How the Berlin Conference Clung on Africa: What Africa Must Do

How the Berlin Conference Clung on Africa: What Africa Must Do

Tuesday, 30 June 2015

Kijiwe chakutana Simiyu


          Baada ya dada yao Mijjinga na Mipawa aitwaye Rhoda Bujiku kudhalilisha na kuteswa na nesi, walitutonya kama wenzao wanaoheshimika na kuogopwa kayani. Walitutaka tutie timu kule liliko tokea tukio ili kuwalazimisha watawala wetu washenzi kuchukua hatua. Hivyo, minutes za kikao hiki cha Kijiwe zinatokea Mjini Maswa mitaa ya Nyalikungu ambako tulipiga kambi kwa wiki kulaani unyanyasaji huu wa kishetani.
          Mijjinga anaanzisha mada, “Jamani mmesikia aibu ya dada yangu kunyanyaswa, kuteswa na kuaibishwa huko kwetu Usukusini?”
          Mipawa anachomekea, “Kaka umenigusaga pabaya ngwana wetu. Sikujua kuwa bado kuna watu wenye roho za kinyama na washenzi kiasi hiki?”
          “Yakhe mbona mie mwaniacha Solemba? Kwani hili mnoongelea wala sijawapata vilivo wallahi.” Mpemba analalamika.
          Mbwamwitu anadakia, “Ulitaka uwapate vilivo wapi na kwanini mbona Mpemba wataka kulete mambo ya Mpopobawa?”
          “Yakhe una haki ya kuachwa Solemba na usipate pa kutupata japo ukitupata nasi tutakupata au vipi. Anyways, nadhani tumefanya kosa kidogo. Tumeanzisha mada bila kufanya introduction.” Mijjinga anampasia gazeti la Danganyika Kwishnei Leo. Anaendelea, “Hebu soma kichwa cha habari utapata dozi yako.”
          Kabla ya kuanza kusoma gazeti Mpemba anajitetea, “Yakhe acha matusi. Kama wataka dozi weye si useme badala ya kuwasingizia wenzio. Kama wataka sema yakhe.”
          Mipawa anaingilia kati, “Acha niwachomekee kwa mpigo. Kinachogomba hapa si dozi wala nini bali kupataga habari kamili. Si usomage kazeti na kujua anachomaanisha nkwingwa.”
          Mpemba anajibu, “Yakhe nakuheshimu sana. Hivo ngoja nsoma lau nijue anichomaanisha huyu msukuma mwenzio.”
          Mgosi Machungi anaamua kutia timu, “Ami huna haja ya kusoma. Niishasoma hii habai iiyotokea kule Simiyu Maswa ya mjamzito kunyima huduma eti kwa sababu anazaa kia mwaka.”
          “Alaa kumbe. Kama habari ndo hii sina haja ya kusoma gazeti. Kwani bi Nkubwa alinieleza upuuzi na unyama huu wallahi hadi nikashindwa hata elewa inakuwaje kwenye kaya kama yetu haya mambo yanatokea.” Mpemba anajibu.
          Msomi anaamua kukatua mic, “Mnashangaa la mjamzito kunyanyaswa kudhalilisha na kuteswa! Kama umma wote unafanyiwa hivyo, itakuwaje kwa kiumbe mdogo tena wa mashambani kama huyu? Kilichofanyika si kipya. Upya wake ni kwamba vyombo vya umbea vimelipata an kulirusha hewani. Wako wajawazito wengi wanaotendewa mabaya hata zaidi ya haya.”
          Kabla ya kuendelea, Mzee Maneno anamchomekea na kusema, “Si wajawazito wote wanatenzwa hivyo Msomi. Wale wa kisiasa tunaowana na matumbo yao wasiyotwambia ni lini watajifungua wanatendewa vizuri.”
          Msomi anarejea, “Unaongelea wale wazembe wenye viribatumbo vya chumo la ufisadi. Hao achana nao. Tunaongelea wajawazito wa kweli ambao inaonekana sasa hawatakiwi hasa ikizingatiwa kuwa wachovu wanaongezeka kwa kasi ya ajabu.”
          Kabla ya kuendelea, Kanji anatia timu, “Lazima mama zae toto nyingi. Sisi Bombei iko zaa hadi mia.”
          Mchunguliaji anaingilia kati, “Kumbe nave Kanji iko pata mimba na kuzaa toto kama mama! Kanji iko kumbuka kuwa hata hindi hapa nazaa sana ili pate piga kura na kuwa bunge baadaye?”
          “Wallahi hakuna kitu kimeniuma kama kumnyima huduma mjamzito eti kwa vile anazaa kila mwaka. Kwa vile tupo hapa Simiyu, lazima tumtafute huyu nesi tumshughulikie lau aone kuwa kuzaa ni neema. Mie najitolea kumkamata na kumpa mimba ili aone uchungu wa mimba kama hajawahi kujaliwa kuzaa mnasemaje?” Kapenda anaongea kwa uchungu.
          Msomi anakwanyua mic, “Shehe Kapende unakokwenda ni mbali. Tujiepushe kulipiza visasi kwani hakujengi. Huna haya ya kumkamia huyo mpuuzi. Yaani kweli hasira hasara. Yaani unataka umbaki mwenzio bila kujali kama ana miwaya au ni mali ya mwenyewe! Tupunguze hasira ili tuweze kuwasaidia wajawazito na wahanga wengine wa utwahuti na ushenzi huu. Hasira hasara ndugu yangu.” Anakohoa kidogo na kuendelea, “Kaka huna haja ya kupambana na mbwa wakati mwenye mbwa yupo. Hapa nadhani tatizo ni lisirikali wala siyo huyu nesi ingawa naye ni sehemu ya tatizo ambalo ni kubwa kuliko hili tunaloona hapa.”
          “Wakati mwingine tuwe makini tunapolaumu. Sasa hapa lisirikali linaingiaje wakati aliyetenda upuuzi huu ni mpuuzi mmoja?”
          “Nashukuru kwanza umeuona upuuzi ingawa sikubaliani na utetezi wako wa lisirikali. Hujui kuwa kama sheria zingetumika kuwabana wapuuzi kama hawa wachovu wasio na hatia kama dada yetu huyu wasingeumizwa bure?”
          “Yakhe nakubaliana nawe. Twapaswa kuwajibisha lisirikali kwani ndilo liniowapa hawa wapuuzi jeuri ya kufanya upuuzi wao.” Mpemba analalamika.
          Mijjinga anaamua kumchomekea, “Nasikia huyu muuaji aliposikia tunatia ametimkia kusikojulikana kwa kuhofia tusimfanyie kitu mbaya. Nasikia wachovu wenye hasira walitishia kumchoma moto yeye na nyumba yake. Kwanza, nashangaa huyu muishiwa wa eneo hili ni nani mbona hasikiki akikemea lau upuuzi huu? Sijui kama huyu angekuwa mkewe angeweza kukaa kimya huku akikimbiza per diem mjengoni ambako nako hana analofanya?”
          Mipawa anadakia, “Unaualizia muishiwa wa jimbo hili wakati yuko kwenye madili mjengoni? Huyu jamaa ni wa hovyo kuliko yeyote aliyewahi kuwakilisha eneo hili. Hata hivyo, simlaumu. Kwani, anawakilisha tumbo lake mjengoni huku akipiga domo juu ya upuuzi na kuacha mambo ya maana kama haya.”

          Kijiwe kikiwa kinanoga si akapita mkubwa wa Wilaya. Acha tumtoe mkuku kabla hajaokolewa na wachovu tuisimfanyie kitu mbaya!
Chanzo: Tanzania Daima Julai 1, 2015

Monday, 29 June 2015

Breaking News: SOUL ON SALE is out!!!!!!!









































Dear readers and friends,
I am delighted to notify you that my new book Soul On Sale (SOS) is now out. By the way, I have submitted another one AFRICA REUNITE OR PERISH today.
The synopsis of the book
Soul On Sale (SOS) sounds like a rap song though it isn't. It isn't purely a poem but a long- provocative and vigorous song focusing on the history of injustices and those suffering from injustice urging them to take action. It explores colonialism, corruption and neocolonialism Africa faces. It chides victims to self-reinvent so as to change the status quo manned by begging and venal potentates. It seeks to provoke readers to feel empowered and responsible. Thus, stand and change the world's status quo sui generis. It employs an enthralling-flow style in free verse to catch the attention of the reader.
  • Publisher: Langaa RPCIG (June 16, 2015)
  • Language: English
  • ISBN-10: 9956762849
  • ISBN-13: 978-9956762842
  • Paperback: 118 pages

Wagombea CCM mtendeeni haki Kikwete


                   Imekuwa kama fasheni sasa. Kila mtangaza nia ya kutaka kuteuliwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kupeperusha bendera yake katika uchaguzi ujao, anamponda rais Jakaya Kikwete wanayenyukana kumrithi. Wanamuona kama mtu ambaye hana lake tena baada ya kutundika viatu mwishoni mwa mwezi wa kumi. Kila anayekuja anakuja na gea ile ile ya kufanya vyema kuliko Kikwete ambaye wanamuonyesha kama mtu wa hovyo, asiye na msimamo, mwoga na ambaye ameruhusu nchi ijiendee. Hawamtendei haki rafiki yao hata kama kweli ana udhaifu wake unaojulikana. Pia wanampomshambulia Kikwete bila kuushambulia mfumo uliomtengeneza, wanawandanganya wananchi. Kwani, bila kubadili mfumo jambazi wa sasa, hata akichaguliwa malaika ataondoka ikulu akiwa shetani. Huu ufisadi na ulegevu wanaomshambulia Kikwete kwao,licha ya kuushiriki, watautenda wakiingia madarakani. Kama tungekuwa na mfumo unaoshikisha adabu watawala baada ya kuondoka madarakani kwa kuwashitaki wanapofanya madudu, Kikwete sasa asingekuwa analaumiwa. Tuliyaona alipoondoka Benjamin Mkapa akiwa na tuhuma za kuiibia umma. Kesho atafuata Kikwete na kesho kutwa atafuata mmoja wa hawa wanaomuandama.
          Haiingii akilini watu wanaounda serikali ile ile kuitupia madongo wakati walikuwamo –na bado wengine wamo –ndani na walikuwa na uwezo wa kutoa ushauri au kurekebisha mambo kwa nafasi zao. Hata hivyo, wanaomshutumu Kikwete wakati walikuwa naye kitanda kimoja wana bahati. Angekuwa marehemu baba wa Taifa marehemu Mwl Julius Nyerere sina shaka. Angeishawafukuza wengi kazi ukiachia mbali kuwapaka kuhakikisha hawapenyi kwenye chujio la CCM. Washukuru Mungu CCM imeishiwa hata uongozi wenye kuweza kukaripia watovu wa nidhamu kama hawa. Hata hivyo, haimaanishi kuwa watu wasikosoe. Kinachopaswa kuzingatiwa ni kwanini wakosoe sasa wakati walikuwa humo humo wakitenda makosa wanayojifanya kukosoa sasa? Hii ni aina fulani ya unafiki unaonuka.
Kwa vile Kikwete amejigeuza punching bag –kwa sababu anazojua mojawapo ikiwa kuwamo ukweli kwenye madai ya wahusika –wanaweza kumtukana watakavyo na asifanye kitu kwa vile naye alipoingia aliingia kwa gea hii ya maisha bora kwa wote akinaanisha wakati ule maisha hayakuwa bora chini ya Mkapa. Ukimpiga mzazi wako nawe mwanao atakupiga tu. Inashangaza hata akina Salva Rweyemamu anaowalipa vizuri wafanye kazi ya kumtetea hawafanyi hivyo. Je nao wamemgeuka wakitafuta fursa ya kupata mwingine wa kuwatumia ili wamtumikie baadaye kama walivyofanya kwa Kikwete? Je hawa nao wanalipwa kwa kazi gani iwapo wanalala kwenye usukani?
          Makala hii hailengi kumtetea Kikwete. Hiyo ni kazi ya watajwa hapo juu hata kama hawaiwezi au kuigwaya kwa sababu ya maslahi binfsi baadaye. Tunachotaka kuweka wazi ni kwamba wananchi wasihadaike na kuwaona hawa wanaomkosoa au kufichua udhaifu wake ni tofauti naye. Ni wale wale. Jogoo wote hunya ndani kiasi cha kuwafundisha vifaranga. Wanachofanya ni utapeli wa kutaka waonekane wao ni safi wakati wamo kwenye dimbwi moja la matope liitwalo CCM. Kwa lugha nyingine ni kwamba anayeiponda serikali ya Kikwete akitokea mle licha ya kuwa moungo ni mnafiki ambaye anapaswa kuogopwa kuliko hata ukoma. Kwani, anajiponda mwenyewe au kujivua nguo akiadhani anamfanyia hivyo Kikwete. Kama ameweza kumgeuka huyo aliyemtengeneza atashindwa kuwageuka wananchi? Wanachosema kingekuwa na maana kama wangekuwa nje ya serikali husika tena baada ya kujitoa kupinga hicho wanachosema sasa. Waulize: Mlikwina au mlikuwa wapi?
          Ukisikia kauli kama hii iliyotolewa na waziri wa Mambo ya Nchi za Nje na Uhusiano wa Kimataifa Bernard Membe unashangaa. Membe alikaririwa akisema, Ninawatumia salamu mapema, sitakuwa na kigugumizi kwa wanaotesa Watanzania. Nitahakikisha Watanzania wanachukia rushwa na kutakuwa na sheria kali dhidi ya mtoa na mpokeaji rushwa. Kama ni watumishi wa umma, watakwenda na maji....” Je asemayo Membe ni ya kweli au funga kamba? Akiwa kama waziri alifanya nini kupigana na rushwa. Kama Membe alishindwa kupambana na rushwa kwenye wizara yake ambapo mabilioni ya shilingi yametumika kifisadi kwenye balozi zetu nje ataiweza nchi nzima?
          Mwingine aliyewaacha wengi hoi ni Samuel Sitta aliyekaririwa akisema, “Ili kukomesha tatizo la rushwa, hatuna budi kutunga sheria itakayotenganisha biashara na uongozi.” Ni ajabu anayesema haya ni mwanasheria na aliyewahi kuwa spika wa Bunge. Kwani Kikwete ndiye aliwazuia kutunga hiyo sheria au ni kamba kama kawaida ili uonekane una sera na mipango vya kuwakomboa wananchi wakati letu moja?
          January Makamba naye hakubaki nyuma kwenye kurusha madongo kwa serikali ya Kikwete aliyefanya kosa akamteua tokana na ushawishi wa baba yake. Sasa anamlipa ambavyo hakutegemewa. Alikaririwa akisema, “nitafanya mabadiliko ya kisheria, kimfumo, kitaasisi na kijamii ikiwamo kuipa meno Takukuru kuwa na mamlaka kisheria ya kuwashtaki watuhumiwa wa rushwa moja kwa moja mahakamani.” Hivi bila rushwa itokanayo na kujuana na kulipana fadhili Makamba angekuwa hapo alipo tokana na jina la baba yake?
          Mwingine aliyewaacha wengi hoi ni Stephen Wassira aliyekaririwa akisema, “Kumbukeni sijatajwa katika kashfa kama za Escrow, EPA, Richmond na nyinginezo.” Je aliyetajwa kwenye hizo kashfa zote zaidi ya rais Kikwete ni nani? Je kutotajwa kwenye EPA Escrow na Richmond ndiyo kigezo cha kuwa msafi wakati kuna kashfa nyingi zinapita bila kutangazwa wala kushughulikiwa?
          Tumalizie kwa kuwashauri wananchi hasa wapiga kura kuwa makini na waongo na wanafiki wanaofanya u-Petro wa kumkana Bwana na u-Yuda wa kumsaliti Bwana. Kambale wote wana sharubu na nyani wote mchezo wao ni mmoja. Hivyo, msiwaamini sana sana wakaange kwa mafuta yao kambale hawa.
Chanzo: Dira Juni 29, 2015.

Saturday, 27 June 2015

The world will miss you “Vasco da Gama”

          The other day my shushus, spies photocopied the diary of Mr Big whom detractors nicknamed Vasco da Gama of Africa due to his taste and love of touring the globe. After getting it, I decided to pen this piece to show the boozers how their dosh is burnt. I also decide to use this opportunity to make an evaluation of what Mr. Big will miss after being retired.
          Jokes aside, the guy loved globetrotting. To crown it, he loved to be accompanied by his cronies, courtiers, relatives and bootlickers.  Why had he to bother if the boozers picked the tab? So, today I am going to dwell on Mr. Big’s matanuzi to show how urahis make people mad. The y do so aimed at enjoying the world without paying any coin from their humungous mshiko paid for doing nothing but globetrotting. Today I am not going to beat around the bush. I am descending down to the issues.
          According to Mr. Big’s diary whose copy my shushus brought to me, the man has really seen the world. Methinks he is the most traveled ruler on earth up till now. If there is a person who can compete with him as far as globetrotting is concerned is none other than his namesake Vasco da Gama of Spain.
          Look at the entries of the diary. In January, the son of man toured France, Germany, Mozambique and Saudi Arabia (Just to console the royal grieving family for the loss of their king-Abdul). Ironically, when mzee Mchonga returned the number we did not see anything like that from Saudia! Was it kiherehere or what to not reciprocate the way the Saudis did when our beloved father of nation died or just mere ignorance and kujigonga because they have petrodollars? February saw the sightseer hit the road so as to tour Ethiopia, Kenya and Zambia. March as well saw the tourist in Burundi, Rwanda and Namibia while in April the tourist visited Algeria, Burundi and the US. In May the son of man was in the US once again! Try to imagine. How much dosh did the man burn in such hocus-pocus. I know his handlers will come up with many hoo-has such as claiming that the man was invited by the rulers of those countries he toured if not going there to attend some conferences. Well, does it mean that the man has to accept all invitations? If yes, why didn’t he send his aids such as the VP, the PM, or ministers even ambassadors to represent him? We don’t see Brack Obamiza globetrotting despite his country being rich and hegemonic so as to need to influence every hunk on earth.  Again, there some fyatus who say that the dude tours many western capitals seeking some cure for his ailment. So be it. But they must tell us the truth if it is true that the guy goes for such services.
          What’s more, since he came to ulaji, the dude has always concealed the number and names of those eaters that accompany him in his merrymaking trips abroad. Why has he been hiding the names of those eaters if there isn’t anything fishy?  Now that time for eating and touring for free is up for him, I am sure he’ll miss these trips the same way the world of tourism abroad will miss him dearly. I wish the coming head should be barred from abusing our dosh like this. It pains me beyond comparison especially when I am told that my dosh is spent by the dude in his begging missions. Why should we beg as if we have neither brains nor hands? Why begging while we throw away our resources not to mention offering tax holidays to swindlers and thugs knows as investors?
          Due to  the penury our hunk has always been in, one would think that the dude would stay in his office and plan how to revamp our bed-ridden economy. Instead the guy has created more of a financial and economic black hole to our coffers. I am told our debt has swollen hugely just because of globetrotting.
          Off the cuffs: The head of Promotion and condoning corruption Bureau (PccB) Eddy O’ shea spoiled my day when he asked foreign countries to help him in combating escrow as if he were serious.  Go tell it to the birds. Stop politicking. If you’re serious take on them instead of hoo-ha.  You know everything. If Swiss authorities offered to help you to unmask all that have accounts there you refused how will you work on new help? Go ask your boss who shields those criminals simply because they are in the same bed. Does an order to arrest Rugemalayer and Singa need any help from abroad? Please stop your big talk. If you can't work just put up or shut up.
Source: Guardian June 28, 2015.

Mlevi kuangusha hekalu Beach

Baada ya lisirikali kugwaya hekalu la mchunaji mwana siasa Gettie Rwakatarehe na ule mjengo uaji wa uhindini, mlevi anapanga kujenga mhekalu wake kwenye maeneo yaliyozuiliwa hasa kule Mbezi kwa wazito. Ili nisisumbuliwe lazima kwanza niongee na mheshimiwa Esta Ulaya asininange mjengoni kam alivyomtolea uvivu Rwkatarehe. Maana kama kaya hii isingekuwa na wenyewe hasa mafwisadi kama Rwakaterehe, kwa jinsi muishiwa huyu alivyosiliba, hili hekalu lingedondoshwa siku hiyo hata kama ni kazi hii kufanyika usiku lakini wapi!
Unajua muishiwa Ulaya alinangaje? Ngoja nimnukuu nisionekane ima namzushia au kuleta rongorongo. Alizoza tena mchengoni tena mbele ya mama Kipaza Sauti na kamera zote za runinga hata zile za mablog uchwara, “Jumba la Shilingi bilioni moja lile bomoeni…mnasema sheria ni msumeno, huu msumeno unakata kwa baadhi tu huku kwa wengine unakuwa butu?” Japo aliyosema muishiwa yana mashiko, namtaarifu kuwa aende akatambikie ndipo asikilizwe vinginevyo anatwanga maji usawa huu ambapo ngedere ndiyo waliokabidhiwa shamba la mahindi.
Kumbe muishiwa Ulaya hakujua kuwa sheria za Bongolalaland ni kama treni –hukata upande mmoja wa wachovu huku ukipuliza upande wa pili wa wanene kama akina Rwakaterehe, Rugemalayer, Singasinga na mafisadi wengine. Ukitaka kujua kuwa kaya yetu ni ya kitapeli na rongorongo, uliza ule mkwara wa yule mchunaji Gwajimama umeishia wapi. Jamaa kawakati chochote kitu wanene wakaamua kumgwaya na kufyata mkia.  Hebu niulizie hao ndata waliostukia ujambazi wa huyu mchunaji kiasi cha kutaka awasilishe kila nyaraka za ukwasi wake na asifanye hivyo. Acheni wachovu waliwe wanajiona kwa vile hataki kulianzisha lau kieleweke au pasitoshe kama si kuchimbika bila jembe.
Kama wajalaana wametuibia njuluku za escrew na kutu-screw mchana kweupe na wakaendelea kutesa na kutanua unategemea nini? Hamkumsikia fisadi mwingine eti naye anayegombea urahis akiwasifu akina Ni Ziro Kadamage kuwa ni matajiri wa kupigiwa mfano wakati ni majambazi ya kawaida yaliyojificha nyuma ya ukwasi na vyeo?
Hivyo basi, kwa vile dili langu la kuuza na kusambaza mibwimbwi na kufanya ujambazi mwingine linalipa, basi nitaangusha bonge ya hekalu tena karibu na lile la Rwakatarehe nione watanifanya nini. Nani mara hii kasahau mhekalu mwingine wa Heze Maige wa mabilioni ya njuluku ambao hauna maelezo? Nani ameishamweka kikaangoni aeleze alivyopata hayo maelfu ya dolari tena akalipa kashi. Mara hii mmesahau hata zile tambo za kurejesha njuluku za ughaibuni! Zimeishia wapi? Sana sana wajalaana na majambazi yanakamua na kuendelea kuficha nyingine zaidi huku wachovu na walevi wakiendelea kufungwa kamba kuwa lisirikali litarejesha njuluku wakati kiendacho kwa mganganjaa huwa hakirudi.
Ili kunogesha mchezo, nitavamia eneo wazi liwe la shule au mtaa mimi sijali. Nitalivamia kulitwaa na kuangusha kitu cha haja halafu nione watanifanya nini. Kama waliiba na kuuziana nyumba za kaya na wakaendelea kujikeshachekesha eti wanapambana na ufisadi wakati wanaupamba, nani aogope kuvamia viwanja vya wazi na kufanya kweli kama walivyofanya akina Rwakatarehe na majambawazi wengine?
Ili kuhakikisha project yangu inapeta, lazima niwaite wajalaana wa site na kuwakatia kitu kidogo wahakikishe ima wananighushia hati za kumilki kiwanja au wanafanya vitu kinyume cha sheria kama wenzao wa kwenye lisirikali wanavyofanya kwenye mikataba ya uchukuaji uitwao uwekezaji ili nikienda kwa pilato nipewe haki.
Siku hizi ujanja si kufuata sheria bali kuzivunja. Ujanja si kuwa muadilifu bali mbadhilifu. Wale wanatakaoshikilia uadilifu watachekwa hata na kunguru usawa huu ambapo kaya imegeuka shamba la bibi na chizi ambapo kila kinyama mwitu huja na kujichumia na kuukata na kutanua. Anayebisha aende akaulize wazee wa site ilipo kampuni ya wanuka jasho ya UdA. Si habithi mmoja akitumiwa na vigogo na watoto wao ameitwaa na kuimilki huku wazee wa site wakikatiwa chao na mchezo kuisha. Nasikia kuwa jamaa hawa majambawazi wakubwa wanyemelea mradi wa mangwala ngwala yaendayo kasi jijini ili wazidi kutengeneza njuluku. Kama yote haya yanafanyika na hakuna anayenyea debe, niogope nini kuangusha hekalu langu ugogoni na uzitoni kama Rwakatarehe?
Hata hivyo akina Rwakatarehe wana bahati ya mtende. Maana kama nisingeamua kucheza mchezo wao nikaamua kuwa upande wa pili ningewahamasisha walevi tukaenda kuangusha ule mjengo wenyewe bila kujali nani wala nini. Kwa vile ukienda Roma fanya kama waroma, uzalendo umeiniishia na kuamua kuwa kibaka na jambazi kama wao. Maana ukiangalia walevi ninaowapigania na kutaka waache kuliwa na kaya yao kubakwa, unapata kichefuchefu. Wadude wenyewe hawajitambui wala kutambua mazonge wanayoletewa na ngurumbili wenzao wanene. Sasa mimi niwafanyeje kama wameamua wenyewe kujirahisi na kuliwa mchana tena wakijiona? Hivi jamani, hawa wadude washikwe wapi ndipo wastuke?
Kujua kuwa walevi na wachovu wataliwa sana na kuendelea kufanyiwa kitu mbaya hebu soma maneno haya na Nipe Mapepe Ninaye yule kidhabi mkuu wa rongorongo chamani. Alisema, “Rangi inayoenda Ikulu ni hii (anaonyesha shati lake la kijani ambayo hutumiwa na chama hicho). Tuna uhakika na ushindi wa Rais. Kwa namna yoyote ile, CCM itarudi Ikulu hata kama ni kwa bao la mkono... bao ni bao tu ili mradi refa hajaona.” Hili ni tangazo kuwa Nambari wahedi itachakachua uchaguzi na kuendelea kuwashika mateka walevi. Pamoja na makufuru haya, umesikia nani akiingia mtaani kupinga njama hii chafu. Ama kweli walevi ndiyo waliwao. Msipobadilika mtaliwa sana wakati mimi nikijinoma kwenye hekalu langu ninalopanga kuangusha kama Rwakatarehe. Nyie liweni lakini mimi simo!
Chanzo: Nipashe Juni 27, 2015.

Thursday, 25 June 2015

Buriani Kamukara


Japo sikuwahi kukutana na marehemu Edson Kamukara uso kwa uso, tulifahamiana na kuongea sana karibu kila wiki kabla hajahama toka gazeti la Tanzania Daima.  Kamuraka ndiye aliyekuwa mhariri wangu katika gazeti la Tanzania akishughulika makala zangu mbili maarufu kama Kijiwe na Nyingine ambayo sijui waliipa jina gani.
Nikiwa najiandaa kulala, nilipitia kwenye mitandao japo kujua kilichojiri nyumbani. Kama kawaida huwa nasoma habari za huko hasa ikizingatiwa kuwa wakiamka tunalala na tukiamka wanajiandaa kwenda kulala. Hivyo, taarifa ya kifo cha Kamukara kilichotokana na moto wa jiko la mchina zimenichanganya kwa jinsi nilivyomjua kijana huyu ambaye alikuwa anaonyesha kuwa na bright future. Nimeona madhara ya mgao na umeme usio na uhakika umaskini na ushenzi mwingine vinavyoandama nchi za kiafrika. Ni bahati nzuri kuwa ni leo tu nilikuwa napitia kwa mara ya mwisho kitabu changu kipya cha AFRICA REUNITE OR PERISH ambapo masuala kama haya nimeyaongelea kwa undani zaidi.
 Kama nilivyodokeza hapo juu, sikumjua kwa sura japo tulijuana sana.
Kamukara alikuwa kijana si muaminifu tu bali mkweli na mstaarabu. Nakumbuka malipo yangu yakichelewa au kupunjwa tokana na makosa ya kiuhasibu alikuwa halali hadi anapata ufumbuzi. Kama hakuwa anacho anachojua aliweza kusema bila kuficha.
Kwa majonzi naona siwezi kuendelea. Ama kweli wema hawadumu.
NENDA SALAMA MAREHEME EDSON KAMUKARA
Mungu aiweke pema peponi roho yako.
Aaamiiiiiiiiiiiiiiiiiiinaaaaaaaaaaaa

Kinana: Wananchi si hamnazo


          Katibu mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Abdulrahaman Kinana huwa si mtu wa kuishiwa vituko. Wakati mwingine akiongea mambo huwa unashindwa kuelewa kama anaelewa anachosema au wale anawaambia kama anaamini kuwa wana akili kama yeye. Maana hujiongelea vitu wakati mwingine kiasi cha kuacha maswali kuliko majibu.  
Kwanza, amejitahidi kujionyesha kama kiongozi tofauti na wenzake kwa kutumia muda mwingi akitembelea mikoa na wilaya za Tanzania bila mafanikio. Anachofanya Kinana licha ya kuwa kinyume na bosi wake yaani rais Jakaya Kikwete ni kama suto kwa Kikwete. Wakati yeye akipenda kutumia siku nyingi vijijini mikoani, Kikwete anatumia muda mwingi kwenye majiji makubwa ughaibuni.
          Pili, Kinana huwa anatoa kauli za kujikanganya, kukanganya na wakati mwingine hata kujisuta. Mfano juzi alikaririwa akiwa huko wilayani Ngara akisema, “Msikubali kuyaachia mashamba yenu kabla hamjalipwa fidia. Lazima mpewe mkono kwa mkono na siyo vinginevyo, Serikali haiwezi kutekeleza mradi kama haina fedha za kutosha kuwalipa.” Kinana alikuwa akijibu malalamiko ya wananchi kuhusiana na ardhi zao kutwaliwa bila fidia wakati wa ujenzi wa miradi ya maendeleo. Inashangaza kuwa serikali inayofanya haya ni ya chama anachokiongoza Kinana. Kama siyo kuwahadaa wananchi –sijui wachague chama chake –ni nini wakati ana uwezo wa kwenda kuongea na wenzake wakalipa hiyo fedha ya wananchi?
          Pia Kinana akiwa wilayani Kyerwa alikaririwa akisema, ““Hakuna haja ya kutumia ‘pasipoti’ kuhudhuria harusi au msiba wa ndugu yako aliye nchi jirani, itoshe kutumia vitambulisho.” Je ni lini Kinana akawa waziri wa mambo ya Ndani au ya Uhusiano wa Afrika Mashariki? Je anapotoa amri kama hii haingilii mamlaka ya waziri mhusika ukiachia mbali kusahau kuwa anaweza kuwahadaa wananchi asijue kuwa wengi wanajua msimamo wa Tanzania kuhusiana na uhuria wa kuvuka mipaka yake kwa nchi jirani? Inakuwaje Kinana anapingana na msimamo wa nchi kwa kutaka kutoa ruhusa kwa jambo ambalo bunge halijaridhia? Je hapa Kinana alilenga kuonyesha ujinga wake au jeuri yake kama siyo kuchanganya na kuingilia mamalaka ya wizara husika? Je Kinana aliongea haya kutafuta mtaji wa kisiasa na kuonekana anawajali wananchi wakati matatizo yanayowahangaisha yamesababishwa na serikali ya chama chake?
          Sehemu nyingine Kinana alipoonyesha usanii ni pale alipokaririwa akiwa wilayani Muleba akisema, “Uchangiaji wa mafuta ya Mwenge ni wa hiari, si kuwalazimisha wananchi na kusababisha Serikali kutoaminiwa na mkichangisha fedha hakikisha Mwenge huo unafika kwa wananchi wa eneo husika.” Kwanza, watendaji wengi vijijini wanatumia mbio za mwenge si kuchangisha pesa ya mwenge tu bali kujipatia chao ukiachia mbali kuwanyanyasa wananchi. Na hilo si kwamba Kinana halijui. Analijua sema anawafanya watu wapumbavu tu. Pili, ukidurusu kauli ya Kinana kwenye kipengele kinachosema, “mkichangisha fedha hakikisha Mwenge huo unafika kwa wananchi wa eneo husika” haelezi utaratibu unaopaswa kutumika kuchangisha. Na kwanini kuchangisha kana kwamba mwenge ni muhimu hivyo? Kwa mtu ambaye angetaka kuwasaidia wananchi tokana na mateso wanayopata na wizi wanaofanyiwa, angewakataza kuchangia mwenge.  Lakini unaposema mchangishe na kuhakikisha mwenge unafika kwa wananchi husika una maanisha nini kama hakuna shurti na wajibu fulani?
          Pamoja na Kinana kuwachukulia kama watanzania hasa wa vijijini na mikoani ni kama hamnazo, alipata habari yake mjini Bukoba alipotakiwa aeleze ni lini Meli ya MV Victoria meli pekee wanayotegemea wakazi wa mkoa huo kuwaungisha na sehemu nyingine za nchi kwa njia ya majini, alijaribu kujikanganya hadi wakamzoea. Ndipo alichukia na kukaririwa akisema, “Suala la meli itakuja lini sijui, ila kama mnataka niseme uongo nitasema kama hilo ndilo litanisaidia kutoka hapa salama, ila watakapokuja wakubwa zenu waliowatuma waambieni walete hiyo meli kwa sababu kila kitu kinakwenda kwa mipango. Rais alitamka msubiri sasa kama mmepewa elfu kumikumi ili mje mharibu mkutano haya.” Kumbe kwa Kinana wanaompinga wamepewa elfu kumi kuja kumpinga na si kupinga hoja zake zisizo na majibu au tuseme mashiko kwa kero za wananchi? Je Kinana anaweza kutoa ushahidi kuwa waliomzomea walihongwa elfu kumi? Je walihongwa na nani na kwanini linin na wapi? Je kauli ya rejareja kama hii haimuonyeshi Kinana kama mtu anayeamini katika kutoa na kupokea rushwa? Kama aliweza kuwaamuru wananchi waingie nchi jirani kwa vitambulisho tofauti na sheria ya nchi, alishindwa nini kuamuru hao waliotoa, kupokea rushwa na kutaka kuvuruga amani wachukuliwe hatua kama siyo usanii na kuwadhalilisha wananchi?
          Tutamalizia na kauli ya mwenzake, Katibu wa Itikadi na Unenezi wa CCM taifa Nape Nnauye aliyeongea utumbo kana kwamba wananchi ni wapumbavu wasiojua kupambanua. Alikaririwa akiwa wilayani Ngara akisema, “Katiba ni mradi wa wanasiasa kugawana madaraka. Ipite au isipite wakubwa hao watakuwa Dar es Salaam wakigongeana glasi huku wewe ukishuhudia kupitia runinga. Tuwaache wao waendelee na suala hilo na sisi tufanye ya kwetu.” Nnauye alikuwa akongelea vurugu zilizozuka wilayani mle wakati wa kujadili katiba mpya ambayo hata hivyo iliuawa na CCM. Ni kam alikuwa anawambia kuwa “nyinyi mlie tu” tukiamua hamna cha kufanya bali kushuhudia tukitanua nanyi mkiendelea kuumia.
          Kwa ufupi ni kwamba wapinzani wanapaswa kuzitupia macho ziara za Kinana na Nape za mara kwa mara mikoani huku wakichambua hoja zake kwa makini. Kwani anawanufaisha na kujibomoa bila kujua. Maana kauli zake nyingi humuonyesha kama anayewafanya wananchi hamnazo wakati wanazo.
Chanzo: Dira Juni 25, 2015.

Tuesday, 23 June 2015

Kijiwe chasikitika kutoagwa


          Baada ya munene kuanza kujivinjari ughaibuni na kidosho chake na marafiki, washirika, wapambe, ndugu, na waramba makalio wake, Kijiwe kimestuka na kuonyesha hasira zake dhidi ya ujidhalilishaji, na udhalilishaji huu wa kujitakia.
          Mpemba ndiye analianzisha leo. Anaamkua na kusema, “Jamani mmesikia kuwa jamaa yetu Njaa Kaya kenda zake Ulaya na ugabacholini kuwaaga utadhani sie tuliomchagua hatuna thamani? Huyu jamaa kaingiliwa na nini yakhe?”
          Kanji kaguswa pabaya! Anakwanyua mic na kulalama, “Pemba veve nafanya mbaya sana bwana. Kama kuu nakwenda Bombei aga veve nahusu nini? Veve taka aage mke yako?”
          Mpemba anajibu mapigo tena akiwa anaonyesha kuchukia kidogo. Anasema, “Tuheshimiane Kanji kabla sijakuita gabacholi bure ingawa wote wale wale. Kwani kosa langu nini yakhe au kusema ule ukweli nionao kama npiga kura wa kaya hii?”
          Mgosi Machungi naye hajivungi. Anakula mic, “Hapa azima tiambizane ukwei tena ukwei mtupu. Kama aivosema Ami anachofanya jamaa yetu ni udhaiiishaji wa kujitakia. Kwanini aage ughaibuni wakati sisi tiliompa kula atiache kana kwamba hatina thamani? Oh tate nane hii si haki waahi.”
          Msomi Mkatatamaa anakatua mic, “Mie sishangai. Kimsingi, huyu  jamaa  hakuwa rahis wa kaya bali rahis wa ughaibuni aliyekesha na kushinda kwenye pipa akienda kuzurura hadi akaitwa Vasco da Gama. Ukisikia utumwa wa kujitakia utokanao na kutojiamini na ukoloni mamboleo ndiyo hivi. Sijui atakapotundika jezi atazurura vipi na kutanua bure. Heri, akawaage hao aliowafurahisha na kuwafaidi kuliko sisi aliotuudhi na kutusikinisha. Aende mwana kwenda tu.”
          Mijjinga anakatua mic huku akiweka ki-sumsung chake mezani ili kila mtu akione kilivo cha bei mbaya, “Nakubaliana na wasemaji wote waliotangulia. Heri akitoe lau njuluku zetu zipone. Maana alivyozitumia kwa kutanua na kuzurura hukuk akiwapa tafu mafisadi wenzake mwenzenu sina hamu. Heri atokomee mwana kutokomea tunusuru heshima na njuluku zetu au vipi?
          Kapende, kama kawaida yake anakandia, “Hakuna haja ya kumshangaa wala kumlalamikia jamaa. Kama aliendesha kaya kwa kubomubomu, kwanini asiwashukuru washitili wake? Isitoshe, asipokwenda kule kupewa ten per cent yake mnadhani atakula mafi yake baada ya kustaafu?”
          “Mkuu unakosea. Atakuwa analipwa mabilioni ya kustaafu baada ya kutuchuuza. Huoni Tunituni Ben anavyozidi kuchana utadhani anataka kujaa kwenye ramani ya kaya?” Anachomekea Mipawa.
          Mheshimiwa Bwege anakatua mic huku akimtazama Sofia Lion aka Kanungaembe ambaye anaonekana kutopendezwa na mada ya leo. Anakula mic, “Mijitu isiyoridhika hata ikilipwa matrilioni bado itataka mengine.  Lazima jamaa akaage ili wamkatie kitu kidogo ili baada ya kutundika jezi lau apate pesa ya kuzururia kama kawa. Kosa tunalofanya ni kudhani kuwa tunapochagua mafisadi wanageuka kuwa wenzetu au marahis wetu. Wenzenu wanatafuta ulaji ili wakale na hao mabwana zao wanaowaaga wakati wakitusaza sisi.”
                    Sofi kapata mwanya na sababu. Anakwanyua mic, “Siku zote nawambia. Mtakufa bure kwa vijiba vya roho. Mlitaka awaage nyinyi na majungu yenu? Kwanza, hawaamini mnaweza kumdhuru licha ya kuweza kumzomea.”
          Kabla ya kuendelea Mbwamwitu anamchomekea Sofi, “Walitaka azomewe kama Kinamna alivyozomewa na akina Nshomile baada ya kuleta rongorongo kuhusiana na meli yao na kucheza makidamakida na uhai wao siyo?”
          Msomi anaamua kurejea, “Mie nadhani jamaa amejivua nguo kutuonyesha tulivyokuwa tukifanya makosa tukidhani yeye ni bosi wakati ni kibaraka wa hizo kaya anazokwenda kuaga. Sitashangaa kusikia akisema eti anakwenda kumuaga Obamiza wakati hamtaki hata kumuona. Hata hivyo, tusishangae wala kulalamika sana. Kama mzee Mchonga alikuwa na hatukuona wasaudia kuja kuhani msiba wake lakini yeye kwa kimbelembele na kiherehere chake akijitia kwenda kule eti kuhami msiba wa falme lao. Anadhani jamaa wanamjali wala ku-appreciate kujipeleka kwake? Mie nadhani jamaa anatafuta per diem zaidi ukiachia mbali kutanua mara ya mwisho kwa kodi za wachovu aliowasaliti na kuwachuuza.”
          Mijjinga naye anarejea tena, “Usemayo profesa Msomi ni kweli tupu. Nadhani hapa kuna somo kubwa kuwa next time watuchague sisi wenye rekodi ya kutopenda kuzurura wala kuabudia wageni. Hii tisa, kumi ni atakaporudi utamuona amezungukwa na magabacholi na mafisadi wakimpa zawadi kwa kuwawezesha kutuibia mchana kweupe. Mie wala sishangai wala kuona ajabu. Huyu ni wa hovyo hivyo kama anavyoonyesha. Ama kweli mwanaharamu ni mwanaharamu hata umtie kwenye chupa shurti ainua kidole!”
          Mzee Maneno naye hataki kupitwa. Anakula mic, “Nadhani sisi kama wapingaji wa kweli lazima tujiandae kutumia mazabe yake haya kuwakaanga wenzake wanaokaangana wakitaka kuchukua ulaji tena ili watuuze utumwani kama siyo kutuchinja. Kaya inatuhitaji kwa sasa kuliko wakati wowote ndugu zanguni.”
          Kapende anadakia mic, “Hapo umesema mkuu.  Lazima mwaka huu mzee mzima aingie ikuu na kuipiga deki huku akiwanyongelea mbali mafisadi na jamaa yetu akiwemo bila kumsahau Tunituni.”
          “Wewe umeua!” Anachomekea Mchunguliaji aliyekuwa akisoma gazeti.
          Kijiwe kikiwa kinanoga si tukasikia kelele za mdege wenye mafua ukirejesha aibu yetu. Tuliondoka haraka haraka kwenda barabara ya Uindependence kumzomea jamaa akifika na msafara wa walaji na wezi na mafisadi wenzake!
Chanzo: Tanzania Daima Juni 24, 2015.

Monday, 22 June 2015

Kikwete anapokwenda kuaga Ulaya!

  • ... Finland wakati wa dhifa iliyoandaliwa kwa hashima yake jijini Helsinki
                   Hivi karibuni vyombo vya habari vilimkariri rais Jakaya Kikwete akiwa ziarani Ulaya Magharibi aliposema eti alikwenda kuaga. Kitendo hiki japo kinaweza konakena kama cha kawaida, kina maana zaidi yale yanayoweza kuonekana juu. Kwa wenye akili wanajiuliza: Inakuwaje rais achaguliwe Tanzania, aanze kwenda Ulaya kuaga kana kwamba wapiga kura wake wako kule? Je inakuwaje rais anawapa kipaumbele wazungu badala ya wapiga kura?
          Kimsingi, wakoloni walitukomesha kwa jambo moja kuu. Waliondoka lakini wakabakiza ukoloni nyuma. Waliwaachia wakoloni weusi wauendeleze na kuhakikisha Afrika inaendelea kunyonywa na kunyenyekea. Hii ndiyo maana rais anaweza kutoa kipaumbele kwa wazungu badala ya wapiga kura. Na hii si kwa wazungu tu. Jikumbushe watanzania wanavyohangaika kumchagua rais lakini baada ya kuapishwa akadakwa na makundi ya wafanyabiashara tena wengi wa kigeni wasiopiga hata kura.
          Kwa vile serikali za kiafrika huishi kwa kutegemea kuombaomba na kukopakopa, wanaozifadhili wana thamani zaidi ya wale wanaozipigia kura. Katika kitabu changu kinachotarajiwa kutoka hivi karibuni nchini Kameruni cha Africa Reunite or Perish, nimeelezea dhana kuwa Afrika lazima iwe tegemezi yenye kujigonga na kuombaomba kama ukuku ambapo kuku huzalisha mayai yenye virutubisho kibao akaishia kutoyala na badala yake akalishwa makapi na nafaka. Haiwezekani Afrika iwe na mali na raslimali nyingi lakini iendelee kuombaomba.
          Kwa wanaoujua maana ya uzalendo na uhuru wa kweli, kitendo cha rais kuwapa kipaumbele wafadhili badala wapiga kura, ni ushaidi tosha kuwa Afrika haijawahi kuwa huru. Sikumbuki waziri mkuu wa Uingereza au rais wa Marekani kuja kuwaaga waswahili kwa kuendelea kuipa serikali yake mali ghafi iliyomsaidia kukuza uchumi wa taifa lake. Sikumbuki. Je watawala wetu wanaridhikaje na udhalilishaji huu? Je tutaendelea kuwa tegemezi hadi lini kiasi cha kuridhika na udhalilishaji huu?
          Ukiangalia utawala wa Kikwete na ule uliomtangulia, unagundua kitu kimoja, ulithamini wageni kuliko wapiga kura. Sijui ni kwa sababu marais walikuwa mawaziri wa mambo ya nchi za nje au uwezo wa kuelewa hata sijui.  Rais mstaafu Benjamin Mkapa alikuwa na furaha alipokuwa nje ya nchi kuliko alivyokuwa nchini. Alifikia mahali kuwakandia waandishi wa habari wenzake wa nchini kuwa huwa hawamuulizi maswali ya kumsisimua na kumfikirisha utadhani alikuwa na usomi wa kuzidi wengine zaidi ya ulimbukeni. Hata akina profesa Ibrahim Lipumba hawawezi kuwa na ulimbukeni kama huu.
          Kikwete licha ya kuonyesha kuwa mpiga kura si chochote mbele ya mfadhili, ameacha historia kuwa rais aliyesafiri sana duniani akiandamana na watu wengi tena ambao majina yao yaligeuzwa siri kwa sababu ajuazo. Ni rais ambaye –kutokana na kupenda kusafiri sana –watani wake walimpachika jina la Vasco da Gama. Tofauti na da Gama ni kwamba, Kikwete alikuwa akienda kuomba si kwa lengo la kujikomboa kama alivyofanya da Gama aliyeenda kupora kwa lengo la kujikomba kiuchumi.
          Kitendo cha Kikwete kwenda kuaga ughaibuni –hata hivyo –kinabeba tafsiri nyingi. Wapo wanaoona kama ni uugwana wa mhusika kwenda kuwashukuru wafadhili wake kana kwamba nchi inatoweka. Wanasema hii si uungwana bali udhalilishaji kwa vile kinachosaidiwa si yeye bali ni taifa. Hivyo, anapoondoka atakuja mwingine na kumalizia. Wapo wanaoona kam alichofanya Kikwete ni kupenda kutanua tu huku akilipwa per diem na tabia ambayo watani wake wanaona aliishaijenga ya kutokaa ndani.  Alichofanya Kikwete kinakupa faida au somo gani, inategemea uko upande gani.
          Ila kwa wanaojua utegemezi wa Afrika, kitendo cha Kikwete ni kikwazo kwa uhuru na umoja wa kweli wa Afrika kwa vile kinaonyesha alivyoridhika na kuombaomba na kukopakopa. Katika kitabu nilichotaja hapo juu kuna sura nzima ya begging will nary build Africa au uombaomba hautaijenga Afrika. Kwani watawala wanapaswa kuwa na mipango na mikakati ya kutumia raslimali kuinufaisha na kuiendeleza Afrika badala ya kutegemea kuombaomba.  Katika sura hiyo mwandishi anaonyesha namna watawala wa Kiswahili wanavyopenda kuombaomba na kukopakopa bila kujali maslahi ya mataifa yao kwa vile wengi hawatakuwa madarakani wakati wa kulipa. Mwandishi anawaeleza watawala wa kiafrika kama wakoloni weusi walitumia mfumo wa jambazi wa kiingereza Fredrick Lugard wa gawanya utawale kuwatawala, kuwanyonya na kuwauza ndugu zao nao wakijiuza pia. Anatoa mifano mingi kwenye when da Gamas are in the state houses akionyesha marais wanaosifika kwa kusafiri sana barani.  Mwandishi analinganisha ziara za viongozi wa nchi tajiri na watawala wa nchi maskini na matanuzi yao.
          Ingawa rais Kikwete ana uhuru wa wapi na nani aanze kuaga, kitendo cha kuwapa kipaumbele wafadhili au tuseme wazungu haikiwezi kuwafurahisha wapiga kura waliomwezesha kuwa pale tena si kuwa pale tu bali kumwajiri. Ni bahati mbaya kuwa kwa Afrika rais si mtumishi wa umma tena bali mtumikishaji wa umma. Maana haiwezekani wakati wa kustaafu mwajiriwa akaenda kuwatembelea marafiki zake kabla ya mwajiri ambaye humpangia hata malipo baada ya kuondoka kazini. Kikwete huyu huyu anayewapa vipaumbele wazungu anasahau kuwa akistaafu ataendelea kutunzwa na kulipwa fedha ya wapiga kura na walipa kodi hawa hawa anaowapa kipaumbele cha mwisho. Kama kuaga ni dili basi ningekuwa Kikwete ningeanzia majimboni nikamalizia Ulaya kuliko kufanya tofauti.
Chanzo: Dira