Amana, Mwananyamala na Temeke ni historia? Hawajui hata wizi na kubadilishiwa watoto kumepungua ukiachia mbali uhaba wa madawa kutokana na juhudi zako?

Eti wanahoji ni kwanini wafadhili wako na matumizi na mapato ya ofisi yako hayafanyiwi ukaguzi wa mahesabu na taarifa kuwekwa wazi! Wanasema eti wengi wanaoifadhili NGO yako walikuwa wafadhili wa EOTF ya mtangulizi wako Anna Mkapa ambaye baada ya mumewe kutokwa na madaraka hawataki kumuona achia mbali kumchangia. Eti wanasema wanachangia madaraka si wewe! Hivi hawa wana akili kweli? Inakuwaje hawakuamini wewe mke wa kiongozi wao? Isitoshe biashara zako zinawahusu nini kama si wivu wa kipuuzi?

Wengine eti wanauliza ni kwanini kila shughuli ya WAMA inasimamiwa nawe na si wasaidizi wako? Kwani umewambia kuwa umechoka kiasi cha kuhitaji mtu mwingine kusimamia shughuli za asasi? Isitoshe wanajua siri ya kuanzisha NGO hii. Si nao waanzishe zao ingawa hazitapata wafadhili kutokana na kutokuwa na waume wenye madaraka.

Katika utafiti na uzoefu wangu nimegundua kuwa wabongo wamefyatuka si kawaida. Wanaweza kuhoji lolote. Siyo kama wale wa zamani. Halafu wanaonekana kuwa na hasira si kawaida. Ni wanoko hakuna mfano. Una habari kuwa njaa ndiyo imewafanya wawe hivi? Kwa taarifa yako, taarifa za hivi karibuni zilizotolewa na serikali ya mumeo ni kwamba takribani nusu yao wanakula mara moja kwa siku kama komba huku serikali yao ikitanua na kutumia mara mbili ya kipato chake. Kwa vile wanaona wewe uko karibu na rais wanadhani misafara yako ni sehemu ya haya matumizi wakati si kweli.

Eti wanasema kuwa mke wa baba wa taifa Mama Maria Nyerere hakuwa na NGO. Ni kweli. Lakini wakumbuke kitu kimoja. Zama hizi si zile za Nyerere ambapo kitu hiki ilikuwa sawa na tembo kupita kwenye tundu la sindano. Inabidi tuwambie kitu kimoja. Mambo yamebadilika sana. Na kwa sasa hatujengi tena siasa ya ujamaa na kujitegemea bali soko huria la kila kitu kuanzia haki hata siasa. Na isitoshe wakati ule ufisi na ufisadi ulipigwa vita vilivyo badala ya maneno matamu na dili za nyuma ya pazia. Kwa sasa ni ufisadi ufisadi mtindo mmoja. Ndiyo maana watu wana ufisadi wa kuhoji kazi zako tukufu. Isitoshe Nyerere alikuwa akipoteza muda mwingi kwenye maadili badala ya madili kama sasa. Bila dili watu hawawezi kuendelea.

Pia wanapaswa kufahamu kuwa wakati wa Nyerere wanawake hawakuwa na matatizo mengi kama sasa kutokana na mambo kubadilika hasa mafisadi kuliibia taifa. Hivyo, kwa hali hii ambapo ulaji ni lazima, lazima kuwepo na NGO ya ikulu kuwasemea akina mama kutokana na wizara yao kushindwa kutokana na kushikiliwa na wanasiasa.

Wanaongeza kuwa watoto wa Nyerere hawakuwa makada na wakuu chamani. Jamani zama hizi zimepita. Watoto wa Nyerere hawakuwa wamesoma siasa kama wa sasa. Na isitoshe Nyerere alikuwa mkali sana. Hayo tuyaache.

Mama naomba niishie hapa. Naogopa kukuchosha kutokana na kuwa na kibarua kizima cha kuizunguka nchi na dunia. Nakutakia afya njema na mafanikio katika shughuli zako za ujenzi wa taifa lenu. Pia hawa wanaotishia misafara yenu wanapaswa kutoka usingizini. Kwanini wasiende Kanani badala ya kuishi kwa magendo na matumaini? Kama wale waheshimiwa wa Kagoda na Richmond, chonde chonde mama waombee msamaha hawa waliotaka kukugonga. Maana si kosa lao bali maisha. Kuwakamata ni kuukwepa ukweli. Ni hatari kukwepa au kushindana na ukweli. Nao wana roho na matumbo kama sisi. Naomba niishie hapa.
Chanzo: MwanaHALISI Aprili 8, 2010.

7 comments:

Anonymous said...

Du! Umemsiliba huyu pimbi. Ila mtu akisoma kwa papara anaweza kudhani unampamba kumbe unambomoa!
Sanaa nimekubali ipo.
Big up sana mwanangu maana huyu pimbi ni mwizi sawa na sura mbaya Anna Mkapa.
Hoja zako ni za msingi. KWanini kuanzisha NGO baada ya mumewe kupata urais?
Mwita

Anonymous said...

Si na wewe uanzishe yako, mbona NGO zimejaa kibao na hata kazi zao hazionekani, mlitaka alipoacha ualimu kwa kuwa mke wa rais avae hijabu na kujifungia ndani? Je ni yeye tu Africa nzima mke wa rais mwenye NGO? Nendeni zenu huko ni mfumo dume ndio unaowasumbua, mlitaka akae ikulu anapiga deki na kuosha masufuria?

Si kila kiandikwacho kina mantiki, umeuliza utumbo mtupu wala haunogi, na huyo juha kumuita mwanadamu mwenzie pimbi wala sishangai, maana hata huko atokako kumelaaniwa na Muumba kama mtu aweza chinja watoto wadogo wasio na hatia ni binadamu kweli hao au masalia ya binadamu?

Mwanamke mpinga mfumo dume

Anonymous said...

Kumbe imewachoma! Wewe unayejiita mwanamke mpinga mfumo dume kampinge baba yako. Kamwambie abebe mimba ndipo ufurahi. Pimbi wenu hata angepiga deki ikulu sawa. Kwani kama angetaka urais angegombea siyo kuishi kama kupe mgongoni mwa mumewe. Mbona Maria Nyerere hakuwa na NGO na anaheshimika kuliko hawa malaya wawili tajwa hapo juu?
Mwita

Anonymous said...

Kaka Mwita umenena. Hili shankupe na nung'aembe linalojifanya kutetea wanawake ni fisadi. Linajipendekeza kwa jambazi la kike Salma ili iweje? Nina wasi wasi hili jimama ni chaga au ni Anna Mkapa mwenyewe. Umefika wakati kuwambia wake wa marais kuacha kuishi kama kupe. Wanafilisi taifa letu kupe hawa.Ila ipo siku ukweli utadhihiri na yatanyea debe.Tumeishaanza kuamka. Kwanini familia ya Kikwete kila mahali? Ukienda ikulu Jakaya, NGO, Salma, UVCCM, Ridhiwan na msenge wake JAnuari Makamba na shoga Lawrence Masha. Kuna nini hapa kama si ufisadi mtupu?
Nyambane

Anonymous said...

Nyie ndio mafisadi mliozoea kutoa roho za watu huko kwenu, ndio maana badala ya kutoa hoja mnatoa matusi.

Mtu yeyote mwenye kukimbila kutoa matusi ni kwamba ameishiwa tena amefilisika kimawazo na kiakili. Kwani anakuwa hana jipya la kusema basi anabaki na matusi tu yasiyo nakichwa wala miguu. Ni sehemu gani ya katiba ya nchi inakataza mtu asishiriki shughuli za siasa kisa mumewe au mkewe ni Rais?

Nendeni shule mkatoe tongo tongo za macho, someni mambo yananyotokea duniani kwenye mtandao ili mpanue mawazo yenu mgando. Hata huko duniani wanakoishi watu, na sio kujaribu kuishi, wake za marais wanajishughulisha na shughuli za jamii. Mfano mke wa Obama. Na mfano mwingine ni Hillary Clinton alikuwa akifanya kazi mbali mbali za jamii kabla hajaingia kwenye siasa mwenyewe. Ajabu nyie sijui mnaishi karne gani, kwani ukienda kuchukua fomu za uongozi utanyimwa, kazi uvivu, matusi na majungu, hamna lolote jipya! Ushamba tu unawasumbua, hii yote ni shauri ya kuishi maporini mkija mjini mwashangaa!

Anonymous said...

We juha sina mfano. Michelle Obama anafanya shughuli gani na ana NGO gani zaidi ya kufanya shughuli za White House. Nitajie NGO ya Hilary Clinton nitakutafutia mume uishi maisha ya heshima. Unahukumu wakurya wote. Huu ni ushahidi kuwa huna akili zaidi ya msongo wa mawazo kutokana na kuwa nungaembe na shankupe. Utajisikiaje kama nitasema wachaga wote mnatembea na baba zenu na kaka zenu bila kubakiza wajomba?
Salma na Anna watabaki kwenye historia kuwa ni majizi yanayotumia ikulu. Kama shughuli za jamii zingekuwa deal basi kazi hiyo wangeanzisha Mama Maria Nyerere na Sitti Mwinyi. Acha ubabaishaji shangingi wee. Tulia upata mume uishi maisha ya staha malaya wewe.

Ndugu Nkwazi N Mhango said...

Wapendwa wasomaji wangu,
Nawashukuru kutembelea blogu hii ingawa naumia kuona mnavyovuana nguo kiasi cha kupotosha hoja. Nawashaurini mvumiliane kwenye tofauti zenu za misimamo na mawazo.
Nachelea kusema kuwa matusi hayajengi ukiachia mbali kupotosha hoja. Pia nakubaliana na tofauti zenu ingawa natofautiana na jinsi mnavyotetea hoja zenu.
Kimsingi dhana nzima ya magazeti haya meme ni kujenga na kuleta maelewano.
Kila la heri,
Nkwazi