The Chant of Savant

Wednesday 21 February 2024

Niamini SGR Itaanza Majaribio Yesu Akirudi

Tangu kaya ianze kujimwambafy na kujaribu kujenga reli ya mwendo kasi usio kasi ila ukakasi, nini kimefinyika? Kwa tuliojua kila kitu, tulifyatua kuwa mngonje baadhi ya mafyatu wafyatue njuluku na ngonjera tamu tamu katika hii kaya ya majaribio. Hamjakisikia Kibashiti kikishitshit kila mahali kinatatua matatizo wakati chenyewe tatizo nambari wani kama Riz One? Tangu lini kaya ikiwa maabara ya kufanyia majaribio ya kila usanii. Heri maabara hufanyiwa majaribio ya kisayansi na siyo jinai na ubangaizaji. Japo kaya yetu inapaswa kuitwa Tanzamajario, leo nitagusia jaribio moja tu hapo juu na kuacha mengine mengi kama vile na Dip Weed na waishiwa wa Covid-19 ambayo naamini mafyatu wengi bado wanayakumbuka hata kama wameufyata ili wafyatuliwe hadi wafyatuke. Mfano, hawa Covid-19 wa njengoni wanapokea marupurupu kwa stahiki vipi zaidi ya kubebwa na CcM ambayo nayo inategemea mafyatu kuishi?

            Ifuatayo ni historia fupi siyo ya ujenzi ambao umegeuka ujembuz  na rongorongo za kuwafyatua mafyatu kuwa sasa Shrewd Goof Railroad (SGR) itaanza kuwasafirisha wao na mizigo yao wasijue kumbe SGR ni mzigo wao. Alianza doktari Ashantu Kijudge ambaye alifungua dimba akisema kuwa majaribio ya safari, siyo safari, ya SGR yataanza 12/11/2019.
         Baaada ya Doktari Kijudge kuchemsha alikuja doktari Doktari Hasani Abasi akadai kuwa safari za rongorongo zingeanza mwaka 2021 iwe mwanzoni au mwisho, siyo muhimu. Jiulize. Zilianza? Nope. Kwanini? Kamuulize huyo fyatu aliyefyatua haya yote au waliomtuma kutufyatua akaishia kuwajifyatua na kuwafyatua tulipostukia hii janja uchwara. Baada ya hapo alikuja doktari Leonadi Chamuliro akidai majaribio, siyo safari, yangeanza Agosti 2021. Yalianza au la? Wote mnajua. Je ni aibu kwa sirkal au aibu? Mtajibu wenyewe.
        Baada ya Chamuliro, alikuja kubwa lao waziri kuba sana dugu yangu Katelefoni Maja Liwa aliyetufyatua kamba kuwa safari za madanganyio na mafyatulio zingeanza Julai au Agosti 2021. Guess what. Hapakuwa na cha safari wala zali bali kafiri, sufuri, rongorongo, na aibu kwa sirkal ya siri kali. Hivi hawa mafyatu wana kumbukumbu au ni mataayira yaliojificha kwenye unene feki? Baada ya kuona mambo yameiva tokana na mafyatu kuamini kila urongo na upuuzi, si alikuja Mkuugenzi Ma-son-ja Kadogo Sir aliyesema, kama mabosi wake Chamu na Katelefoni kuwa mambo yote yangekuwa mswano kuanzia Agosti 2021. Mwe! Nini kilijiri? Utopolo mtupu. Sijui kama hawa jamaa zimo au la.
        Kuona hayawi, Katelefoni Majiliwa alirejea na kujipiga mtama akisema kuwa majaribio, siyo usafiri, yataanza kati ya Januari au Desemba, 2022. Kama vile hawa mafyatu wanene wababaishaji wanashindana ushahidi au ni vipofu kama nondo, Kadogo Sir alirejea akasema majaribio yangeanza Aprili 2022. Yalianza? Jibu na sema wewe fyatu uliyekuwa ukingojea huu usafiri. Mwenzenu situmii garimoshi kwa kuogopa moshi. Huwa natumia pipa ili kuwakoga mafyatu ambao hawajawahi wala hawatawahi kutumia pipa kupaa bali kutengenezea gongo.
    Baada ya bana kuba Katelesimu, si naye Atupile mwakibwete alitia guu asijue anajichafua kabla hajafyatuliwa na kubwagwa na maza. Alisema  safari za majaribio zingeanza Februari 2023. Zilianza au la? Jibu mwenyewe. Baada ya hapo alikuja Gereson or son of gere Msigwer alikazia kauli ya Mwakibwete kuwa majaribio yangeanza Februari 2023. Je yalianza? Iko uliza veve dugu yangu ile kuba nafanya kama taira nadanganya kama toto na hapana fatua na fanya kweli kama ile fatu fatukaji fatuzi nafatua gazetini fatu yote some japo iko jinga na shukua hatua komesa hii fatu na fatuma nafatua vote fat. Sisi kule Bombei fatua kila fatu hadi vote nafatuka na kukimbia kuja fatua nyinyi jinga hapa. Hapana ona namna natajirika nyinyi nakufa sikini tokana na jinga yenu dugu yangu? Sasa nadanganywa safari ya SGR iko fanyika na najua haiku. Kwanini ruhusu hii jinga kuba fatua ninyi kama kweli iko fatu?
        Tuendelee baada ya kufanya lecture ya KanjiKadogo Sir alijua urongo huu akaukanusha kwa  kufyatua mwingine kuwa mambo yangeanza  Mei 2023. Baada ya kufika Juni,  Msigwer alijibu kwa rongorongo nyingine kuwa safari za majaribio, siyo safari, zingeanza Julai 2023.
        Funga kazi ni Mahame Mbawala waziri wa Uchukuaji alipona mwaka unayoyoma akasema majaribio yangeanza Januari mwaka huu. Ninapofyatuka ni Februari. Sasa niaminini mie. Safari za majaribio ya SGR zitaanza siku Yesu atakaporudi kuja kuzoza nami ili nimpe inshu zote. Ukiangalia ubangaizaji wote huu unajifunza kitu kimoja kikubwa na muhimu. Hakuna cha SGR wala nini bali rongorongo na upigaji. Nikiangalia yanayongoja kaya hasa uchakachuaji ujao ambao maza amekamia. Mafyatu watapigwa na kufyatuliwa hadi wakome wasipofyatuka wakafyua badala ya kuufyata na kuamini kila upuuzi. Naweza kusema kuwa SGR haitajfanya majaribio ya safari achia mbali safari zenyewe hadi Yesu arudi. Hapa sijagusia migao ya maji na mameme.
        Hivi Yesu anarudi lini?
Chanzo: Mwananchi leo.

No comments: