WASIFU WA MAREHEMU
Dk. Masaburi alizaliwa Machi 24 mwaka 1960 na alisoma Shule ya Msingi Nseke iliyopo Serengeti na mwaka 1978 alijiunga na Sekondari ya Wavulana ya Tabora na kuhitimu mwaka 1981.
Mwaka 1982 Dk. Masaburi alijiunga na Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) na kuhitimu mwaka 1985 na kupata cheti cha ufundi wa magari.
Mwaka 1985-1990 alichukua mafunzo ya ugavi na kupata Shahada ya Ununuzi na Ugavi kutoka Bodi ya Ugavi wakati huohuo akichukua mafunzo ya ununuzi na ugavi nchini Uingereza Chuo cha Chartered Institute of Purchasing and Supply ambapo alitunikiwa cheti cha Diploma ya juu ya Ununuzi na Ughavi mwaka 1988.
No comments:
Post a Comment