How the Berlin Conference Clung on Africa: What Africa Must Do

How the Berlin Conference Clung on Africa: What Africa Must Do

Friday, 20 February 2015

Bila kujikomba kwa CCM, Kikwete na ukoo wake baadhi ya mlioko nje hamuwezi kuishi?

Kuna tabia ya ajabu imejitokeza ambapo baadhi ya watanzania wanaoishi nje ya nchi hujikomba kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kama njia ya kurejerea nyumbani. Majiji ya Washington, New York na London yanaongoza kwa wasanii kujifanya wana uchungu na CCM. Jamani kama mmeshindwa si mrejee huko mkawa wakereketwa tu? Watu badala ya kujisomea na kutafuta maisha kwa njia halali wanaingia usanii kiasi cha kutia kinyaa. Pichani hapo juu mtoto wa rais Jakaya Kikwete, Ridhiwani au rais wa nyuma ya pazia anawasili New York tayari kwa maadhimisho ya miaka 38 ya kuzaliwa CCM. Hawa wanaomwambudia Kikwete na ukoo wake makaratasi yao yamekaa sawa? Kama yamekaa sawa, wamejiandaa vya kutosha kuishi maisha ya mpambano huku ugenini? Wamejiongezea maarifa angalau wawe na cha kurejea nacho nyumbani kama wataamua? Au wameamua usanii na kujikomba kama mtaji? Mimi hakika sielewi.

4 comments:

Anonymous said...

Mwalimu hapo kila kitu kinajieleza tena kaa nao mbali hawa watu wakitumwa wakuzuru watafanya hivyo kumbuka uteuzi wa mwambata wa ubalozi na mkuu wa wilaya mmoja hivi karibuni vyote vimeendana na harufu na matendo ya kumwaga damu ndiyo sifa ya kupata cheo.

Kimsingi watu wanahangaikia kupata vyeo na fedha, wakati kimsingi kinachotakiwa katika nchi hoi hae kama yetu ni viongozi bora na wajibikaji kihalali.

Sivyo hivi sasa tunaishi kwa mipango ya muda mfupi ya kiahalifu halafu yakitokea makundi madogo ya kiahalifu tunashangaa, nchi zote za Afrika ziliingia katika matatizo ya vurugu na vita kwa sababu ya haya tunayoshabikia sisi mbumbumbu(Wahalifu) na kuona kuwa tunapata majibu ya matatizo yetu. Kumbe tunachochoe vita vya vyenyewe kwa wenyewe kwa matendo yetu.

Wahalifu wakuu hivi sasa ni wala rushwa kubwa hivyo tunapoendelea kufanya masihara basi jipu linatatoa usahaa!

Ndugu Nkwazi N Mhango said...

Anon,
Japo usemayo ni kweli, hakuna haja ya kuwaogopa ngurumbili ambao hata wakiua nao wanakufa. Hatuwezi kukaa pembeni na kuacha wahalifu wachache waendelee kutuelekeza kuzimu. Najua madhara ya kusema ukweli. Hata hivyio, lazima ukweli usememwe despite what. Kama hawa wanaojifanya wanaipenda CCM basi warejee Tanzania waijenge badala ya kudanganya wanaipenda wakati wanatafuta gea ya kurejerea baada ya mambo kuwashinda ughaibuni. Mngekuwa mnaipenda CCM mngekimbia utawala wake? I don't pay a hoot. Nitasema na nina hakika hakuna awezaye kunidhuduru. Siasa za kijambazi zimepitwa na wakati. Lazima tuwaambie hata kama hawapendi kuwa hawana sera bali njaa na usanii. Huku ughaibuni kuna vyuo bwerere. Nendeni mkasome na kujikomboa badala ya kuendekeza kujikomba kwa vinyamkera na mafisadi.

MAWALA WA SEMBE HAO KWANI HUTUJUI MTU WA MAANA MWENYE MAKARASI YAKO UGHAUBUNI UTAANGALIKA NA RIDHIWANI