Kwa vile sifa zinatoka kila kona kuwa amefanya makuu
na makubwa mengi hata kama hajawahi kushika chaki wala kufundisha hata
chekechea, maza sasa ni prof emeritus. Huu ndiyo urathi wa jiwe. Isitoshe, si
vibaya kumtia moyo kipenzi maza yetu. Naona yule anasonya cheo gani hiki
ambacho siyo udoktari wa heshima. Wajua
maana yake? Ni prof mstaafu. Alifundisha na kustaafu Chuo gani? tafadhalli
sana. Usiniulize. Mimi ni kama fyatu Paulo. Fuata nikwambiacho siyo nifanyacho
fyatu wangu. Mafyatu wameniomba nimuombe maza akubali kupewa hadhi hii.
Usiniulize toka Chuo gani? Kwani, lazima kiwe chuo? Nani anashindwa kufyatua
Chuo feki na kufyatua vitu kama hivi? Wanaotaka kunifyatua kwa kuja na ubunifu
huu, wajiulize. Mbona mafyatu wengine wanapomtunuku hamuohoji bali kuimba kwaya
doktari doktari utadhani vyura na chawa? Sasa, mtake msitake, mtaanza kuimba
prof emeritus hata kama wengine hamuwezi kuitamka.
Raha jipe mwenyewe au mpeane. Kuna kosa gani, mfano, kumpa dingi kipenzi cha maza uprofesa ili afanane ni waivu wake? Isingekuwa katiba yetu kutoliona hili, ningependa bwana nkubwa aitwe rahish kwa vile bi nkubwa ni rahis. Wakwe na watoto wao ningependa waitwe marahishi ili kuweka ulali katika ulaji wa kifamilia.
Ikiwapendeza, chata lake, familia, mawazi-ri, marafiki, na hata mafyatu wapewe udoktari wa heshima. Kwani, lazima kuunga mkono juhudi bila kuwa chawa wala kunguni. Si inapendeza kwa kila mnene kuwa na cheo na shahada nene? Mbali na ‘kuunga mkono jihitihada’, tunataka kuwakomesha mawazi-ri wanaotunyanyasa na kutokoga kwa udoktari tena uchwara na siyo kama huu mtukufu wa kupewa na kusifiwa kama njia ya kuunga mkoni jitihada. Kama wengine waliitwa Mungu bila kuchukia wala kuwaonya waliofanya hivyo, hamuoni kuwa hii inapendeza na kuvutia?
Kwa sababu kufisia nayo ni sera, kwanini mafyatu wasiiunge mkono? Kama hata chawa wanaongea na kuimba sifa, sisi ni nani? Ni mwanakwaya gani aliwahi kuuliza mantiki ya wimbo auimbao? Fuata nyuki ule asali. Kama alivyovunga fyatu mgoshi Yusif Makambale kuwa mama amewapa asali warambe, nani hataki kuramba asali hata kama asali yenyewe mafyatu hatuioni? Sie tunakula ima kwa imani au macho wakati akina mgoshi Makambale wakiramba asali kupitia vitegemezi vyao vilivyopewa ulaji mnene na mnono katika mfumo wa kifamilia zenye majina manene.
Mafyatu tunaanza na prof emeritus. Kama haitatosha, kama yule profedheha Kabundi wa magamba allivyomuita mwendaze aliiyemuumba maza Mungu, tutamuita muungu mwenyepenzi na mwenzi kipenzi cha mafyatu hata kama hatupendwi. Katika nchezo wa karata tatu, lazima ufyatuke na kufyatua ili kufyatua ufyatue ulaji. Japo wengi watashangaa kwanini mafyatu wazima tena wasomi tunafyatua kitu siyo kituko kama hiki. Kwani hao waliomwita mwendazake ni watoto au maamuma?
Kwa taarifa yenu, kuna aina mbili za uumbaji. Upo ule wa mwenyewe Subhana na ule wa ngurumbili ambao kwa kisambaa huitwa political creation or cloning. Hapa, mafyatu tegemezi wasioweza kujisimamia, hujikomba ili kuumbwa au kuibuliwa na wenye maulaji ili wapate tonge na kujaza mifuko yao isiyoshiba wala kushukuru. Hii haijalishi mhusika ni msomi, mtu mzima, mwanaume au mwanamke. Ni tabia binafsi ya fyatu kutojiamini au kuishia mbinu na ubunifu wa kula bata. Huu ni uchangudoa wa kisiasa unaoonekana kuanza kukubalika hata kushabikiwa. Je nini madhara yake? Kupata wanene wasio na sifa na wanaotumikia matumbo yao badala ya mafyatu. Pia, inawezekana wahusika wakajikuta uso kwa uso na popobawa au poposhungi.
Sisi tumeamua kumpa uprof emeritus si kwa sababu ya kujikomba au kutafuta ulaji. La hasha. Tunafanya hivyo ili kutimiza mila. Naona yule anacheka. Sisi siyo wachumia tumbo. Ni wanafalsafa ambao ukiwaelewa, utajua nini tunamaanisha. Utakubali kuwa tunachomaanisha ni tofauti kabisa kwa sababu hatuwezi kuumbwa wala kupewa ulaji. Nani awape fyatu ulaji wamfyatue? You know what I mean. Lengo letu ni kumsuta, sorry, kumvuta ili aende chuo akajikunje na kupewa hii kitu ambacho tunamzawadia kama motisha. Unanifahamu?
Turejee kwa wanaojikomba aka machawa, tokana na uchangu wa kisiasa, wahusika wanaweza kutumiwa hata na maadui toka ughaibuni kutufanyia kitu kibaya kama vile kutununua, kutugeuza watu, mbali na kutubinafsisha sisi na mali zetu kuanzia bandari hadi washirika wetu wa bedroom. Are you there? Patamu hapo. Kabla ya kubinafsisha mshirika wangu wa bedroom, nitahanikiza waanze na wao. Kwa warume, mtajijuu. Kwa manzi, haina shobo. Muulize bi nkubwa anavyoshare na wenzake. Sorry, don’t think I’m a party pooper. Nalonga kisambaa japo mjue fyatu ni doktari tena mwenye PhD ya ukweli si ya kughushi wala kuzawadiwa.
Kwanini nami nisipe uprofesa emeritus?
Chanzo: Mwananchi leo.
No comments:
Post a Comment