Kisa cha
jamaa yetu toka tena kwetu Tanzania (mji hatutaji) kinafikirisha na kufundisha
kwa wale ambao hawajaingia mkenge kama huyu bwana. Akiwa amesikia mazuri mengi
juu ya kuukata kwa kwenda majuu, jamaa alianza mipango ya kwenda majuu kwa njia
yoyote ili mradi mambo yake yamnyokee. Alitaka kuukata asijue unaweza kumkata
yakamkuta ya kumkuta kama yalivyomkuta. Sawa na vijana wetu wengi, baada ya
mambo kuwa magumu na kuwepo misifa mingi juu ya majuu, kijana aliamua kuingia
mawindoni kusaka fursa za kumwezesha kukamilisha mipango yake ya kuukata.
Kwanza tukiri. Huyu jamaa alifanya utafiti japo si kwa makini. Hakuwe peke
yake. Vijana wetu wamejikuta kwenye hatari mbali mbali kama vile kuingia kwenye
mataifa ya watu kinyume cha sheria na kuishia kurudishwa hata kufungwa huku
wakishuhudia ndoto zao zikiyeyeuka.
Zamani walikuwa wakizamia kwenye meli. Siku hizi hii njia ni kama imezibwa. Wapo wanaoamua kuomba vyuo ng’ambo ili waweze kuingia kule. Wakishaingia, hukimbia vyuo na kutafuta vibarua lau wajikimu na kuanza pilika za kupata makaratasi ya kuwawezesha kuishi kule kihalali. Wengine huamua kuoa hata kuolewa ili waweze kuishi kule. Kutokana na hii, vijana wetu wengi wanaolewa na wanawake wa Kizungu ili iwe passport ya kupandia majuu. Katika kisa hiki, picha hii inajitokeza kama tutakavyoidurusu.
Tupo kwenye supermarket na jamaa toka Sudani. Bila hili wala lile, anatuijia mama Kizungu akiwa na watoto machotara wa Kiafrika na Kizungu. Kwa kuona hivyo, tunajua huyu mama kaolewa na Mswahili mwenzetu. Tunajipa moyo kuwa yupo sehemu akifanhya manunuzi, hivyo, akimaliza, atatokea japo tujuane. Wakati tukiwaza hili, yule mama wa Kizungu atujongelea na kutusalimia kwa uchangamfu kana kwamba tunajua. Hatushangai. Ni shemeji yetu hata kama hatujui atokako mumewe. Maana, huwezi kujua. Anaweza kuwa mweusi lakini siyo Mwafrika hasa kama anatokea Caribbean au Amerika ya Kati. Baada ya kutumakua kwa Kiingereza, nasi, bila ajizi wala hatujivungi. Tunajibu salamu zake. Anatuuliza “nyie mnatokea Afrika?” Tunamjibu kwa bashasha “haswa.”
Mama wa Kizungu anatuuliza swali ambalo si Wazungu wengi huuliza kwa vile, kama ilivyo kwa Waswahili kuwa kila Mzungu anatokea Ulaya, nao wanadhani kuwa kila mtu mweusi anatokea Afrika bila kujali nchi walizotengeneza wao. Anauliza “mnatoka nchi gani Afrika?” Swali lake linanishangaza na kunifikirisha. Nami nauliza “umewahi kwenda Afrika? Anajibu “ndiyo, naijua Tanzania ambako ndiko anakotokea mume wangu ambaye bahati mbaya nilimzuia kuja nasi ili akae na watoto.”
Msudani mmoja anadakia huku akionyesha kidole kwangu “huyu jamaa anatokea Tanzania.” Mama anatabasamu. Napigwa na mshangao tokana na Wazungu wengi kudhani Afrika ni nchi moja. Hivyo, wengi hawajui kuwa Afrika ina nchi zaidi ya hamsini walizotengeneza japo sasa wanaziunganisha. Namuuliza “ni wapi unajua Tanzania?” Anajibu “Arusha, Zanzibar, na Darasalam.”
Baada ya maongezi mafupi, nawataka radhi tuondoke. Yule mama anatuaga kwa furaha akisema “kama mnaishi hapa, tutakutana tena na mtaongea na mume wangu.” Nami namjibu, “hatuishi hapa. Tunaishi mpakani na Marekani kama kilometa 40 toka hapo japo huwa tunakuja mara nyingi hapa kununua bidhaa.”
Baada ya kuachana na yule mama, Msudani mmoja anasema “wallahi huyu mama kanifurahisha. Anaipenda Afrika.” Namkatalia. Namuuliza “umesikia alivyosema kuwa anasikitika alimzuia mumewe kuandamana nao ili akae na watoto?” Naongeza “huoni kuwa mwenzetu kaolewa?” Jamaa anastuka. Namwambia “huyu Kawajia yaani mama wa Kizungu hafai.” Tunaachia maongezi hapo na kwenda zetu. Nilipofika nyumbani, nilimpa Nesaa kisa kizima yakaishia hapo.
Baada ya kama mwezi mmoja, tulirejea na familia kununua mahitaji kawaida. Bila hili wala lile, mwanetu mmoja anasema “naona Waafrika wale.” Kugeuka, tunamuona yule mama wa Kizungu na mumewe Mwafrika wakitujongelea. Mama wa Kizungu ananisalimia kwa bashasha. Anamwambia mumewe “ni yule jamaa niliyekwambia.” Tunapeana mikono jambo ambalo Wazungu wengi huwa hawafanyi. Namgeukia Nesaa na kumwambia “huyu ndiyo yule mama niliyekwambia.”
Familia mbili zinachangamkiana wazazi na watoto. Mume wa Mzungu ananiuliza kwa kiswahili fasaha na mshangao “hii ndiyo familia yako?” Namjibu “naam.” Anajibu kwa kunyong’onyea “heri wewe umekuja na mkeo.” Nilimuuliza “mwenzetu Tanzania unatokea wapi na ilikuwaje ukawa huku?” Jamaa alitaja atokako Tanzania na namna alivyokuwa akifanya kazi kwenye utalii walopokutana na mkewe wa Kizungu wakaamua kufunga ndoa. Japo hakusema, lengo la kufanya hivyo ilikuwa ni kuukata kwa kuja majuu ambako uliishia kumkata.

Japo si wote, wengi wa vijana waliojiingiza kwenye ndoa hizi
huishia kuolewa na kutumikishwa mbali na kutumiwa kuzaa watoto ambao kwa nchi
zenye upungufu wa watu ni mali, huyu jamaa unaweza kumuweka kwenye kundi hili.
Isitoshe, si yeye tu. Wapo wengi ambao, mara nyingi, hujutia uamuzi wao pale
wanapojikuta wakimilkiwa na kutumikishwa kama mashini za ngono na watumwa wa
mapenzi.
Kufupisha kisa kirefu, yule bwana, pamoja na kunituchangamkia, hakuonyesha nia ya kutaka tumjue lau kutukaribisha siku moja tutembeleane. Hakutoa namba yake ya simu. Nami, kadhalika, sikutoa namba yangu ya simu. Kwa lugha ya mwili, hakuwa tayari kuwa karibu nasi. Nami nilifahamu ni kwanini. Angependaje tuwe karibu tuone anavyoishi? Pia, tunadhani alijua tunajua waume wa namna hii wanavyoishi kama tutakavyobaini kwenye kisa kingine cha Mfilipino aliyeolewa na mama wa Kizungu.

Chanzo: Mwananchi J'pili.
No comments:
Post a Comment