Heko Rais Magufuli

Saturday, 26 May 2018

Je Mengi anasaidia wengine huku akidhulumu wengine?


                Reginald Abraham Mengi, wa mizania ya kitanzania na kiafrika, ni tajiri. Hata hivyo, utajiri wake unaweza kutia shaka. Je inakuwaje tajiri kama Mengi anayeonekana akisaidia wengine kuruhusu dhuluma iendelee kwenye makampuni yake? Hii inajenga hisia kama kweli utajiri wa Mengi siyo kama ule wa tapeli  Abbas Gulamali aliyesifika kwa kutoa misaada na kudhamini vilabu vya mpira wakati wafanyakazi wake walikuwa wakifanya kazi bila kulipwa kwa muda mrefu.
               Baada ya kujaribu kuwasiliana na Mengi bila mafanikio, nimeamua kuwa naweka madai yangu dhidi ya magazeti ya Nipashe na the Guardian ambayo yamenidhulumu zaidi ya shilingi 8,000,000 bila kuhusisha interests kama nitaamua kushitaki. Bado sijaamini kama kweli Mengi, kama kweli ni tajiri, kama anavyojionyesha, anaweza kushindwa kulipa fedha kidogo kama hiyo. Dhuluma yangu imewezeshwa na wahariri wangu Edmund Msangi na Gaudensia Mngumi ambao wameamua kujenga chuki ili kupata namna ya kunidhulumu. Naamini kupitia wavuti huu ipo siku Mengi atapata taarifa za dhuluma hii ambayo si ya kwanza wala ya mwisho tokana na kupata taarifa toka kwa wahanga wengine ambao hawana namna ya kukabiliana nayo. Mie nitatumia wavuti wangu kupambana na dhuluma na ufisadi huu tena vinavyofanywa na watu wanaojidai ni matajiri.

No comments: