Tuanze na usemi maarufu kuwa elimu ni ufunguo na elimu ni nyenzo inayoweza kuleta mageuzi ya kweli na kubadilisha jamii pakubwa kama alivyowahi kuasa nguli Nelson Lolihlahla Mandela. Kwetu binafsi, Nkwazi hakutaka kusomea shahada ya Uzamivu (PhD) lakini Nesaa alimghasi hadi akaamua kuisomea na kuipata. Kwa muktadha huu, juzi, kilitokea kituko kati ya vingi vinavyofanyika na kutoripotiwa au wahusika kushughulikiwa kisheria chini ya kisingizio cha mila na tamaduni.
Kwenye kisa tajwa hapo juu, wazazi wajinga, wapumbavu, na wenye tamaa walitaka kumkatiri binti yao eti wakitaka wamuozeshe wapate utajiri. Ukiuliza ni utajiri gani huu na kiasi gani unaoruhusu na kuwezesha ukatili na unyama huu licha ya ukosefu wa ubunifu na uvivu, unashangaa na kuumia. Wazazi hawa laanifu wasioona mbele wala nyuma, walitaka kumuozesha binti kwa shilingi milioni nne na ushei! Yaani tumefikia pabaya hivi kiasi cha kumlinganisha binadamu na fedha zinayokuja na kupotea ilhali akabakia katika majuto na mateso visivyo na sababu zaidi ya ulafi, uroho, upofu, na tamaa?
Kwanza, unapomuuza bintiyo kwa tamaa na upofu huu, unampa fursa aliyemnunua kwa kisingizo cha kumuoa kumtenza kama mali na kifaa alichonunua tena kwa bei mbaya. Unataka mamilioni ya fedha, unauza nini? Ni wangapi hujiuliza swali hili na mengine mengi au kuvaa viatu vya wahanga hawa wasio na hatia isipokuwa kuzaliwa na wazazi mafisi na wapumbavu wenye uroho usiomithilika? Je, hii siyo jinai inayopaswa kuadhibiwa vikali ili kutoa onyo kwa wengine wanaoshindwa kutafuta na kujikwamua toka kwenye umaskini kiasi cha kuishiwa na kutegemea mabinti zao kuwa chanzo cha utajiri uchwara?
Pili, japo kuoa na kuolewa ni jambo la heri, hata hivyo, lifanyike kwa hiari na makubaliano kwa nia ya kuanzisha familia na si kuuzana. Baba unataka na kudai mamilioni ya fedha! Kwani bintiyo ni ng’ombe au shamba uuze na kujinasua kwenye umaskini?
Tatu, wazazi mnapowauza mabinti zenu, licha ya kuwakatili na kuwadhalilisha, mnatoa mfano gani? Hizi siyo zama za ujima za kuuzana na kudhalilishana. Kumuuza mwanao kuna tofauti gani na utumwa uliopigwa marufuku duniani tokana na udhalilishaji, unyama, na ukatili wake? Binti wanaouzwa, wana tofauti gani na mbuzi au ng’ombe?
Nnne, kwa mujibu wa gazeti la The Daily Monitor (Agosti 2, 2026) la Uganda, hali imekuwa mbaya nchini humo hadi rais Yoweri Museveni amelazimika kuingilia. Baada ya kupata taarifa kuwa kuna wazazi wanawauza mabinti zao kwa kisingizio cha kuozesha, Museveni alinukuliwa akisema “Wanyankole...ng’ombe 16...kwanini utake kutajirika kupitia watoto?”
Tano, kwa vile hili ni janga linalokua si Uganda tu bali katika nchi nyingi hasa baada ya maisha kuwa magumu, tunatoa angalizo kama wandoa na wazazi. Msifanye watoto wenu kuwa chanzo au mtaji wa kupata utajiri hadi mnawauza na wengine, kuwakatisha masomo na kuharibu maisha yao ya baadaye kama kisa kingine kilichotokea hivi karibuni kule Shinyanga ambapo wazazi walitaka kumkatisha binti masomo kwa thamani ya shilingi milioni nne na ushee.
Sita, hivi, mbali na ujinga hata upumbavu, tamaa na ukatili wa kijinsia, hawa wanaotenda jinai hii kweli wanajua thamani ya binadamu? Utashangaa kukuta hawa wanaotaka mamilioni, hawajawahi hata kumaliza kulipa mahali za wake zao.
Saba, kabla ya kufikia uamuzi wa kumuuza mwanao, jikumbushe. Hivi, wanaawake waliofanya makubwa duniani kama vile Ellen Johnson, rais mwanamke pekee wa Liberia, Nandi-Ndaitwah (Namibia), Magreth Tatcher Waziri mkuu wa zamani wa Uingereza, na wengine kama hao wangelazimishwa kuozeshwa na kukatishwa masomo yao, wangeweza kufanya makuu waliyofanya?
Nane, binti yako siyo chimbo la dhahabu wala nyenzo ya wewe kupata utajiri wa haraka. Ana haki na thamani sawa na binadamu yeyote. Mpe muda na uhuru wa kuamua ni lini ataolewa. Kwani, kuna usemi kuwa ukimuelimisha mwanamke, unaelimisha jamii nzima kwa ujumla. Tuna wanawake wafanyabiashara na wasomi maarufu nchini. Tujiulize. Kama wangeuzwa kama huyu binti wa Shinyanga, wangekuwa wapi?
Tuhitimishe wa kuzishauri mamlaka zetu kuhakikisha jinai na kadhia hii inakomeshwa mara moja ili kuwanusuru mabinti waliopata bahati mbaya kuzalilwa na wazazi katili na mafisi. Pamoja na ulazima na umuhimu wake, ndoa isitumike kama kisingizio cha kkuwakatili watoto wetu. Kesho ije kwanza na mengine yafuatie. Tuwape haki ya kuchagua ima kuolewa au kujielimisha na si kuuzwa utumwani kwa kisingizio cha ndoa.

Chanzo: Mwananchi J'pili, jana.
No comments:
Post a Comment