How the Berlin Conference Clung on Africa: What Africa Must Do
Monday, 22 September 2008
As Thabo Mbeki heroically exits
Though the political long and noble journey of Comrade Thabo Mvuyelwa Govan Mbeki may seem to have lapsed in a tragicomedy, chances are, just soon, we will remember him.
He exits without any participation let alone in economic corruption. What an ideal and exemplary leadership!
He did not stage any fight when ANC called shots as to "recall" him back as if he was unwanted material. The sage has it. Whoever live by sword he will die by it. Ours is to patiently wait and see. How many kit and caboodle of swindlers and freebooters Africa does have that need to be recalled? Sadly they have hijacked Africa and her people. The sage has it, the good ones never live longer as in the case in point.
Mbeki's journal is nobly over. Jacob Zuma's uphill one is commencing. Will he deliver? Time will surely tell.
Mbeki goes with a legacy. He believed in what he believed in especially democracy and liberation.
Differently from other African Potentates like Yoweri Museveni, Paulo Kagame, Theodore Nguema, Meles Zenawi,, Robert Mugabe, Omar Bashir, Omar Albert Bongo, Hosni Mubarak, Denis Sassou Ngweso, Yahya Jammeh, Muamar Gadaffi, you name it, Mbeki did not live in phantasmagoria and bulimia.
Go Mbeki go. Fare thee well for the job fare-thee-well done. You had a vision-cum-mission despite being foiled and recalled.
You have ushered in a new dawn for Africa in that country should come first and party last.
You answered the call nobly and open minded and hearted. Go doyen go. Never say anything. God himself will speak one day.
Africa thieves we call presidents that hide behind rotten-party politics have to take a note.
You were a lion of a man Mbeki. But never turn back. The world will speak itself on your behalf. Go join Nelson Mandela, Kenneth Kaunda, Joachim Chissano, Ali Hassan Mwinyi and others whose legacies shine. Step aside and look on. Time will come when the side stone that builders rebuffed will be the best of all stones.
The man is the one that stands alone.
Cry not Mbeki. For your legacy will for ever defend you as it speak for you. Cry not. For you are not leaving in shame like Benjamin Mkapa, Bakili Muluzi, Fredrick Chiluba and other hyena like mumbo jumbos. You have left as clean as when you stood to fight apartheid. What a noble exit!
Go Mbeki. But one thing is eminent. Rest assured. For what forced you out is nothing but opening Pandora's box. What even pains a lot is the fact that your shoes are so big that those day dreaming can step into them will soon find how wrong they are.Is Mbeki’s exit opening of Pandora’s box? Will this be like Gorbachev’s kaput perestroika for ANC as pro-white parties eye the state?
Nkwazi Mhango
Je Kikwete ametimiza matarajio huku muda ukiyoyoma?
Wiki ziliyopita tuliangalia jinsi ziara za mara kwa mara nje ya nchi za rais Jakaya Kikwete zilivyo hasara na balaa kwa taifa.
Wiki hii tunajadili balaa jingine kuhusiana na Kikwete hasa unapokuja mstakabali wa taifa. Hatufanyi hivi kwa kumchukia bali kumpenda. Maana kumekuwapo na madai uchwara kuwa vyombo vya habari vinavyomkosoa vinatumwa na wabaya wake kufanya hivi. Huenda vipo vinavyotumwa. Lakini siyo safu wala gazeti hili. Kinachotusukuma kutoa mchango wetu kwa Kikwete ni kutaka wananchi wetu waishi maisha waliyoahidiwa naye. Basi.
Hakuna ubishi: rais Kikwete tangu aingie madarakani hajakidhi matarajio ya watanzania ukiachia mbali ahadi alizozitoa kwa hiari yake mwenyewe.
Ni miaka takriban mitatu tangu ‘achaguliwe’ kwa kishindo cha Tsumani ambacho kinaanza kugeuka Tsumani kweli hasa kimadhaa.
Wakati wa kampeni, hata baada ya kutawazwa, Watanzania walionyesha kuwa na matumaini makubwa naye. Taratibu, mambo yalianza kuchacha. Aliyedhaniwa ndiye akawa siye! Alipounda serikali yake mabaka na mabaki ya Benjamin Mkapa (rais wa awamu ya tatu), watu wakaanza kujua kilichokuwa nyuma ya pazia. Walianza kuelewa. Kipya kinyemi japo kidonda.
Mara maneno yakaanza kusikika: Msanii, Fisadi, Chekacheka na mengine mengi. Bahati mbaya naye aliridhika na utani huu ingawa unabeba ukweli. Hakujibu wala haonyeshi nia ya kufanya hivyo! Je anajua madhara yake kwa utawala wake huko tuendako?
Katika kuwatathimini watawala wazuri na wabaya kuna dhana nyingi. Tunasema watawala. Kwa sababu siku hizi Afrika haina viongozi. Walikwishatoweka. Na hatujui kama watarejea.
Katika kuelezea aina za watawala, wachambuzi tuna aina nyingi mojawapo zikiwa, wenye masikio makubwa na midomo midogo. Hawa ndiyo wanaotufaa. Husema machache na kutenda mengi. Hawa ni nadra kuwapata katika kizazi cha sasa cha rushwa na ubabaishaji.
Wapo wenye midomo mikubwa na masikio madogo. Hawa ni wengi. Hawa hawafai. Ni waongo na waropokaji. Kama MC, wanaweza kusema lolote bila kuchelea matokeo ya maneno yao. Wanaweza kuwaahidi watu asali wakawapa usaha na shubiri. Wanaweza kuahidi pepo wakatoa jehanamu. Wapo. Na ni wengi kweli kweli. Wapo kila nchi, wizara, mkoa, wilaya na kijiji.
Hawa kama matapeli wamewaumiza wengi. Tofauti na matapeli ambao huumiza watu binafsi, hawa wameumiza mataifa.
Kuna kundi la tatu ambalo ni matokeo ya jicho langu. Hawa ni wale wenye midomo mikubwa lakini bila masikio. Hawa ni wengi kadhalika.
Je Kikwete ndugu msomaji unamuweka kwenye kundi gani? Yapo makundi matatu. Lile linalofaa; lisilofaa na hatari kabisa. Yaani la mwisho katika darasa la leo.
Ili kukupa picha kamili ngoja tutoe mfano mwingine. Jamaa mmoja mjivuni alikwenda hospitalini akiwa amefungwa kamba mkono mmoja huku mwingine ukiwa umevishwa glovu. Waliomuona walimshangaa wasijue alichokuwa akikitaka na kukimaanisha!
Alipofika alianza kuwatandika makonde wagonjwa! Baada ya kumaliza alianza kujisifu yu bingwa wa masumbwi duniani! Wenye akili walihoji. Ubingwa gani wa kushindana na wagonjwa? Leo utasikia watu wasio fikiria wakiimba amani amani na mshikamano. Je kweli Tanzania inavyo vitu hivi au ni kujilisha pepo? Tungekuwa na mshikamano tusingeibiana. Rejea ujambazi wa EPA na Richmond.
Turejee kwa Kikwete na kichwa cha mada. Je tangu aingie madarakani yapata miaka mitatu amefanya nini unaloweza kujivunia kama mpiga kura na mtanzania? Je ametimiza matarajio yako au amenoa kwa kiasi gani? Je huko tuendako anaonekana kuweza kuidhi au kuzidi kuyapoteza?
Mengi yameishaandikwa na kusemwa juu ya utawala wa Kikwete. Ingawa Kikwete amekuwa mgumu kidogo wa kubadilika, kuna haja ya watanzania kutoshika tama na kukata tamaa. Kuna haja ya kubadili mbinu za kuhakikisha wanapata kile tulichochagua. Hawakumchagua Kikwete kwa kumpenda kama Kikwete. Walichagua ahadi zake na sera zake ambavyo, kwa bahati mbaya, ameshindwa kuvitekeleza. Yeye bila kutimiza ahadi ni sawa na hayupo. Anatengeneza ombwe. Ni jambo la hatari kwa utawala wake hasa kama watanzania wataonyesha hasira zao kwenye uchaguzi ujao. Wana kila sababu ya kufanya hivyo iwapo Kikwete hatabadilika. Amewaangusha na kujiangusha.
Wapo wanaosema: amewakumbatia mafisadi huku akiwatosa wananchi. Rejea kutoshughulikiwa kwa mafisadi wa Richmond na EPA bila kusahau kumpa ulinzi rais wa zamani Benjamin Mkapa, familia na marafiki zake kinyume na utashi wa watanzania.
Pia rejea kutoa msamaha kwa mafisadi alikokutangaza hivi karibuni alipokuwa akihutubia bunge, Agosti 21, ambapo alitoa siku 71! Kwanini asingoje mahakama zikatimiza wajibu wake ndipo aingilie kisheria badala ya kuvunja sheria? Je haraka hii ni ya nini kama hana maslahi katika kadhia nzima? Maswali ni mengi.
Rejea kuendelea kuwa kimya juu ya kurejeshwa kwa mgodi wa machimbo ya makaa ya mawe ya Kiwira uliotwaliwa na Mkapa na familia yake.
Rejea kupewa orodha ya wauza mihadarati kama alivyowahi kukiri Kikwete na asiifanyie kazi. Anangoja nini? Nani anajua? Je hawa ni akina nani kwake? Nani anajua? Ataanza kuwashughulikia lini? Kadhalika hakuna ajuaye isipokuwa yeye.
Kikwete hata hivyo anao muda wa kujirekebisha. Ukichukulia na uvumilivu na ustaarabu wa watanzania ambao mara nyingi watawala wamekuwa wakiuona kama woga, kama hatafanya hivyo huko tuendako anaweza kujikuta matatani.
Maana watanzania, kama wakenya, wameanza kubadilika taratibu. Rejea kwa mfano tukio la hivi karibuni huko Matemange mkoani Ruvuma ambapo wananchi wenye hasira waliozoea kuwaua vibaka walimuua polisi baada ya kumtuhumu kumuua ndugu yao.
Reja tukio la mwanzoni mwa mwakani mkoani Tabora ambapo wananchi walichoma nyumba za viongozi wa kijiji waliotuhumiwa kujihusisha na ufisadi.
Je hali kama itaendelea hivi na Kikwete akaendelea kung’ang’ania marafiki na washirika zake bila kubadilika, huko tuendako ni salama? Je kwa kumchagua hatujajitia hasara na kwenye matatizo?
Sasa ndiyo wakati wa Kikwete kuanza kutekeleza ahadi zake alizotoa bila kulazimishwa. Muhimu apambane na ufisadi badala ya kuuacha uanze kugeuka sehemu ya serikali yake.
Chanzo: Dira ya Tanzania Septemba 23, 2008.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment