Japo inaweza kuonekana kama jambo la ajabu, siku hizi, kumeibuka fasheni au tuseme utaratibu wa baadhi ya watu kusherehekea talaka. Hili, kwa kizazi cha zamani, ni ajabu na jipya. Japo kusherehekea talaka kunaanza kuzoeleka baada ya kutangazwa sana mitandaoni, kiakili na kiuhalisia, kuna la kusherehekea na kushangilia katika talaka? Hili ndilo swali litakalotushughulisha leo.
Swali ambalo wengi wanaweza kujiuliza ni je, wahusika wanatuzunga kwa kutafuta umaarufu au kiki? Ni kweli wanafanya hivyo kutokana na furaha au kujiliwaza, kukomoana, hata changamoto ya afya ya akili? Kwenye chapisho na Waite na wenzake (2002) la Does divorce make people happy?, walihitimisha kuwa kinachoitwa furaha ya kuachika si furaha bali mlinganisho wa masahibu aliyopitia mhusika na kuwa nje yake. Zimmermann na wenzake (2006) kwenye chapisho lao la Happily ever after? Cohabitation, marriage, divorce, and happiness in Germany walifanya utafiti nchini Ujerumani. Walihitimisha kuwa maisha ya ndoa huleta furaha na ridhiko na talaka ina athari hasi.
Je, talaka, hata kwenye dini zinazoruhusu, ni jambo la furaha au huzuni? Anajibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu, Dk Dorothy Gwajima “kikawaida ndoa ni jambo la heri na furaha, na talaka ni jambo la huzuni, ambalo haitarajiwi.”
Je, wahusika wanakuwa na ndoa za kupanga ili zitakapovunjika wafanye sherehe na kupata wanachodhamiria? Je, zinakuwa ndoa za kweli walizoingia bila maandalizi au kwa kufuata vitu fulani ambapo wakivikosa, wanavunja ndoa na kusherehekea kujitoa kwenye kifungo cha kujitakia?
Tukio lilotangazwa hivi karibuni nchini ni pale mama mamoja jina hatutaji, alipoarika watu kusherehekea kuachika. Hapa, pia, kuna mashaka na maswali; kwa sababu mhusika anaelezea kuwa ameachika mara tatu.
Tuzidi kudurusu. Ukitaarifiwa msiba wa ndugu ya jirani yako na ukakuta kuna sherehe na si matanga, utafanya nini? Utajenga dhana na kutoa hitimisho gani? Je, binadamu tunaanza kubadilika hadi kushabikia na kusherehekea misiba na majanga? Kusema ukweli, ni vigumu kujua msukumo na sababu vya kufanya haya zaidi ya kutaka kiki au kukomoana kwa walioachana. Je, inawezekana wanaosherehekea, kama kweli walikuwa kwenye ndoa, ndiyo chanzo cha kuvunjika ndoa zao? Je, ni tangazo kuwa wanaotaka kuchukua mzigo wachukue au kuhalalisha mipango iliyofanyika nyuma ya pazia ambapo mtalaka hujenga mazingira ya kufanikisha kuishi na yule aliyemtaka na kusababisha kuvunja ndoa yake?
Turejee mfano wa msiba. Ukikuta mtu anashangilia na kusherehekea msiba wa ndugu yake, zaidi ya kujenga dhana kuwa ndiye muuaji, nini zaidi unaweza kudhania? Ajabu, wanaoonyesha kusherehekea talaka ni wanawake. Yupo mwanamke mkenya aliyepata umaarufu kuwa kutangaza na kueneza fasheni hii kiasi cha kuwa chanzo kizuri cha kumuingizia fedha tokana na TikTok kumlipa kwa kuwa na wafuasi wengi. Hatujaona sherehe ya kuacha iliyoandaliwa na mwanamme.
Japo bado ni mapema kutoa hukumu dhidi ya utamaduni huu mpya, tukiri. Lazima kuna tatizo fichi na kubwa. Kama jamii, tuikabili changamoto hii ili taasisi ya ndoa isibomolewe tokana na malengo na matendo ya watu wachache wenye ajenda fichi. Maana, si kawaida binadamu kupigwa akacheka badala ya kulalamika na kulia au kupata hasara akasherehehekea.
Tumalizie na ushauri wa Dk. Gwajima aliyekaririwa akisema “wataalamu wa masuala ya ndoa, saikolojia, mahusiano, migogoro na wengine kuja na tamko baada ya kuitafiti changamoto hii ili kuepuka kuwavutia vijana wakaishia kusababisha hatari kwa ndoa zao. Kwani, bila ndoa, hata kama siku hizi watu wanaweza kuzaa nje ya ndoa, hakuna taifa. Na kama lipo hasa likitokana na utaratibu wa nje ya utaratibu uliokubalika, litakuwa ni taifa la hovyo na hatarishi.
Baadhi ya mambo ni ya kudurusu na kufikiria kwa makini na si kufuata mkumbo.

Kwa wengi, hasa wanaofunga ndoa zisizo na vipengele vya kuachana kirahisi kama wakristo, talaka haishangiliwi wala kusherehekewa. Ni msiba na bahati mbaya kwa walio wengi. Je, nini husababisha kusherehekea talaka? Mbali na utamaduni na malengo ya wahusika, si rahisi kutoa jibu moja au mawili.
Chanzo: Mwananchi J'pili leo.
No comments:
Post a Comment