How the Berlin Conference Clung on Africa: What Africa Must Do

How the Berlin Conference Clung on Africa: What Africa Must Do

Tuesday, 12 December 2023

Maza, Kaa Chonjo kama Kuna Zengwe Kufyatuliwa Chongo-loh!

 

Maza Kipenzi na Kipendwa japo wapo wanaoponda,

Naomba nichonge nawe kiduchu tena kwa utuo bila kufyatua wala kufyatuka. Katibu mkuu mjiuzulu wa chata chako, Dan Chongo-loh–––uliyemfyatua usijue kama waweza kuiwa ntego wa warume kama alivyowahi kuonya mama Gettie Monge-la­­­­––––aliingia na kuondoka ghafla bin vu. Kuna tetesi kuwa Chongo-loh alichafuka baada ya mambo yake binafsi kufichuliwa mitandaoni. Ukiangalia kashfa iliyomfyatua Chongo-loh ambayo ni mambo ya kibinafsi ambayo wengi wanafanya ukalinganisha na watuhumiwa wa kufyatua mabilioni, huoni mantiki. Je uchafu wa Chongo-loh unawaathiri vipi mafyatu? Anasikitisha alivyoingizwa na kuchomolewa. Nadhani Gettie atakuwa anashangaa ulivyomfyatua haraka bibie mwenzako haraka wakati warume wakiendelea kufyatua na kutesa. Je is it the nature of things au ni lile bifu na Bashiti ambaye anaonekana kushika kani asijue itamshika kitambo? Wapo wapi akina jiwe hata yule Sam wa kwenye Bibi lia?

 Je nani anamfyatua nani akifyatua mazingira ya kufyatua tokana na ufyatuzi huu? Nani anamfyatua nani kati ya fyatu alyekufyatua hadi ukamfyatua Chongo-loh? Je huu ni mchongo wa chongo kibashit aonaye maulaji bila kujikumbusha mafyatu kama Katelefoni Hanga, Joni Okelllo, Eddy Sokoi4, Horaace Koli-imba (waliiohagiwa, kusokoinwa, na kukolimbwa na wapambe nuksi ili wasiharibu kitumbua chao), Eddy Ewassa na wengine wengi waliofyatuliwa kwa sababu waliwafyatua wenzao ili wafyatue ulaji.

Laiti shehe Obeid Karumekenge angefufuka na kukupa somo. Laiti Sayyidna  Abuba-kar as-Siddiqq au umar ibn al-Khattabbb wangefufuka na kukupa somo juu ya fitna na tamaa. Laiti Sayydina Muhamaddd  bin Abdullahh ibn Abd al-Muttalibbb ibn Hashimmm ibn Abd Maaanāf angetunuku na kukupa somo hili adhimu.      

Simjui Chongo-loh. Sina uhusiano wala shida ya kumtetea. Wala mie si chawa bali fyatu wa kawaida aliyemepiga vitabu hadi mlango wenye maandishi yasomekayo: no more clases and education for you. Najua unajua. Ninaishi Kanada, kaya ya neema na shibe. Isitoshe, mie ni mbukuzi wa kiwango cha Doktari original siyo feki wala wa kupewa. Hivyo, unaweza kuona. Sina njaa japo, kama fyatu wengine ukiwemo wewe, siwezi kusema sina shida. Nani anataka kumkufuru Allah Subhanahu Wa ta’ala (SWT)?

Kama magwiji fyatu kama Nebkadineza, Samson, Genghis Khan, Mirambo, Mutwa Mkwawa, Nyungu ya Mawe na wengine waliofyatuka na kufyatua walifyatuliwa, sie ni nani? Isaac Malyamungu alimponza Idi Amin. Heinrich Himmler alimponza Adolf Hitler wa Ujerumani kabla ya kugawanywa na baadaye kuunganishwa. Nuon Chea alimponza Pol Pot wa Kambodia. Galeazzo Ciano alimponza Benito Mussolini wa Utaliano. Juan Manuel Guillermo Contreras Sepúlveda alimponza Augusto Pinochet wa Chile, Abdallah Sanussi alimponza Muamar Gaddafi, Izzat Ibrahim al-Douri alimponza kakayo Saddam Hussein. Georgy Malenkov alimponza Nikita Khrushchev kule Urusi. 

Mwisho, nyoka alimponza Eva––––kama kweli ni ukweli–––ambaye naye alimponza Adam japo kama siyo rongorongo za madume na mfumo dume. Orodha ni ndefu. Sitaki nikuchoshe. Ni fyatu wengi wanene safi wamepotezwa au niseme: wamefyatuliwa na wapambe wao wawaimbiao sifa na pumbazo ili kuwapumbaza na kuwafyatua kwa maslahi binafsi ya kesho.

            Ukivaa viatu vya wenzako, utagundua kuwa wengi walioapishwa siyo wale wanaojitiatia. Likifyatuka, huwaoni. Nani alidhani Pita angemkana mwana wa Adamu au wayahudi wangemsulubu Mwana wa Maria? Nani alidhani kuwa Jiwe angesahaulika baada ya wale aliowatengeneza kufanya kila jitihada asahaulike? Nani alidhani Shaytan angelimuasi Allah pamoja na kumpa kila alichotaka hata bila kuomba wala kutamka? Fyatu ngurumbili hatosheki. Ukidhani utani, angalia walio karibu yako kuanzia baba, ndugu, marafiki, na hawa wanasiasia wachumia tumbo. Sidhani mafyatu kama Bashit, Januwari Ma-rope mwana wa Mgoshi, Mapepe Ninae mwana wa Moze, Riz Njaa Kaya na wengine wanaweza kukuvusha.

            Kwanza, wanajua malengo na mipango yako ya mbili zero 25. Unadhani wanafurahia wakati, kama warume, wanajiona wanafaa kuliko wewe maza? Wahenga walisema, siyo kila ving’aravyo ni dhahabu. Tia akili umbuje angu. Acha niongee kisambachi nikichanganya na Kinyachi.

Maza kaongee na faza murumeo. Huenda, anaweza kukuokoa na hiki kitanzi na mtego ulioingizwa na ukajiingiza. Je unayakumbuka maneno fyatu ya maza Gettie Monge-la? Nasisitizia kifyatufyatu. Achana na mafyatu hawa wa kirume. Watakufyatua na kukurostisha. Chongo-loh, alikuwa mikono safi asiye na kabobo wala ngebe kama huyu fyatu unayamdekeza hata kama alikupendekeza uteuliwe mgombezi mwenzi.

Kabla hujafyatua milomo na kunienga kama hamanazo, jiulize na jipime. Wewe na Jiwe nani fyatu mchimvi anayeweza kumfyatua hata chawa na kiroboto aliowaumba mwenyewe? Je alipomfyatua huyu kidhabi, unadhani alikuwa amefyatua hadi kupagawa? Naomba ufyatue nukta hapo. Tia akilini. Yesu bin Mariam ambaye ni fyatu mwenzangu alisema kuwa siyo kila ajae akisema Bwana Bwana, atauona ufalme wa mbinguni. Siyo wote wanokuchekea wancheka kwa furaha. Wengi roho zawafyatua na kuwanyotoa kwanini wewe si wao.

Nisisitize, sina uhusiano wala usuhuba na Chongo-loh wala wewe. Andika na pigia msatari au weka nyota au mkazo maneno haya kwenye kumbukumbu zako. Siku ya siku ikifika utanikumbuka na kutamani ungewasiliana nami kabla ya hayo yatakayokufanya ukumbuke unabii huu fyatu wa mafyatu.

            Hii ni lecture au research paper?!!

Chanzo: Mwananchi, kesho.

 

No comments: