How the Berlin Conference Clung on Africa: What Africa Must Do

How the Berlin Conference Clung on Africa: What Africa Must Do

Tuesday, 4 June 2019

Picha ya wiki: Rais anapobeba kapu kwenda kununua samaki

Image result for photos of magufuli shopping at the fish market plastic bags

Tofauti na watanzania walivyozoea kuona rais akiwa chini ya ulinzi mkali, rais John Pombe Magufuli ni rais anayewza kuchomoka ikulu na kwenda kujichanganya na wale anaowaongoza. Katika picha hii aliukaribisha mwezi wa Juni kwa kwenda kwenye soko la Samaki Ferry kununua samaki tena akitumia kapu kama ishara ya kupambana na uchafuzi wa mazingira utokanao na matumizi ya plastiki. Alipoingia madarakani Magufuli aliwaacha hoi wengi ndani na nje ya nchi kwa kushikiri usafishaji wa mitaa kabla kutua jijini Mwanza aliposhuka kwa mamantilie na kununua vinywaji na kugawana na wananchi. Mtoto huyu wa mkulima, hakika hajasahau alikotoka. Hili ni somo kwa wananchi kuwa cheo ni dhamana na lazima kiongozi afanane na wale anaowaongoza. Hapo juu, hii ndiyo picha yetu ya wiki. Hongera rais Magufuli kwa kuongoza kwa vitendo.

No comments: